Unaolewa na hustler? Dishi limeyumba nini?

Unaolewa na hustler? Dishi limeyumba nini?

Halafu hii tabia ya kudharau wanaume maskini sio nzuri kabisa...wewe sio mpangaji wa riziki maisha ni kutafuta mkuu, kwa hiyo usifikiri kila aliyeolewa na 'hustler' mwisho wake huwa mbaya.

Ajuae ya leo na kesho ni Mola mkuu
Hahahaaaa! Pambana na hali yako josee.
 
Ewe dada amka shoga yangu. Unaanzaje kuolewa na mlalahoi mwenzako? Tafuta mtu mwenye kukupa raha ya maisha; -mitoko ya nguvu, nyumba safi, usafiri poa, n.k. Siyo unaolewa na mjinga mjinga tu ana vyeti vya elimu ya juu lkn maisha ya chini. Unaambulia kuandikiwa meseji zenye maneno magumu ya kingereza tuuu. Au unaolewa na mtu mwenye kifua cha mazoezi lkn hana kitu mfukoni. Huyu ataendeleza mazoezi yake kwenye mwili wako tuuu.

Wenzako wakiolewa wanaenjoy eti wewe unajifariji kwamba hayo ndiyo mapenzi ya kweli. Mmh!! Kweli?? Unajisikiaje unapo olewa na hustler, unachakaa na kuzeeka kabla ya wakati kwasabb ya ugumu wa maisha? Mara unakutana na classmate, choir-mate, au hata mpangaji mwenzio unakuta anazidi kuwa kijana wewe umepinda mgongo na miguu na unanuka uvundo kisa unataabika na mlalahoi anayekutesa na maisha magumu.

Eti unadanganywa tuanze maisha wote mpenzi wangu. Hii!!!! Mkiyaanza maisha wakati mna nanihino mtayakamilisha lini wakati mnaongeza shida kwa kuzaa watoto? Nenda kwa mtu mwenye maisha mazuri shosti. Acha uzwazwa.
-Umeolewa unapandishwa bodaboda ya kukodi?
-Umeolewa unaishi kwa baba mwenye nyumba?
-Umeolewa halafu mumeo ndo kwanza anatafuta kazi? Hana A wala B. Pole yako

Hivi unapokuwa unamkubalia mlalahoi wa dizaini hii unakuwa unawaza nn? Au umevurugwa?

Wanaume maskini pishana nao round about.

HUHITAJI KUPENDWA, unapendwa na Wazazi wako.
Umelaaniwa wewep
 
Sexless, maisha hayawezi kuwa sawa maana hatuko kwenye ujamaa, uchumi ni wa ubepari huu, kuna wenye nacho na wasio nacho. Hivyo basi kila binadamu kwa ubinadamu wake ana haki ya kupenda na kupendwa regardless hali yake ya kiuchumi au vinginevyo.

Ingekuwa ni just simple like that dunia ingekuwa na akina Bil gates tu!! Cha msingi ni kuwa na mtu atakayeongeza kitu ktk maisha yako. Material things zinatafutwa. Kuna aina fulani ya wanaume ambao yaani wako sharp by nature na hawahitaji msaada wamwanamke kufika mahali fulani, ila kuna wale wanaohitaji a little push ili waweze kurealize the potentials they have na kuzifanyia kazi.

Ila sasa kama ndio mmekutana wote mnaohitaji kusukumwa ndio mtabakia hapo hapo maana hakuna wa kumsaidia mwenzie. Tuliumbwa jinsia mbili kwa sababu maalumu(sio kuunganisha vikojoleo tu) tunategemeana in one way or another. Hivyo basi cha msingi hapa ni kufundishana kutokuwa comfortable ktk umasikini as hakuna anayefurahia umasikini hata kidogo, we have to push hard,very hard ili tujikwamue na angalau tukienda outing akili ziko relaxed.
(hiki cha leo kwakweli ni cha arusha sio mimi. )
 
Back
Top Bottom