Vishoka wamerudi kwa kasi Uhamiaji; maafisa ubalozi wengi siyo wataalam wa sheria za nchi. Mwanamke msikivu Dr. Makakala tusaidie kuondoa hizi kero

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Kwa sasa nina miaka 59 na katika umri wangu more than 50% ya maisha yangu nimekuwa nikikimbizana kutafuta mkate nje ya Tanzania. Kukimbizana huku kumenifanya niwe nafuatilia sana masuala ya watanzania na wageni kupata huduma. Kuna watu duniani wamefanikiwa kwa kuteseka sana, wanakamatwa wanaachiwa wanakamatwa. Katika historia yangu ya kuifahamu Uhamiaji naamini Dr. Makakala ni msomi mmoja wa wapo ambaye ametumia elimu yake kubomoa mifumo ya ukiritimba ndani na taasisi hii na kuleta mifumo ambayo sasa tunaweza tunajivunia kwamba Tanzania na sisi tupo Duniani

Lakini pamoja na juhudi zake nimeanza kuona watu wanaanza kutumia vibaya mifumo huu. Wapo viongozi Uhamiaji wameondoa huduma ya first in first out. Lengo lao nikuwakaribisha vishoka kupata mwanya wakwenda kusukuma maombi ya wateja wao huku wasio na vishoka wakiendelea kuteseka.

Awali kulikuwa hakuna malalamiko ya kuchelewa kwa pasipoti, Ilala sasa hivi wateja wameanza kuondoka mikoani kwenda kuombea pasipoti Dar na ushauri huu wanapewa na maafisa baada ya kuona viongozi wengi wanakalia majalada bila kutoa huduma.

Dr. Makakala nadhani ukiomba leo upewe list ya maombi yaliyokaa mwezi au miezi miwili yapo kwa afisa mdogo na mkubwa utapata idadi kubwa kuliko unavyofikiri. Lakini wakati huo yupo mtu anapeleka maombi ya pasipoti siku hiyo hiyo na kupata bila kuwa na haraka yoyote.

Tuondolee watendaji hawa wanaotaka kuturudisha nyuma, ondoa viongozi wasiopenda kuwajibika kwenye taasisi yako tupate huduma kwa wakati. Tuondolee maafisa Ubalozini wasiopenda kutoa huduma bali wamekaa kukwamisha huduma.
Tuondolee masharti ya madereva wetu wakivuka mpaka wakirudi wanaanza upya kutafuta viapo, barua za mwajiri na pasipoti mpya za karatasi. Mhe. Rais ameshasema tusiwabane watu wetu ,huyu anayeleta masuala ya kulazimisha watanzania kila siku kupanga foleni kuomba pasipoti za muda ni nani?

Dr. Makakala nakushauri imarisha maeneo haya yafuatayo utakuwa umetusaidia sana Watanzania.

1. Napendekeza viongozi wa Uhamiaji waweke huduma ya sms na email kwenye maombi ya pasipoti. Ombi kikikamilika wateja wapate taarifa na kama kuna tatizo wateja wapate taarifa. Mbona kwenye visa na permit wateja wanapata taarifa? Kama hakuna viongozi wanaonufaika na kukosekana kwa uwazi kwanini tuendelee kwenda kupanga foleni Uhamiaji kuulizia pasipoti wakati tuna majukumu mengi?

2. Mfumo wa huduma za pasipoti uwe na first in first out na viongozi wao wawajibishwe pale inapobainika mteja amewasilisha maombi muda mrefu na hakuna hatua zilizochukuliwa. Ukiweka hii huduma kila atakayeomba pasipoti atapata kwa wakati na vishoka wataondoka. Kukosekana kwa ukaguzi wa muda wa kutoa pasipoti kunapelekea wateja kusumbuliwa na maafisa wachache na hivyo kulazimishwa washirikiane na wahalifu.

