Ungependa kiongozi gani aje Jukwaani kutoa majibu na ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayoendelea nchini?

Aje waziri wa afya atuelezee hili janga la macho kuwa mekundu

Limeshakuwa janga mtaani sio watoto wala watu wazima

Macho yanakuwa mekundu, yanatoa tongo tongo na machozi
 
Majaliwa, huyu hauwezi kusinzia kwani ni birudani tupu.
 
Tatizo lake muongo muongo, anaweza akatupige sound mchana kweupe.
Huyu kapitishwa shule na mzee wa soga nini PM aliyekuwa anaishi ni lowassa tuu basi nayule aliyewahifariki miaka ya nyuma ndio waliitendea kazi hio nafasi.
 
Reactions: xox
Hata Mimi huyu Mchengerwa na Ummy Mwalimu tunataka kujua na wajibu hapa maswali hasa kuhusu hospitali na vituo vya afya …naomba mumlete mmoja wapo hapo hasa wa Tamisemi !
 
Ninashauri kila kiongozi wa umma awe na verified account ya JF na ninyi JamiiForums muweke flag ya Tanzania Government ID kuanzia za viongozi wakuu hadi vitengo vya umma ambavyo mtambuka ambao wamekubali kama TRA, TANESCO na kadhalika. Tukisema tuwaalike kwenye midahalo maana yake mmegeuka kuwa Media House. Tunataka platform ibaki kama platform ya kuwafikia wahusika kwa mapana yake.

Tukipata hizo ID zao inakuwa rahisi sisi wachangiaji kuwauliza maswali na kuwatag kwenye madokezo yetu ya kila mara.
 
Walishasema mabwawa ni rainwater proof yaani maji ya mvua yamegoma kuingia mabwawani.

Sana sana tunaumiza kichwa na hao jamaa wahujumu wakubwa wa uchumi wa Tanzania
 
Protocol yake ngumu sana
 
Tunamtaka mama kizimkazi maana mawaziri wake wameshindwa sukari bei juu umeme haueleweki mawaziri wanatoa matamko watendaji hawatekelezi serikali kupitia waziri mwenye dhamana imetoa bei elekezi ila leo hii ukienda madukani bei juu, wakuu wa mikoa wapo, Wakuu wa wilaya wapo si uhuni huu tunataka mama mwenyewe shida nini makomda kawatikisa kidogo Wakurugenzi wakastuka mama anaogopa nini tikisa mawaziri wake
 
Sisi Watanzania hatuhitaji Ufafanuzi Bali tunahitaji Utatuzi WA Changamoto mbali mbali zinazotukabili ikiwemo ya Umeme,Maji, Sukari,nk

Ufafanuzi maana yake sababu or Chocho la kutokea hatuhitaji hayo tunahitaji Utendaji.Ufafanuzi umekuwa ukitolewa Kila Léo bila ufumbuzi wowote ule.
 
Hatutaki ufafanuzi tunataka marekebisho ya katiba, umeme, sukari, tume huru ya uchaguzi na hali nzuri ya maisha. Aje Mbowe atupe mstakabali wa nchi hii.
 
Kwa kuanza, binafsi ningependa aje waziri wa ujenzi pamoja na waziri wa ardhi

Nina maswali muhimu kuhusu changamoto za hizo wizara huku kwetu
 
Kwa kuanza, binafsi ningependa aje waziri wa ujenzi pamoja na waziri wa ardhi

Nina maswali muhimu kuhusu changamoto za hizo wizara huku kwetu
Nakubaliana nawe changamoto za hasa Wizara ya Ardhi. Huko mbeleni changamoto kubwa inakuja kuwa migogoro ya ardhi, hivyo ni vyema wahusika wakatujuza mikakati ya kupambana na janga hili lijalo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…