Katika hili sakata la kitita cha Mafao ya matibabu nichangie kwa kuanza kusema

Hamduni

Senior Member
Apr 25, 2020
155
108
Katika hili sakata la kitita cha Mafao ya matibabu nichangie kwa kuanza kusema.

Afya ni siasa, Afya ni Biashara na Afya ni Maisha

Hakuna ubishi kuwa Serikali inapaswa kushirikiana na watoa huduma mbalimbali kutoka sekta binafsi. Katika mfumo wa afya Tanzania Serikali imekuwa imekuwa ikishirikiana na sekta binafsi na kuilea hili inufaike na pia kuhudumia wananchi. Na niwe tu muwazi katika hili Serikali imekuwa ikihitaji ustawi wa watoa huduma za afya kuendelea kuimarika kila siku.

Licha ya Serikali kuwa ndiyo yenye raslimali nyingi, yaani vifaa, watalaam, vitendanishi, miundombinu na vifaa vya tiba kwa zaidi ya asilimia 95 nchini bado umuhimu wa sekta binafsi katika huduma za afya unaonekana. Hospitali binafsi zimepata afueni ya kodi mbalimbali katika uwekezaji wao. Tunatambua hii ni sera ya Serikali katika huduma za jamii.

Kwa muktadha huo, suala linaloendelea la baina ya Mfuko wa Taifa wa Bima (NHIF) na baadhi ya hospitali binafsi linasikitisha. Kwa mujibu wa kitakwimu za matumizi ya huduma za afya nchini, watanzania zaidi ya asilimia 90 wanaokwenda hospitali wanatibiwa kama wagonjwa wa nje (Outpatient), na pia wengi wao wanatibiwa katika hospitali kuanzia ngazi ya zahanati mpaka Hospitali za Rufaa za Mkoa ambao pia wengi wao hupata matibabu katika hospitali za Serikali.

Hii ni kutokana na uhalisia kuwa sehemu kubwa ya mtawanyo wa mtandao wa hospitali uko chini ya umiliki wa Serikali. Sipingi hoja za baadhi ya wamiliki binafsi wa hospitali ila nazitazama katika jicho la utu na uhalisia. Kwa namna wanavyolichukulia hili na kuleta hofu kwa wananchi hususan wanachama wa NHIF! Je, ni mikoa mingapia Tanzania hii ina mtawanyo mzuri wa hizo hospitali binafsi tofauti na Dar es Salaam? Wananchi wangapi wanaweza kuhudumiwa na hizo hospitali kwa pesa taslimu? Jibu ni wachache.

Mwanzoni nimeeleza utayari wa Serikali kufanyakazi na sekta binafsi hususani katika sekta ya Afya. Na hili linadhirishwa na takwimu za malipo ya madai ya zinazolipwa na NHIF kwa mwaka. Hospitali hizo binafsi zinategemea malipo ya NHIF kwa asilimia 70-85. Na kiuhalisia gharama za huduma kutoka katika hizi hospitali zinakuwa juu zaidi. Jambo ambalo si sawa.

Tukubali tukatae. Tusilite siasa kwenye afya za watanzania. Tusibidhaishe afya za watanzania. Afya ni suala na huduma nyeti sana katika usalama wa Taifa. NHIF ikifa kwa sababu tumefunikwa na lindi la kutete chakula cha wachache tujue wanufaika zaidi ya milion 4,987,292 watateseka au watakosa tiba. Kwangu mimi uhai wa NHIF ni muhimu kwa ustahimilivu wa sekta ya afya na Taifa.

Leo hii, hospitali nyingi binafsi zimejenga majengo na kununua vifaa vya tiba kutokana na uwepo wa NHIF. Mfuko umekuwa ni chanzo cha kuaminika na imara cha mapato na kinachotabirika kwa hospitali zote nchini katika kipindi cha miaka 22 ya uhai wake.

Suala hili tulitazame katika mtazamo sahihi. Na si kuhemukwa. Ni hivi karibuni tu Ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Serikali zimeonyesha mianya ya upotevu wa michango ya wanachama kupitia mifumo ya tiba na ulipaji madai, leo Mfuko umekuja na tiba ya hoja za mkaguzi wananchi wanatiwa tashwishwi ya kuuzuia Mfuko kufanya kazi.

NHIF mpaka sasa imesajili vituo 9,200 na kuna Hospitali binafsi 5 tu ambazo zimegoma. Na niwakumbushe tu mkataba wa kutoa huduma kwa wagonjwa ni kati ya NHIF na Vituo vya kutolea huduma za afya si APHFTA. Lakini pia Mfuko umeshafanya jitihada za kuhakikisha wanachama wake wanapata huduma katika vituo mbadala.

Kwa mfano Mfuko unawanachama zaidi ya 2000 ambao wanaendelea na kupata huduma za kuchuja damu (dialysis) na kati ya hao wanachama 316 ambao wote wako jijini Dar es Salaam wamekuwa wakipata huduma hiyo miongoni mwa hospitali hizo. Kwa taarifa nilizonazo, Mfuko tayari umeshachukua hatua za haraka za kuwasiliana na wanufaika wake na kuwaelekeza katika vituo binafsi vinavyoendelea kutoa huduma ya kuchuja damu. Sina nia ya kuvitangaza ila kwa urahisi na maslahi ya wagonjwa ninavitaja.

Munufaika wa huduma za Mfuko ambaye yuko jijini Dar es Salaam na anahitaji huduma hizo anapaswa kwenda katika hospitali ama vituo vifuatazo; Hindu Mandal (Ilala), Muhimbili, Mloganzila, Baraka Plaza Mikocheni, Kintonka (Temeke), RRH Temeke, Cardinal Rugambwa, Seifi – Ada Estate. Huku kote kunatoa huduma kwa kutumia bima za NHIF.

Pia, nimesikitishwa na kauli ya Mwenyekiti wa APHFTA Bw. Egina Makwabe ya kutoa masaa 48 kwa wagonjwa waliopo hospitali kuondolewa. Hili si kweli, hospitali zilizopokea wagonjwa na kupata idhini ya Mfuko kuendelea kuwahudumia kabla ya tarehe ya kuanza rasmi ya Kitita cha Mwaka 2023 watapaswa kuendelea kuhudumia bila kuathiriwa na mabadiliko. Yaani waendelea kutibiwa kwa mujibu wa idhini iliyotolewa kwa mujibu wa Kitita cha matibabu cha mwaka 2016. Nadhani ndugu yangu Makwabe alipaswa kutambua hili.

Hata hivyo, wanachama wa APHFTA wana uhuru wa kuendelea kutoa huduma tofauti na hii hali inavyokuzwa wana wajibu adhimu katika jamii. Mpaka sasa kuna hospitali kubwa zinaendelea kutoa huduma kama walivyoingia mkataba na NHIF.

Pamoja na Serikali yetu kuwa na uvumilivu mkubwa, ni wakati sasa wa kuwaangalia Watoa huduma kama hawa wasio na uzalendo na kuwachukulia hatua.

"Nakupongeza sana Mhe. Ummy hakika wewe ni mpambanaji na umeonesha ukomavu wa kiasiasa"
 
Huko Afya Ummy anasemwa semwa hatoshi na ndiye chanzo cha yote

Ungemshauri ajitengue kwa afya ya watz
 
Back
Top Bottom