3. Mhe. Rais ametangazia wafanyabiashara wa Zambia waingie nchini siku 180; sisi wafanyabiashara wetu wanapewa pasipoti za muda ukivuka mpaka tayari imeisha muda wake. Kila siku madereva na wafanyabiashara wadogo wanalazimika kwenda Uhamiaji kuomba karatasi za kusafiria. Ondoeni hizi pasipoti za kwenda mara moja huu ni urasimu na mnapingana na Mhe. Rais katika kurahisisha biashara. Jiulizeni katika nchi zinazotuzunguka ni nani anatoa hizi pasipoti kama za kwetu? Hiki ni kikwazo kikubwa cha biashara

4. Pigeni marufuku vishoka kuingia ofisini kwenu......haiwezekani upo kaunti anakuja mtu siyo afisa anakusumbua.Piga marufuku hao watu maofisini

5. Maombi ya pasipoti ya diaspora waliopoteza pasipoti katika harakati za kutafuta maisha huku ughaibuni yapunguziwe masharti. Watu wengi waliozamia nje kupata mapasipoti ya awali ni ngumu. Legezeni masharti watu waache kuishi nje kinyemela.

6. Maafisa wengi wa Uhamiaji ubalozini naamini siyo wataalamu, watakuwa wamepelekwa vilaza kwa upendeleo aidha wa familia au vinginevyo. Majibu ya maafisa ubalozi nje siyo ya kidiplomasia na vitu vingi ukiwauliza aidha kwa simu au umefika physically utashangaa hata sheria za nchi kichwani hakuna. Pelekeni maafisa wanaoweza kutoa ushauri kwa watanzania kisheria au kitaratibu. Mhe. Rais ameonyesha kutuunga mkono diaspora ila hana rasilimali watu katika balozi wanaoweza kumsaidia tuone tunafaidika na maono yake. Kutupa special status kwetu ni progress kubwa sana kuelekea dual citizenship

Naomba nikutakie kila la heri na kupongeze sana kwa kuboresha huduma za Uhamiaji; leo wageni wanaomba visa kama wanavyoomba wakitaka kuingia Ulaya. Hii ndiyo Tanzania anayotaka kuiona Mhe. Rais , amefungua nchi ninyi watendaji kazi yenu nikuondoa vikwazo kwa watanzania na wageni. Kila la heri mdogo wangu
 
Jambo la mwisho kabisa website ya Uhamiaji kwanini haina namba za simu za kutoa malalamiko? Nimemaliza kuandika uzi huu nataka niwapigie nba hazipatika.

Email iliyopo pia hakuna Sehemu imewekwa kwamba hii inatumika kwa ajili ya waombaji wa pasipoti.

Hakuna namba wala sura za viongozi wa Uhamiaji kwenye website. Wakiweka sura za viongozi na namba zao ingesaidia sana kumpigia simu kiongozi moja kwa moja.

Hata viongozi wa mikoa hakuna namba zao.....hii ni weaknes kubwa sana kwenye utoaji wa huduma.

Transparency ni jambo jema sana na linapaswa kuanza na kuweka wazi taarifa za viongozi wa taasisi waweze kuwajibishwa na wananchi kwa majina yao.

Wananchi walimfahamu mkuu wa Uhamiaji Wa mkoa au wilaya na wakapata shida watamtaja kwa jina lake.

Boresheni website yenu tuwafahamu kwa sura na majina wanakwamisha huduma .
 
Kwa sasa nina miaka 59 na katika umri wangu more than 50% ya maisha yangu nimekuwa nikikimbizana kutafuta mkate nje ya Tanzania. Kukimbizana huku kumenifanya niwe nafuatilia sana masuala ya watanzania na wageni kupata huduma. Kuna watu duniani wamefanikiwa kwa kuteseka sana, wanakamatwa wanaachiwa wanakamatwa. Katika historia yangu ya kuifahamu Uhamiaji naamini Dr. Makakala ni msomi mmoja wa wapo ambaye ametumia elimu yake kubomoa mifumo ya ukiritimba ndani na taasisi hii na kuleta mifumo ambayo sasa tunaweza tunajivunia kwamba Tanzania na sisi tupo Duniani

Lakini pamoja na juhudi zake nimeanza kuona watu wanaanza kutumia vibaya mifumo huu. Wapo viongozi Uhamiaji wameondoa huduma ya first in first out. Lengo lao nikuwakaribisha vishoka kupata mwanya wakwenda kusukuma maombi ya wateja wao huku wasio na vishoka wakiendelea kuteseka.

Awali kulikuwa hakuna malalamiko ya kuchelewa kwa pasipoti, Ilala sasa hivi wateja wameanza kuondoka mikoani kwenda kuombea pasipoti Dar na ushauri huu wanapewa na maafisa baada ya kuona viongozi wengi wanakalia majalada bila kutoa huduma.

Dr. Makakala nadhani ukiomba leo upewe list ya maombi yaliyokaa mwezi au miezi miwili yapo kwa afisa mdogo na mkubwa utapata idadi kubwa kuliko unavyofikiri. Lakini wakati huo yupo mtu anapeleka maombi ya pasipoti siku hiyo hiyo na kupata bila kuwa na haraka yoyote.

Tuondolee watendaji hawa wanaotaka kuturudisha nyuma, ondoa viongozi wasiopenda kuwajibika kwenye taasisi yako tupate huduma kwa wakati. Tuondolee maafisa Ubalozini wasiopenda kutoa huduma bali wamekaa kukwamisha huduma.
Tuondolee masharti ya madereva wetu wakivuka mpaka wakirudi wanaanza upya kutafuta viapo, barua za mwajiri na pasipoti mpya za karatasi. Mhe. Rais ameshasema tusiwabane watu wetu ,huyu anayeleta masuala ya kulazimisha watanzania kila siku kupanga foleni kuomba pasipoti za muda ni nani?

Dr. Makakala nakushauri imarisha maeneo haya yafuatayo utakuwa umetusaidia sana Watanzania.

1. Napendekeza viongozi wa Uhamiaji waweke huduma ya sms na email kwenye maombi ya pasipoti. Ombi kikikamilika wateja wapate taarifa na kama kuna tatizo wateja wapate taarifa. Mbona kwenye visa na permit wateja wanapata taarifa? Kama hakuna viongozi wanaonufaika na kukosekana kwa uwazi kwanini tuendelee kwenda kupanga foleni Uhamiaji kuulizia pasipoti wakati tuna majukumu mengi?

2. Mfumo wa huduma za pasipoti uwe na first in first out na viongozi wao wawajibishwe pale inapobainika mteja amewasilisha maombi muda mrefu na hakuna hatua zilizochukuliwa. Ukiweka hii huduma kila atakayeomba pasipoti atapata kwa wakati na vishoka wataondoka. Kukosekana kwa ukaguzi wa muda wa kutoa pasipoti kunapelekea wateja kusumbuliwa na maafisa wachache na hivyo kulazimishwa washirikiane na wahalifu.

3. Mhe. Rais ametangazia wafanyabiashara wa Zambia waingie nchini siku 180; sisi wafanyabiashara wetu wanapewa pasipoti za muda ukivuka mpaka tayari imeisha muda wake. Kila siku madereva na wafanyabiashara wadogo wanalazimika kwenda Uhamiaji kuomba karatasi za kusafiria. Ondoeni hizi pasipoti za kwenda mara moja huu ni urasimu na mnapingana na Mhe. Rais katika kurahisisha biashara. Jiulizeni katika nchi zinazotuzunguka ni nani anatoa hizi pasipoti kama za kwetu? Hiki ni kikwazo kikubwa cha biashara

4. Pigeni marufuku vishoka kuingia ofisini kwenu......haiwezekani upo kaunti anakuja mtu siyo afisa anakusumbua.Piga marufuku hao watu maofisini

5. Maombi ya pasipoti ya diaspora waliopoteza pasipoti katika harakati za kutafuta maisha huku ughaibuni yapunguziwe masharti. Watu wengi waliozamia nje kupata mapasipoti ya awali ni ngumu. Legezeni masharti watu waache kuishi nje kinyemela.

6. Maafisa wengi wa Uhamiaji ubalozini naamini siyo wataalamu, watakuwa wamepelekwa vilaza kwa upendeleo aidha wa familia au vinginevyo. Majibu ya maafisa ubalozi nje siyo ya kidiplomasia na vitu vingi ukiwauliza aidha kwa simu au umefika physically utashangaa hata sheria za nchi kichwani hakuna. Pelekeni maafisa wanaoweza kutoa ushauri kwa watanzania kisheria au kitaratibu. Mhe. Rais ameonyesha kutuunga mkono diaspora ila hana rasilimali watu katika balozi wanaoweza kumsaidia tuone tunafaidika na maono yake. Kutupa special status kwetu ni progress kubwa sana kuelekea dual citizenship

Naomba nikutakie kila la heri na kupongeze sana kwa kuboresha huduma za Uhamiaji; leo wageni wanaomba visa kama wanavyoomba wakitaka kuingia Ulaya. Hii ndiyo Tanzania anayotaka kuiona Mhe. Rais , amefungua nchi ninyi watendaji kazi yenu nikuondoa vikwazo kwa watanzania na wageni. Kila la heri mdogo wangu
Una point mzee ila hi nchi alisha haribika huwezi kuirekebisha kwa kuandika tu, wote wanajua ila nani athubutu. JpM alijitahidi pia ila baada ya mda hayo mambo yalirudi haraka kwa njia mpya.
 
Tanzania Inazidi Kuoza Na Kunuka Uhamiaji Wapo Hapa JF Wanasonya Tu Kutema Mate. Pesa Ya Dhulma Haimpi Mtu Maendeleo Maana Lazima Ina Laana
Vishoka Huwa Hawajifichi Uongozi Hapo Ilala Unawaona Halafu Kimya
 
Ungeweza kufikisha hoja yako vizuri tu bila kujipendekeza wala kumpa sifa za uongo Mheshimiwa Rais.
Unavyotathimini diplomasia yetu na mahusiano nje ya nchi kati ya awamu iliyopita na sasa unaona ipi bora? Maisha sasa hivi yanataka viongozi wanaowaunganisha wananchi wake na Dunia. Tukumbuke watanzania wengi wameoa na kuolewa na Raia wa kigeni hivyo muda wa kujifungia nchini haupo...
 
Big up mkuu umeongea point tupu..ushauri hii nchi ilipofikia bila kutoa chochote ufanikiwi..wakati wewe unafuatilia maombi ya passport mwezi mzima wenzako wanapigiwa simu na kupelekewa majumbani kwao.
 
Unavyotathimini diplomasia yetu na mahusiano nje ya nchi kati ya awamu iliyopita na sasa unaona ipi bora? Maisha sasa hivi yanataka viongozi wanaowaunganisha wananchi wake na Dunia. Tukumbuke watanzania wengi wameoa na kuolewa na Raia wa kigeni hivyo muda wa kujifungia nchini haupo...
Awamu iliyopita ilikuwa the best.

Tunahitaji kuwa na mahusiano na nchi nyingine yanayotunufaisha sote.

Isitoshe; awamu iliyopita iliwamaliza Kurasini hawa vishoka unaowalalamikia.

2019 nilikuwa na safari ya China kwa dharula, nilipata passport ndani ya siku tatu za kazi.

Nilimaliza application kwa kuchukuliwa alama za vidole Jumatatu asubuhi, Jumatano nikaitwa kuichukua Wizara ya Mambo ya ndani pale Posta.

Sikuwa na connection wala sikutoa rushwa yoyote.
 
Awamu iliyopita ni kweli ilijaribu kupambana na hawa vishoka lakini hawakuweza kuwamaliza.

Kuna jamaa Mmalawi amaishi Tz miaka kadhaa na kufahamu kiswahili cha kuunga unga. Mwaka 2019 alienda uhamiaji na laki 3 unusu akapatapa paspot ya kitz kwa muda wa siku 2 tu.

Mungine alikuwa mkongo ila kajichanganya muda tu. Alienda pale na laki nne na elf 30 kwa muda wa siku 3 pasport ikatoka jamaa akasepea bondeni. Hiyo ilikuwa 2020 chini ya hayati Magufuli.

Hivyo rushwa, wizi na ufisadi sio rahisi kuumaliza duniani hasa Afrika. Ukiwa nje ya tukio hauwezi kujua kinachoendelea.
 
Umekiri awamu iliyopita ilikuwa the best. Huyu wa sasa hakuna anachokifanya.
 
Back
Top Bottom