Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,026
- 20,511
MATAMKO/MAAZIMIO YA USA NA EU YAMESAIDIA NINI WAPINZANI AFRIKA?
Kabla ya Azimio la Zanzibar la 1992, lililozaa mfumo wa vyama vingi Tanzania, kulikuweko na kitu kilichoitwa matamko na maazimio ya Marekani na nchi za Ulaya dhidi ya Tanzania, na dhidi ya nchi Afrika. Msingi wa matamko hayo ulijikita katika utawala wa sheria na demokrasia, huku Washington na Brussels zikijipa umiliki na uendeshaji wa mifumo hiyo ulimwenguni kama sera zao muhimu za mashauri ya Kigeni.
Kuenenzwa kwa mifumo hiyo ya aina ya demokrasia, kumeifanya Marekani na Ulaya kukubalika kwa wingi mweneo mengi duniani na kuzifanya nchi hizo kuwa karibu zaidi na mataifa ya ulimwengu kiasi cha kuamua siasa, uchumi na maisha ya jamii ya maitafa mengi Afrika ikiwemo Tanzania, Ndio, siasa ya Tanzania tangu kuanguka kwa Azimio la Arusha (Ujamaa) na kuzaliwa kwa Azimio la Zanzibar (Ubepari) imekuwa ikiamuliwa kwa sura na macho ya kimagharibi,
Swali ambalo wengi wa kizazi kipya tunatakiwa kujiuliza, ni je, uangalizi wa siasa na demokrasia wa Ulaya na Marekani umekuwa wa uhalisia au mpaka maslahi ya nchi hizo yaguswe ndipo dunia itashuhudia uangalizi kamili na matokeo chanya? Na Je ungalizi huu unahusu utetezi wa vyama pinzani tu au unaangalia pande zote za wadau wa siasa na demokrasia?
Maswali haya yanasimama wima kutokana na hali ya mambo ilivyo afrika dhidi ya wapinzani huku Marekani na Ulaya wakiishia kutoa tu matamko na maazimio yasiyo na maana yoyote wala kuleta matokeo chanya. Nataka nikupitishe kwa uchache Afrika na baadhi duniani uone ni kwa kiasi gani matamko au maazimio hayana msaada kwa siasa na demokrasia ya Afrika. Hadi leo 7 Mei 2026, kuna viongozi kadhaa wa upinzani Afrika walioko jela/mahabusu au wanakabiliwa na mashtaka mazito. Hawa ni baadhi tu ya wanasiasa maarufu kulingana na ripoti za hivi karibuni:
1. Nchini Tunisia Bwana Rached Ghannouchi mwenye umri wa miaka 84 ambaye ni Kiongozi wa chama cha Ennahda, Rached Ghannouchi ni mpinzani mkubwa wa Rais Kais Saied. Amefungwa tangu 2023 na amehukumiwa jumla ya miaka 70 jela kwa mashtaka ya kula njama dhidi ya usalama wa taifa, ambayo yeye anasema ni ya kisiasa. Afya yake imedorora sana na amelazwa hospitali ya gerezani. Nchini Tunisia Viongozi wengine wengi wa upinzani, waandishi na wanaharakati pia wako jela kwa tuhuma za "kula njama dhidi ya usalama wa taifa". Matamko na Maazimio ya Marekani na Ulaya hayajawa na nafasi katika Nchi Huru ya Tunisia.
2. Nchini Mali, kuna tukio la kutisha lilitokea juzi, ambapo kiongozi wa Upinzani Bwana Mountaga Tall, na wenzake Bwana Youssouf Daba Diawara, na Moussa Djire walitekwa na wanaume walikuwa wmefunika sura zao. Bwana Tall anahojiwa kwa "jaribio la kuyumbisha serikali". Tangu mapinduzi ya 2025, kuna "wimbi la ukamataji" wa wanachama wa upinzani zaidi 31. Matamko na Maazimio ya Marekani na Ulaya hayajawa na nafasi katika Nchi Huru ya Mali.
3. Nchini Chad Muungano wa upinzani unaoitwa Groupe de Concertation des Acteurs Politiques (GCAP) yaani "Kundi la Mashauriano ya Wadau wa Kisiasa" unaoongozwa na Bwana Succès Masra ambaye ni Kiongozi wa chama cha _Les Transformateurs ambaye ndie Mpinzani mkubwa wa Rais Mahamat Déby. Alishindana uchaguzi 2024. Muungano huo uliotangazwa kuwa ni haramu na Mahakama Kuu ya Chad tarehe 24 Aprili 2026, na kisha Bwana Succès Masra alikamatwa na baadaye akahukumiwa miaka 20 jela. Matamko na Maazimio ya Marekani na Ulaya hayajawa na nafasi katika Nchi Huru ya Chad.
