Unamiliki nini katika Umri huu?

Unamiliki nini katika Umri huu?

Umri wangu ni miaka 40..
Namiliki baiskeli moja aina ya swala,
Kichwa cha cherehani cha singer,
Stuli 3 na ngoma kubwa za ngozi,,
Kitanda cha kasuku 4/6,
Godoro na mito 2 ya Sufi..
Maua ya plastic 3,
Feni moja Philips,,
Radio aina ya Sanyo,
Pasi ya mkaa,,
Jiko la stove,
Taa ya kandili,,
Kabati la vyombo ,,droo zake zipo juu pembeni lina nyavu..
Kombe kubwa la bati,,
Ndoo 3 za bati,,
Kandambili za mgogo pair 1..
Dah.... Masikini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waungwana wa humu, hapa nina wazo la kijinga tu hapa. Lakini ndio JF ilivyo hata ukiwa na pumba watu wataisoma tu. Mfano mimi nimewaza niandike kila atakayepitia uzi huu utaje kwanza Umri wako na mali ulizonazo hadi kufikia umri wako. Au kama ulishazipoteza kwa ujinga wako au bahati mbaya.
Kwangu mimi naanza hivi japo sijafanikiwa sana katika maisha kwa jinsi nilivyojipangia kuwa.

Nina umri wa miaka 42.
Nina mke na watoto watatu, japo nishakuwaga na michepuko, ila nishaipiga chini.
Nina kaduka ka mtaani kadogo japo kananiingizia kakipato kwa kula mboga na ugali.
Nina kagari kadogo ka kirikuu nilikaagizaga Japan.
Nina pikipiki ya kijapan used inanisadia visafari vyangu vya hapa na pale.
Nishawahi kununua pikipiki pia za kichina kama Fekon na Sanlg.

Nimefanikiwa kujenga nyumba ambayo thamani yake imefika 32Mln.
Nina vitu vya nyumbani vingi tu kama set ya kochi za mbao za kizamani za mninga, vitanda kama vinne vya mbao, TV Samsung 32"flat panel HD, Sony 5.1 channel home theatre, Jiko la umeme na gas, fridge Juba la kikorea, ving'amuzi vya dstv vitatu, Azam kimoja na madish yake, nina dish kubwa la nchi 6, vifaa vya kazi kama grinder, drill sander, nina simu ya sumsung, ipad ya apple, laptop toshiba, printer ya samsung laserjet, na vingine vingi vidogo dogo kama blender, juice dispencer nk.
Huu ni ujinga wangu ninaojisikia kuandika kwa leo. Hebu tuletee na wakwako pia ili tujilinganishe mafanikio yako hadi katika umri ulio nao.

Maana wengine umri mdogo wana mali za mamilioni wengine umri mkubwa wana mali za maelfu na wengine hawana kabisa hela zinaishia kula.

Kwa kifupi mafanikio yangu yametokana na ubahili wangu, sinywi pombe wala kula bata. Hata pamba za bei mbaya za dukani sivai kwa sababu sina pesa za kufanya hayo, la sivyo nitachekwa. Nakomaa sana kwenye kazi lakini napata vihela vidogo sana.

Natamani niweze kujenga ghorofa lenye swimming pool na kuendesha magari kama range rover au wagon yoyote kali. Natamani nipate mchongo utakaonipa pesa nika enjoy utalii sehemu mbali mbali ninazotaka duniani. Maana maisha ni mafupi alafu duniani kuna raha sana.
bodaboda na simu ya tecno
 
.....Ndio Maana Nguli wetu Ally Choki aliimba:
..Ukitaka kujua Password yake ya email atakupa hata ukitaka ya Benki, lakini kamwe hawezi kukupa Password ya Maisha yake!!....
 
