TEC iandae waraka wa kusomwa makanisa yote kwa wiki sita mfululizo kuipongeza serikali kwa mkataba bora uliozingatia maslahi ya Taifa

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,262
9,714
Ndugu zangu Watanzania,

Kwanza niwapongeze sana viongozi wetu wa TEC wakiongozwa na katibu mkuu wake Dr charles kitima kuhudhuria katika Hafla ya utiaji saini wa mkataba wa uwekezaji wa kihistoria pale bandarini ,utakaoleta mapinduzi makubwa katika uendeshaji wa bandari yetu na kuchochea zaidi ufanisi na uharaka wa huduma ,ambayo itakuwa chachu ya kuwavutia wafanyabishara wengi zaidi kutumia bandari yetu,hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa Tanzania tumezungukwa na kupakana na nchi nyingi sana ,ambazo kama tukiboresha huduma na zikawa nzuri basi tutafaidika sana na mapato makubwa na manono yenye Minofu inayotokana na bandari tu.

Hivyo kwa kuzingatia kuwa awali TEC walitoa waraka uliosomwa makanisani kwa wiki sita mfululizo wakionyesha wasiwasi wao juu ya uwekezaji huo,japo serikali yetu ilikuwa imeshatutoa hofu watanzania na pia kutoa nafasi kwa yeyote mwenye maoni kuendelea kuzungumza tu bila hofu,kwa kuwa serikali ilikuwa imetega masikio kusikiliza maoni ya wananchi wote bila kujali itikadi za kisiasa,Dini,kabila,Elimu,umri,cheo n.k.

Hivyo kwa kuwa viongozi wetu hawa wa TEC wamehudhuria na kujionea namna mkataba ulivyo bora,uliozingatia maslahi ya Taifa,ustawi wa watanzania,usalama wa Taifa,uhuru wa Taifa letu na mengine mengi mazuri .nilikuwa naona ni busara na uungwana kwa TEC ikakaa Tena kuandaa waraka utakao somwa kwa wiki Sita mfululizo katika makanisa yote nchini ukiipongeza serikali yetu,kwa kuelezea namna mkataba huu ulivyo mzuri.

Kwa kuwa maktaba huu umeonyesha kikomo au muda wa mkataba kuwa ni miaka 30 tofauti na upotoshaji uliokuwepo awali wa kusema bandari yetu imetolewa bure kwa muda usio na kikomo. lakini pia kila baada ya miaka mitano kutakuwa kunafanyika tathimini juu ya utekelezaji wa kimkataba uliofanyika na mafanikio kama yamefikiwa na kukidhi matarajio,usalama kubaki mikononi mwa Taifa letu,ajira kuwafaidisha watanzania,mkataba haujahusisha bandari zote bali ni bandari ya Dar Pekee na siyo kwa gati zote,kodi zitalipwa kama kawaida,muda wa kukaa mizigo bandarini utapungua kuendana na kasi ya sasa pamoja na serikali kuwa na uhuru wa kujitoa ikiwa itaonekana kuna ukiukwaji wa kimkataba katika utekelezaji wake na ndio maana ya kufanya tathmini kila baada ya miaka mitano n.k.

Hivyo ni vyema TEC kufanya uungwana huu na uzalendo huu ili kuwatoa hofu waumini ambao walikuwa wamepandikizwa mioyoni mwao kwa kusomewa wiki Sita mfululizo.hivyo yapaswa kuondolewa hofu hii kwa kupewa Tena waraka kwa muda huohuo wa wiki Sita mfululizo.lakini pia ni jambo jema na ni njia ya kurejesha mshikamano ndani ya kanisa kwa kuwa jambo hilo lilikuwa limewagawa kwa kiasi kikubwa waumini wengi sana ,hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa waraka huo uliandaliwa na viongozi wetu pekee pasipo kuwashirikisha waumini wote wala kukutana nao kupata maoni yao.

Lakini pia nilikuwa nawaasa viongozi wetu wa Dini kwa unyenyekevu ,staha ,adabu na heshima ya hali ya juu sana kuwa wajaribu kujizuia na kuwa na subira katika mambo makubwa kabla ya kutoa jambo kwa waumini,wajaribu Kukaa na serikali na kuiomba iwape ufafanuzi wa kina juu ya jambo lolote lile,viongozi wetu watambue ya kuwa serikali yetu chini ya Rais samia ni Sikivu sanaa na ipo tayari kupokea maoni ya mtu au taasisi au kikundi chochote kile bila kizuizi au masharti.

Wasiwe wa kwanza kuleta Taharuki au sintofahamu au kuwagawa waumini,wawe wa kwanza kuliunganisha Taifa na kulileta pamoja wakati wakiendelea na juhudi za kutafuta majibu au ufafanuzi sahihi kutoka serikalini.sasa leo tumeona namna jambo hili lilivyofika mwisho na hatima nzuri yenye maslahi mapana kwa Taifa na lenye kuonyesha kuwa kulikuwa hakuna sababu ya kutunishiana misuli na serikali au kutoa nyaraka kwenda makanisani na kuleta mgawanyiko au sintofahamu au taharuki katika jamii.

Mniwie radhi nitakapokuwa nimewakoseeni heshima .mimi ni mwanadamu kama mlivyo ninyi,nimetoa ushauri kwa nia njema kabisa katika dhamira ya kulijenga Taifa letu pasipo migawanyiko au migogoro ndani ya jamii yetu.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Na nyie chawa wa ccm muandike waraka wa kuwaomba radhi watanzania usomwe kwa miezi 3 mfululizo mkijieleza kwa nini mlitaka kuwauza.
Serikali ilikwisha eleza tangia awali kuwa itakapo fika wakati wa kusaini mkataba wenyewe tutaona mambo yote yenye kuonyesha ukomo au muda wa mkataba,haki au uhuru wa serikali kujitoa,masuala ya kodi,ajira,n.k. ila nyie ndio mlikuwa hamuelewi na kushupaza shingo zenu.
 
Unaweza kudhani unajali maslahi ya taifa, kumbe unafukuzia fursa ya kujaza tumbo lako. Halafu usijidanganye kuandika mimada mirefu ukidhani watu wanasoma. Wengi wetu tunasoma title tu na kujua kinachofuatia. Hivyo okoa muda wako kwa kufanya kazi za kukuingizia kipato. Usitegemee uchawa kwakuwa huna hakika utakulipa lini.
 
Serikali ilikwisha eleza tangia awali kuwa itakapo fika wakati wa kusaini mkataba wenyewe tutaona mambo yote yenye kuonyesha ukomo au muda wa mkataba,haki au uhuru wa serikali kujitoa,masuala ya kodi,ajira,n.k. ila nyie ndio mlikuwa hamuelewi na kushupaza shingo zenu.
Kama ilikuwa ni hivyo toka awali, hayo marekebisho wanayosema wamefanya kuendana na maoni ya wananchi ni ya Nini?
 
Tutaandaa walaka.. kwa makonda super komando, mbabeli mtu mbad mdogo wake jiwe tena sukuma gang kabisa yaani myeriko tena mpestina mwenye damu ya kiyahud mjuu kuu wa Putin anaye abudu vatican...hakika Mungu wake ni mkubwaaa sana........
Big up Makonda
 
o.jpg

Naona Akhui yuko Happy sana.
 
Back
Top Bottom