4. Nchini Zambia Kiongozi wa upinzani Bwana Raphael Nakacinda alihukumiwa kifungo cha miezi 18. Na tahadhari imetolewa na wanasiasa akiwemo Kiongozi wa PF Bwaba Given Lubinda akisema viongozi wengi zaidi wa upinzani watafungwa kwa mashtaka "ya kutunga" kuelekea uchaguzi 2026. Matamko ya Maazimio na Marekani na Ulaya hayajawa na nafasi katika Nchi Huru ya Zambia.
5. Nchini Cameroon kiongozi wa upinzani Bwana Anicet Ekane Kiongozi wa chama cha African Movement for New Independence and Democracy (MANIDEM) alifariki 1 Desemba 2025 akiwa kizuizini baada ya kukamatwa 24 Oktoba 2025 baada ya uchaguzi wa urais ulioibua maandamano. Uchaguzi ulimtangaza Rais Paul Biya, 92, kushinda muhula wake wa nane. Anicet alifariki 1 Desemba 2025 akiwa kizuizini katika Kituo cha Ulinzi cha Serikali (SED) jijini Yaoundé. Familia yake na mawakili wake wanasema alikuwa na shida ya kupumua kabla ya kukamatwa. Afya yake ilidhoofika haraka gerezani na alinyimwa matibabu sahihi licha ya maombi ya mara kwa mara.
Baada ya uchaguzi, serikali ilikamata watu wengi wa upinzani na waandamanaji kwa tuhuma za kuhatarisha usalama wa Taifa. Human Rights Watch inasema kifo chake kinaonyesha tatizo la haki na utunzaji wa wafungwa Cameroon. Kuna viongozi wengine wa upinzani nchini Cameroon kama Maurice Kamto, mpinzani mwingine John Fru Ndi alifariki Juni 2023 akiwa nje ya gereza lakini kifo kikihusishwa na shinikizo la utawala wa Biya. Matamko na Maazimio ya Marekani na Ulaya hayajawa na nafasi katika Nchi Huru ya Cameroon.
6. Nchini Afrika Kusini kiongozi wa upinzani bwana Julius Malema ambaye ni kiongozi wa EFF alihukumiwa miaka 5 jela kwa kumiliki bunduki na kufyatua risasi hadharani 2018. Wakili wake anakata rufaa na hivyo utekelezaji wa hukumu hiyo umesimama ukisubiri rufaa. Matamko na Maazimio ya Marekani na Ulaya hayajawa na nafasi katika Nchi Huru ya Afrika Kusini.
7. Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bwana Anicet Georges Dologuele ambaye ni Waziri Mkuu wa zamani na mpinzani mkubwa. Mei 6, 2026 alizuiwa kusafiri kwa kisingizio kuwa amepoteza uraia. Kwamba Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, amemfutia uraia wa nchi hiyo kiongozi huyo wa upinzani. Matamko ya Maazimio na Marekani na Ulaya hayajawa na nafasi katika Nchi Huru ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.
8. Nchini Uganda kiongozi wa upinzani wa muda mrefu Dr Kizza Besygey alikamatwa Nairobi nchini Kenya Novemba 2024 na kushtakiwa katika Mahakama ya Kijeshi, Mahakama Kuu ya Uganda iliamua raia hapaswi kuhukumiwa na mahakama za kijeshi. Kesi ikahamishiwa Mahakama ya Kiraia.
Aliachiliwa kwa dhamana baada ya kufanya mgomo wa kula gerezani kwa wiki kadhaa. Mahakama ilimpa dhamana kali akiwemo kuripoti polisi kila mwezi. Kesi yake ya uhaini na kumiliki silaha bado inaendelea Mahakama ya Kiraia Kampala. Ingawa yuko nje kwa dhamana, amezuiwa kusafiri nje ya Uganda bila kibali cha mahakama na amepigwa marufuku kukutana, kuzungumza ama kuhutubia mikutano ya kisiasa popote bila kibali cha mahakama. Kwa lugha rahisi ni kama yuko kifungoni tu. Matamko na Maazimio ya Marekani na Ulaya hayajawa na nafasi katika Nchi Huru ya Uganda.
9. Twende Ulaya/Mashariki ya Mbali, sasa tuone kama Matamko na Maazimio ya Marekani na Ulaya yana nafasi gani katika Nchi Huru. Baada ya mapinduzi ya kijeshi ya 1 Februari 2021, Aliyekuwa Kiongozi wa Nchi hiyo Bi Aung San Suu Kyi ambaye pia ni kiongozi wa Chama cha National League for Democracy (NLD) alifunguliwa mashtaka mengi na jeshi la Myanmar.
Bi Aung San Suu Kyi alishitakiwa kwa kesi zifuatazo;
Kesi ya kwanza ni kesi ya Ufisadi ambapo alituhumiwa kupokea rushwa ya dhahabu na dola $600,000 kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Yangon.