Hongera sana umefanya jambo la kawaida kabisa la basic need
 
Miaka 58
Mke mmoja watoto wa ndoa 6
Watoto wa pembeni 5 niliwachukuaga ninao home - jumla ya watoto 11
Nina kiwanja...tofali zipo site mwaka wa pili sasa ila kupandisha mambo yamegoma
Nimepanga nyumba nzima...Tandare kwa Mtogole
Sijawahi kumiliki gari...ila nina pikipiki wa ajili ya safari zangu na familia
Nina kibarua Tshs 540,000 kwa mwezi
Watoto 3 wasichana wamezalia home....wapo
Watoto wengine 3 wa kiume, mmoja Dj kwenye bar, Mwingine bodaboda na mwingine yupo home tu hata sijui shughuli zake
Shemeji zangu wawili kaka za wife nipo nao, mmoja dereva wa daladala, mwingine bajaji wana wake zao..wote tunao home
Wadogo wa wife wasichana wamemaliza la saba mwaka jana, ninao home pia - mmoja anajifunza cherehani na mwingine anafanya kazi ya kibanda cha Tigo / Mpesa -
Nina wadogo zangu wawili wa mwisho, wote wanasoma VETA changombe - ufundi magari.
Watoto wengine bado wapo shule......kayumba sina uwezo wa kuwapeleka FM Academia.
Kila ikifika jioni tunakutana wote - tunafanya donee ili tuweze kuwa ha hela ya kuhemea siku inayofuata, kulipa umeme na maji.

Cha moto nakipata !!! na Corona hii kukaa home kichwa kinaumaa!!
Mkuu ni ya kweli haya?
 
22 years old namiliki hp laptop pressario CQ56,kitanda na godoro 5*6 jiko la gesi mtungi wa kg 29.5 taifa gesi, simu smart 4g, sabufa kubwa sea peano,kabati la nguo, music,movies libraly and stationaries, samsung full hd flatscreen with 32 inches, big and muscular body special for cute girls

Daah
 
Miaka 58
Mke mmoja watoto wa ndoa 6
Watoto wa pembeni 5 niliwachukuaga ninao home - jumla ya watoto 11
Nina kiwanja...tofali zipo site mwaka wa pili sasa ila kupandisha mambo yamegoma
Nimepanga nyumba nzima...Tandare kwa Mtogole
Sijawahi kumiliki gari...ila nina pikipiki wa ajili ya safari zangu na familia
Nina kibarua Tshs 540,000 kwa mwezi
Watoto 3 wasichana wamezalia home....wapo
Watoto wengine 3 wa kiume, mmoja Dj kwenye bar, Mwingine bodaboda na mwingine yupo home tu hata sijui shughuli zake
Shemeji zangu wawili kaka za wife nipo nao, mmoja dereva wa daladala, mwingine bajaji wana wake zao..wote tunao home
Wadogo wa wife wasichana wamemaliza la saba mwaka jana, ninao home pia - mmoja anajifunza cherehani na mwingine anafanya kazi ya kibanda cha Tigo / Mpesa -
Nina wadogo zangu wawili wa mwisho, wote wanasoma VETA changombe - ufundi magari.
Watoto wengine bado wapo shule......kayumba sina uwezo wa kuwapeleka FM Academia.
Kila ikifika jioni tunakutana wote - tunafanya donee ili tuweze kuwa ha hela ya kuhemea siku inayofuata, kulipa umeme na maji.

Cha moto nakipata !!! na Corona hii kukaa home kichwa kinaumaa!!
i hope happa umeandka utani maana ukipiga hesabu hao wanao jumlisha na ndugu jumla nyumba iko na watu 20+.
 
Vijana by the age of 30, kuchuma mali nyingi inawezekana na kihalali kabisa, kuna makala namalizia kuandika najua itawaunua wengi muno, humu jf approximately 6 to 7 people watafanikiwa sana, nitatoa vionjo vya siri ya kupata pesa hata haitaji formula nyingi na ngumu ni akili ndogo sana... ingawa nitaileta kwa ID nyingine kabisa
vp ushaileta? kama ndio,uliweka ktk jukwaa lipi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom