Unaolewa na hustler? Dishi limeyumba nini?

Unaolewa na hustler? Dishi limeyumba nini?

Ewe dada amka shoga yangu. Unaanzaje kuolewa na mlalahoi mwenzako? Tafuta mtu mwenye kukupa raha ya maisha; -mitoko ya nguvu, nyumba safi, usafiri poa, n.k. Siyo unaolewa na mjinga mjinga tu ana vyeti vya elimu ya juu lkn maisha ya chini. Unaambulia kuandikiwa meseji zenye maneno magumu ya kingereza tuu. Au unaolewa na mtu mwenye kifua cha mazoezi lakini hana kitu mfukoni. Huyu ataendeleza mazoezi yake kwenye mwili wako tuu.

Wenzako wakiolewa wanaenjoy eti wewe unajifariji kwamba hayo ndiyo mapenzi ya kweli. Mmh! Kweli? Unajisikiaje unapo olewa na hustler, unachakaa na kuzeeka kabla ya wakati kwasabb ya ugumu wa maisha?

Mara unakutana na classmate, choir-mate, au hata mpangaji mwenzio unakuta anazidi kuwa kijana wewe umepinda mgongo na miguu na unanuka uvundo kisa unataabika na mlalahoi anayekutesa na maisha magumu.

Eti unadanganywa tuanze maisha wote mpenzi wangu. Hii! Mkiyaanza maisha wakati mnananihino mtayakamilisha lini wakati mnaongeza shida kwa kuzaa watoto? Nenda kwa mtu mwenye maisha mazuri shosti. Acha uzwazwa.
-Umeolewa unapandishwa bodaboda ya kukodi?
-Umeolewa unaishi kwa baba mwenye nyumba?
-Umeolewa halafu mumeo ndo kwanza anatafuta kazi? Hana A wala B. Pole yako

Hivi unapokuwa unamkubalia mlalahoi wa dizaini hii unakuwa unawaza nini?

Au umevurugwa?

Wanaume masikini pishana nao round about.

HUHITAJI KUPENDWA, unapendwa na wazazi wako.
Mzuuti ntatoa sana
 
mnatukatisha tamaa ya kuoa baadae mnaanza kulialia eti wanaume wa kutuoa hawapo chunga mdomo wako
 
Siyo kweli mkuu, mlalahoi utakutana wapi na mke wa mlalahai mwenye nazo? Mfano mke Meeng nani atamgusa? Unavuja jasho kubeba magunia sokoni kila siku mwenzako anafanya shopping Ulaya.

Mume mzima anaiba hela ya chumvi akaandaye mkeka (aka-bet)
Mpaka mikeka unawekaga kweli Vyuma vimekaza pambana pambana binti
 
Sexless, maisha hayawezi kuwa sawa maana hatuko kwenye ujamaa, uchumi ni wa ubepari huu, kuna wenye nacho na wasio nacho. Hivyo basi kila binadamu kwa ubinadamu wake ana haki ya kupenda na kupendwa regardless hali yake ya kiuchumi au vinginevyo.

Ingekuwa ni just simple like that dunia ingekuwa na akina Bil gates tu!! Cha msingi ni kuwa na mtu atakayeongeza kitu ktk maisha yako. Material things zinatafutwa. Kuna aina fulani ya wanaume ambao yaani wako sharp by nature na hawahitaji msaada wamwanamke kufika mahali fulani, ila kuna wale wanaohitaji a little push ili waweze kurealize the potentials they have na kuzifanyia kazi.

Ila sasa kama ndio mmekutana wote mnaohitaji kusukumwa ndio mtabakia hapo hapo maana hakuna wa kumsaidia mwenzie. Tuliumbwa jinsia mbili kwa sababu maalumu(sio kuunganisha vikojoleo tu) tunategemeana in one way or another. Hivyo basi cha msingi hapa ni kufundishana kutokuwa comfortable ktk umasikini as hakuna anayefurahia umasikini hata kidogo, we have to push hard,very hard ili tujikwamue na angalau tukienda outing akili ziko relaxed.
(hiki cha leo kwakweli ni cha arusha sio mimi. )
Mawazo chanya Sana haya, hongera endelea kujitahidi kukomboa wanawake wenzio kama huyu mtoa mada, ambaye anahitaji ukombozi wa kifkra.
Big up espy
 