Ambapo alipatikana na hatia na kuhukumiwa Miaka 5 jela Disemba 2022. Kesi ya pili ilikuwa ni Kukiuka Sheria za Siri za Nchi, ambapo alituhumiwa Kumiliki vifaa vya mawasiliano vilivyoagizwa kinyume cha sheria, ikiwemo radio call (walkie-talkies).
Alipatikana na hatia na kuhukumiwa Miaka 4 jela Januari 2022, baadaye ikapunguzwa kuwa miaka 2.
Kesi ya tatu ilihusu Kuchochea Machafuko, ambapo alituhumiwa Kuchapisha mitandaoni taarifa zinazosababisha hofu kwa umma na kuchochea chuki dhidi ya jeshi. Alipatikana na hatia na kuhukumiwa Miaka 2 jela Disemba 2021. Kesi ya nne ilihusu Kukiuka Kanuni za COVID-19, ambapo aliuhumiwa Kukiuka masharti ya COVID wakati wa kampeni za uchaguzi 2020. Alipatikaa na hatia na kuhukumiwa Miaka 4 jela, baadaye ikapunguzwa kuwa miaka 2.
Kesi ya tano ilihusu Udanganyifu wa Uchaguzi, ambapo alituhumiwa Kuhusika na udanganyifu katika uchaguzi mkuu wa 2020 ambao chama chake NLD kilishinda kwa kishindo. Alipatikana na hatia na kuhukumiwa Miaka 3 jela na kazi ngumu Septemba 2022. Hadi kufikia Disemba 2022, alikuwa amehukumiwa kifungo cha jumla ya “miaka 33 jela. Baadaye Agosti 2023, jeshi lilipunguza miaka 6 kama sehemu ya msamaha, hivyo hukumu ikabaki miaka 27. Mwezi Mei 2026 amepunguziwa kifungo hadi miaka 18. UN na nchi nyingi za Magharibi zinasema kesi hizo ni za kisiasa na lengo ni kumzuia asirudi madarakani. Jeshi la Myanmar linasisitiza kesi ni halali. Matamko na Maazimio ya Marekani na Ulaya hayajawa na nafasi katika Nchi Huru ya Mynmar.
Kwa nadharia hii tata, ni kwamba takriban nchi 9 zina viongozi wakuu wa upinzani walio gerezani, mahabusu, au wanazuiliwa katika vituo vya polisi. Idadi halisi ya wote ni zaidi ya 300 ukihesabu wabunge, madiwani na viongozi wa ngazi za chini. Mashirika kama Amnesty International na Human Rights Watch ambayo kwa sehemu kubwa yanatuhumiwa na serikali nyingi za Afrika na Mashariki ya Mbali kufadhiri maasi na machafuko ya yanasema nchi nyingi zinatumia mahakama na mashtaka ya uhaini kunyamazisha upinzani kabla ya uchaguzi.
Mjadala mkubwa wa dunia ya siasa za kidemokrasia, ni aina gani ya siasa za upinzani zinaweza kufanyika na upinzani kuingia madarakani bila mapito hayo magumu ambayo yanafunga kabisa milango kwa upinzani? Kwa sehemu kubwa jibu liko Zanzibar lililoasisiwa na Hati Maalim Seif Sharif na Amani Abeid Karimu, Ni siasa za Mezani, ni Siasa za Maridhiano ndizo zitaepusha vifungo na mapito magumu kwa wapinzania. Ni siasa za Maalim Seif ndizo zilivuka bahari na Kutua Nairobi Kenya zikatuama mikononi mwa Raila Odinga na Uhuru Kenyata. Ni siasa za maridhiano za Maalim Seif ndizo zilimfanya Freeman Mbwe abadilli aina ya siasa za chake Chadema na kuwa za mazungumzo na Maridhiano na serikali, kabla wanaharakati hawajavamia chama hichi na kukitwaa na kukirejesha nyuma kabisa kilikokuwa kimetoka miaka 22 nyuma ambako kimsingi ilikuwa ni njia ya kifo. Aina hiyo ya siasa ndio CHAUMMA kimeibeba kama alama ya siasa mpya za Tanzania.
Watawala Afrika na kwingineko duniani hawatishwi na matamko ya hawa wazungu ambao kwanza wamehakikishiwa maslahi yao Afrika yako salama, Pili wana amini dunia huru inawabeba kwakuwa siasa zilizopo duniani sasa ni za MADARAKA sio za Ukombozi kama wanaharakati wanavyofikiri, Na hivyo Wazungu wanamwamini aliyeko madarakani na wanamtii kulinda maslahi yao kwanza, matamko mengi ni geresha yasiyoweza kusaidia upinzani kushika dola!
Kwa nadharia hiyo, Hakuna njia ya mkato kwa vyama haisi vya upinzani Afrika itakayowafanya washike madaraka isipokuwa Meza ya MAZUGUZO NA MARIDHIANO, nje ya hapo tutaozea katika jela za Afrika huku Watawala wakiendelea kutawala wakipokezana wao kwa wao!
Na Yericko Nyerere