Unamiliki nini katika Umri huu?

Unamiliki nini katika Umri huu?

Umesahau kusema kama unajimiliki wewe mwenyewe au unamilikiwa!
 
Waungwana wa humu, hapa nina wazo la kijinga tu hapa. Lakini ndo JF ilivyo hata ukiwa na pumba watu wataisoma tu. Mfano mimi nimewaza niandike kila atakaye pitia uzi huu utaje kwanza Umri wako na mali ulizonazo hadi kufikia umri wako. Au kama ulishazipoteza kwa ujinga wako au bahati mbaya.
Kwangu mimi naanza hivi japo sijafanikiwa sana katika maisha kwa jinsi nilivyojipangia kuwa.

Nina umri wa miaka 42.
Nina mke na watoto watatu, japo nishakuwaga na michepuko, ila nshaipiga chini.
Nina kaduka ka mtaani kadogo japo kananiingizia kakipato kwa kula mboga na ugali.
Nina kagari kadogo ka kirikuu nilikaagizaga japan.
Nina pikipiki ya kijapan used inanisadia visafari vyangu vya hapa na pale.
Nishawahi kununua pikipiki pia za kichina kama Fekon na Sanlg.

Nimefanikiwa kujenga nyumba ambayo thamani yake imefika 32Mln.
Nina vitu vya nyumani vingi tu kama Set ya kochi za mbao za kizamani za mninga, vitanda kama vinne vya mbao, tv Samsung 32"flat panel HD, Sony 5.1channel hone theatre,Jiko la umeme na gas, fridge Juba la kikorea, ving'amuzi vya dstv vitatu, Azam kimoja na madish yake, nina dish kubwa la nchi 6, vifaa vya kazi kama grinder, drill sander, nina simu ya sumsung, ipad ya apple, laptop toshiba, printer ya samsung laserjet, na vungine vingi vidogo dogo kama blender, juice dispencer nk.
Huu ni ujinga wangu naojisikia kuandika kwa leo. Hebu tuletee na wakwako pia ili tujilinganishe mafanikio yako hadi katika umri ulio nao.

Maana wengine umri mdogo wana mali za mamilioni wengine umri mkubwa wana mali za maelfu na wengine hawana kabisa hela zinaishia kula.
Kwa kifupi mafanikio yangu yametokana na ubahili wangu, sinywi pombe wala kula bata. Hata pamba za bei mbaya za dukani sivai kwa sababu sina pesa za kufanya hayo, la sivyo nitachekwa. Nakomaa sana kwenye kazi lakini napata vihela vidogo sana
Natamani niweze kujenga ghorofa lenye swimming pool na kuendesha magari kama rangerover, au wagon yoyote kali. Natamani nipate mchongo utakaonipa pesa nika enjoy utalii sehemu mbali mbali ninazotaka duniani. Maana maisha ni mafupi afu duniani kuna raha sana.
bila shaka utakuwa mhaya wewe
 
ukiona you are above 35 na bado unapost JF jua unatatizo kubwa sana la msingi.
 
Ukitaka mke najitolea.
Nina 30, namiliki nyumba mbili moja ipo kibaha kwa mathias, nyingne ipo morogoro nane nane, nina gari nne (ranger nyeusi, harrier, noah , na spacio), sina mke, sina mtoto, sasa hvi najenga ghorofa moja kimara, nina mashamba ekari 22, nina biashara yangu kubwa tu ambayo inasogeza siku, ni machine za kusaga za kukoboa, nina viwanja viwili. Katika elimu nina degree moja, na sasa hv ninatarajia kusoma masters kwaajili ya sifa tu, si unajua sisi wahaya. Ni hayo tu.
 
Kumbe we ndo admin wa pachu pachu eeh? Makonda anakutafuta sana.
Ila comments zako zinaniuaga mbavu
Nina miaka 23.

Namiliki grupu la whatsapp la PachuPachu, Msingi Kiuno, na ZaUchiZoteHapa.

Nina sabwufa limeharibika sehemu ya flash na pini ya waya imekatikia kwenye tundu.

Nasikia nilikabidhiwa viwanja kijijini kwetu ila sijawahi hata kuviona na kwenda kijijini sitaki.

Nina wanawake wanne wa kudumu na watatu ni occasional.

Sina chumba wala nyumba nalala kwa rafiki yangu Dilongele.

Nina elimu kidogo ya form six.

Pia nina nyege.
 
Watu bana kama unamiliki hvyo vitu nani kakuambia ndio furaha, furaha mmiliki yesu hata ukifa utaishi, unafurahia kumiliki jalala la vitu, ambavyo ukfa unavitipa jalalani
 
Umri miaka 59. Namiliki uhuru wa kujitanafas kwenye JF. Mengine we acha tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom