Ewe dada amka shoga yangu. Unaanzaje kuolewa na mlalahoi mwenzako? Tafuta mtu mwenye kukupa raha ya maisha; -mitoko ya nguvu, nyumba safi, usafiri poa, n.k. Siyo unaolewa na mjinga mjinga tu ana vyeti vya elimu ya juu lkn maisha ya chini. Unaambulia kuandikiwa meseji zenye maneno magumu ya kingereza tuu. Au unaolewa na mtu mwenye kifua cha mazoezi lakini hana kitu mfukoni. Huyu ataendeleza mazoezi yake kwenye mwili wako tuu.
Wenzako wakiolewa wanaenjoy eti wewe unajifariji kwamba hayo ndiyo mapenzi ya kweli. Mmh! Kweli? Unajisikiaje unapo olewa na hustler, unachakaa na kuzeeka kabla ya wakati kwasabb ya ugumu wa maisha?
Mara unakutana na classmate, choir-mate, au hata mpangaji mwenzio unakuta anazidi kuwa kijana wewe umepinda mgongo na miguu na unanuka uvundo kisa unataabika na mlalahoi anayekutesa na maisha magumu.
Eti unadanganywa tuanze maisha wote mpenzi wangu. Hii! Mkiyaanza maisha wakati mnananihino mtayakamilisha lini wakati mnaongeza shida kwa kuzaa watoto? Nenda kwa mtu mwenye maisha mazuri shosti. Acha uzwazwa.
-Umeolewa unapandishwa bodaboda ya kukodi?
-Umeolewa unaishi kwa baba mwenye nyumba?
-Umeolewa halafu mumeo ndo kwanza anatafuta kazi? Hana A wala B. Pole yako
Hivi unapokuwa unamkubalia mlalahoi wa dizaini hii unakuwa unawaza nini?
Au umevurugwa?
Wanaume masikini pishana nao round about.
HUHITAJI KUPENDWA, unapendwa na wazazi wako.