Universe ni Ndogo: No light years between Planets or Galaxies

Universe ni Ndogo: No light years between Planets or Galaxies

Ulimwengu haukuwepo na ulimwengu umeanza baada ya bing bang.na kiuhalisia hakuna kinachofahamika zaidi ya laws of physics kama visababishi na nyuma ya 10exp-32 sec haijulikani nini kilikuwepo ila baada ya muda huo ulimwengu ulitanuka kwa factor ya at least 1078 katika 3 dimension. Yaani ni sawa na kutanua kitu cha 10−9 m,sawa na nusu ya molecule ya dna mpaka kufikia 10.6 light years (au 1017 au 62 trillion miles) .

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu naona unanichanganya mimi mwanafunzi.
1.Mwanzo ulisema kuwa ulimwengu ulikuwa mdogo zaidi ya atom hapo kabla ya big bang.

Nikasema kuwa hii hoja inaoneshaa kuwa kabla ya big bang ulimwengu ulikuwepo pia.
Kwa sababu kitu kuwa kidogo zaidi ya atom hiyo haidhihirishi kuwa kitu hicho hakipo,bali inadhihirisha kuwa kitu kilikuwepo lakini kilikuwa kidogo.

2.Sasa saivi unaniambia kuwa ulimwengu haukuwepo bali ulimwengu ulitokea baada ya big bang.

Sasa ni dhaahi kuwa maelezo yako ya mwanzo juu ya ulimwengu kbal ya big bang hayakuwa sahihi ama ni ubovu wangu wa kuelewa tu ?
 
hakuna kinachofahamika zaidi ya laws of physics
Hivi mkuu kati ya laws of physics na matukio ya asili kipi kilisababisha mwenze atokee ?

Hivi mfano law ya "action and reaction are always eqaul and opposite "

Hii law ndo ilianza kisha tukio la asili la kuwa kila action ina reaction ndo likafuata,au wataalamu waliona kuwa asili ya matendo iko hivyo kwamba action lazima iwe na reaction kisha ndo wakaona waweke kanuni zao ambazo marejeo yake ni matukio na kanuni za asili za tangu na tangu ?
 
Mambo mengi ya kisayansi ni ya kufikirika. Ni ya uongo.

Mtu anatengeneza imaginations zake zisizo na kichwa wala miguu tunakuja kukaririshwa na kumezeshwa.

Mfano eti Stephen Hawking alikua anaumwa akili lakini eti bado anatengeneza formula na theories sijui za black holes na mambo ya uongo uongo yasiyo na kichwa wala miguu.

Hii ilinipelekea kua na mashaka na hadithi nyingi zinazoitwa za kisayansi.
 
Hivi kumbe hata macho yanaona kitu kikishapita au baada ya kitendo kufanyika eeh
 
R
Kuelekea wapi mkuu?
Sijui nikujibuje mkuu maana kila namna ambavyo nilitaka kukujibu japo ndio majibu yenyewe yangeweza kua na ukakasi kwako ila jibu ambalo ni zuri kulingana na swali lako 🙁kuelekea machoni kwako) kwa 7bb mapaka unaona kitu jua kina mwanga ambao lazima uakisi kwako kupiti iris retina na fovea sijua kama nimevipatia ila utaelea tu haya mengne sidhani kama utayaelewa kwa7bb c ya kila m2 wengne inabidi mshangaeshangae
 
Haya makolokolo huwa yanapunguza memory space kwenye ubongo wangu tu. Mke wangu aliniuliza time travel ni nini na inafanyaje kazi, nikamwambia niliona wamepost huko JF ila haieleweki sijui kama wengine wanaielewa.


😄😄😄
 
Umejuaje hilo ?

Una tatizo moja kwenye mada mzima, kwenye masuala yoyote ya kisayansi ukijaribu kukosoa Theory ya mwanasayansi inabidi ulete mbadala wa theory yako wewe.

Umepinga theory almost zote walizotoa wadau, Critics zinaruhusiwa kwenye hizo nadharia nk ila ukikosoa kitu na kusema sikweli inabidi utuletee ukweli upi huu ndio ukomavu.
 
Una tatizo moja kwenye mada mzima, kwenye masuala yoyote ya kisayansi ukijaribu kukosoa Theory ya mwanasayansi inabidi ulete mbadala wa theory yako wewe.
Siwezi kuleta mbadala wa theory nyingine sababu, hakuna theory inayo kosoa ua kuifanya theory nyingine kuwa kweli, sababu nadharia zote zinaweza kuwa vingine.

Ndiyo maana mimi narejea katika uhalisia na Theory haina uwezo wa kutoa majibi sahihi.
Umepinga theory almost zote walizotoa wadau, Critics zinaruhusiwa kwenye hizo nadharia nk ila ukikosoa kitu na kusema sikweli inabidi utuletee ukweli upi huu ndio ukomavu.
Safi kabisa, kuna njia nyingi za kubatilisha uongo wa jambo fulani, na si lazima kuleta lule la kweli tena kwa uwazi, bali kuhoji na kukosa majibu sahihi ya nadharia hizo huonyesha wazi kabisa nadharia husika ni ya uongo.

Mathalani, ishu ya "Rotation of The Earth" , je kuna jaribio lolote ambalo limefanyika kuonyesha dunia ina zunguka ? Jibu sahihi hakuna,ukweli uko wapi ? Ukweli ni kuwa uhalisia unatuonyesha wazi kwamba dunia haizunguki ndiyo maana hatu hisi huo mzunguko wake, na kuna sababu nyingi ambazo ni uhalisia mtupu. Sasa tunapo hoji na kuwauliza wamejuaje hilo, wanatakiwa walete uhalisia na siyo nadharia sababu hakuna nadharia yoyote inayo thibitisha au kukupa ukweli wewe, kama unabisha weka nadharia yoyote unayo ijua wewe.

Kwahiyo ukweli ni kinyume chake, sababu nadharia zote zinaenda kinyume na uhalisia, na uhalisia ndiyo ukweli wenyewe, leo hii tuna ambiwa Jua halitembei lakini kila siku tunaona lina chomoza Mashariki na linazama Magharibi, huu ndiyo uhalisia, na kupingana na uhalisia ni kukataa matumizi ya AKILI.
 
Very interesting, sasa mimi halisi nakuwa wapi?
Wanasema huko nje kuna Multverse yaani universe zipo nyingi halafu zimejipanga parallel. Albert Einstein aliwahi kuja na Theory moja inadai kwamba kuna Features tunaweza kuziona huku duniani lakini source yake sio huku duniani au kwenye universe yetu. Nitatoa mifano miwili.

1. Satellite za NASA zilipopita juu ya bara la Antactica ziliface high electrons zinazotokea duniani eneo lile. Lakini walipochunguza wakaona hakuna source ya electrons pale. Wakahisi huenda electrons zile zinatokea kwenye universe nyingine ambayo iko parallel na yetu.

2. Ukienda sehemu ambayo hujawahi kwenda kabisa. Lakini nafsi inakuambia kabisa hapo uliwahi kufika na unapafahamu. Theory hiyo inadai huenda wewe huyo huyo unaishi universe nyingine na umefika hilo eneo. Pia Theory inadai mtu mmoja unaweza kuishi kwenye parallel universe huku ukawa Polisi. Kule kwenye universe nyingine wewe ni Daktari, kwenye nyingine tena wewe ni Raisi wa nchi. Ila katika different parallel universes.
 
Yawezekana leo hii huko kwao kuna advanced civilizations kama sisi tu ila they can't bridge the distance gap, hilo ndo tatizo kubwa.

Time is relative usisahau hicho kitu. Ungesoma physics in deep ungeelewa.
Kwao wakina nani?
 
Wakipata wanacho kitafuta huenda watapata faida zaidi, assume wagundue sayari yenye kuweza kusupport uhai kama dunia ilivyo, au wakundue extra terrestrial ambao wako advanced kuliko sisi yani wana teknolojia ambayo iko so advanced kiasi kwamba sisi yetu inaonekana kama enzi za mawe?
Na wewe unatuvuruga,
Watawezaje kugundua vitu vya anga na kutunufaisha wakati vitu wavionavyo ni vitu
Vilivyokwisha pita miaka bill 80 huko na vya leo watakaoviona ni watu watakaokuja kuishi mabilloni ya miaka ijayo
 
Na wewe unatuvuruga,
Watawezaje kugundua vitu vya anga na kutunufaisha wakati vitu wavionavyo ni vitu
Vilivyokwisha pita miaka bill 80 huko na vya leo watakaoviona ni watu watakaokuja kuishi mabilloni ya miaka ijayo
Kinachoaminika ni kwamba kama kuna viumbe wengine basi watakuwa na akili na uwezo kuliko sisi, huenda wako so advanced hata kusafiri millions miles within a second wataweza
 
Back
Top Bottom