Ewe dada amka shoga yangu. Unaanzaje kuolewa na mlalahoi mwenzako? Tafuta mtu mwenye kukupa raha ya maisha; -mitoko ya nguvu, nyumba safi, usafiri poa, n.k. Siyo unaolewa na mjinga mjinga tu ana vyeti vya elimu ya juu lkn maisha ya chini. Unaambulia kuandikiwa meseji zenye maneno magumu ya kingereza tuu. Au unaolewa na mtu mwenye kifua cha mazoezi lakini hana kitu mfukoni. Huyu ataendeleza mazoezi yake kwenye mwili wako tuu.

Wenzako wakiolewa wanaenjoy eti wewe unajifariji kwamba hayo ndiyo mapenzi ya kweli. Mmh! Kweli? Unajisikiaje unapo olewa na hustler, unachakaa na kuzeeka kabla ya wakati kwasabb ya ugumu wa maisha?

Mara unakutana na classmate, choir-mate, au hata mpangaji mwenzio unakuta anazidi kuwa kijana wewe umepinda mgongo na miguu na unanuka uvundo kisa unataabika na mlalahoi anayekutesa na maisha magumu.

Eti unadanganywa tuanze maisha wote mpenzi wangu. Hii! Mkiyaanza maisha wakati mnananihino mtayakamilisha lini wakati mnaongeza shida kwa kuzaa watoto? Nenda kwa mtu mwenye maisha mazuri shosti. Acha uzwazwa.
-Umeolewa unapandishwa bodaboda ya kukodi?
-Umeolewa unaishi kwa baba mwenye nyumba?
-Umeolewa halafu mumeo ndo kwanza anatafuta kazi? Hana A wala B. Pole yako

Hivi unapokuwa unamkubalia mlalahoi wa dizaini hii unakuwa unawaza nini?

Au umevurugwa?

Wanaume masikini pishana nao round about.

HUHITAJI KUPENDWA, unapendwa na wazazi wako.
Sasa uolewe na Daudi Bashite halaf moto hakuwashii maana yake nini? Au uolewe na yule Kiongozi Mkuu lkn kila siku mangumi na kudekishwa nyumba nzima ya serikali maana yake nini???
 
Kuna stages, anajikuna anapofika, hata hao matajiri walianzia chini wakapanda juu. Leo anampeleka bar kesho atampeleka vacation Dubai( Kaboom shenzi wewe!)
Na wa hivyo mnaetengenezana hata likiharibika mahali basi kuna ile respect mnakuwa nayo to each other maana mnajua mlipotokea. Ukiikuta ready made pakiharibika ndio fimbo ya kukuchapia.

Ukimpata huyo mwenye nazo ni heri lakini pia ukimpata asie nazo lakini ana potential usimuache, mpe a shoulder to lean on ili mfikie pale unapopataka.
Teh teh..Hasira za nini mpenzi??
 
Wanaume mnakazi,kama hawa ndo dizain ya wanawake mnaoenda kuoa bas polen.

Namshukuru mungu sana niliolewa na huyo huster akiwa na kachumba na ka kitanda but now naongelea kwingine kabisaa....nina sauti ya kusema pale ninapokosewa na nikasikilizwa coz anajua tulipotoka

Akina dada msidanganywe olewa na yeyote ilimradi anajituma kuzisaka.
 
niliolewa na huyo huster akiwa na kachumba na ka kitanda but now naongelea kwingine kabisaa....
Hivi uolewe na mwanaume anayekaribia 40, halafu mnaishi wenye kachumba ka kupanga. Muanze kudunduliza mpk mkajenge nyumba atakuwa hajafa kwa uzee huyo mwanaume? Au kama yuko hai atathubutu kukutoa out wakati wote 2 mshabakia kongolo?
 
Unajitahidi sana kupotosha wenzio. Mtu mpaka awe na nyumba, gari na mkwanja mrefu. Siku zote anakuwa anakusubiri wewe gold digger?!

Pambana na hali yako la sivyo mtatumika sana.
 
Back
Top Bottom