Unamiliki nini katika Umri huu?

Unamiliki nini katika Umri huu?

Uza hivyo vifaa vyako mf. Labtop, ipad, simu, ving'amuzi vya dstv 3, jiko la umeme na hiyo pikpiki ya kijapan ili uweze kununua gari ya ndoto zako ukiongeza na vihela vingine.
 
Waungwana wa humu, hapa nina wazo la kijinga tu hapa. Lakini ndo JF ilivyo hata ukiwa na pumba watu wataisoma tu. Mfano mimi nimewaza niandike kila atakaye pitia uzi huu utaje kwanza Umri wako na mali ulizonazo hadi kufikia umri wako. Au kama ulishazipoteza kwa ujinga wako au bahati mbaya.
Kwangu mimi naanza hivi japo sijafanikiwa sana katika maisha kwa jinsi nilivyojipangia kuwa.

Nina umri wa miaka 42.
Nina mke na watoto watatu, japo nishakuwaga na michepuko, ila nshaipiga chini.
Nina kaduka ka mtaani kadogo japo kananiingizia kakipato kwa kula mboga na ugali.
Nina kagari kadogo ka kirikuu nilikaagizaga japan.
Nina pikipiki ya kijapan used inanisadia visafari vyangu vya hapa na pale.
Nishawahi kununua pikipiki pia za kichina kama Fekon na Sanlg.

Nimefanikiwa kujenga nyumba ambayo thamani yake imefika 32Mln.
Nina vitu vya nyumani vingi tu kama Set ya kochi za mbao za kizamani za mninga, vitanda kama vinne vya mbao, tv Samsung 32"flat panel HD, Sony 5.1channel hone theatre,Jiko la umeme na gas, fridge Juba la kikorea, ving'amuzi vya dstv vitatu, Azam kimoja na madish yake, nina dish kubwa la nchi 6, vifaa vya kazi kama grinder, drill sander, nina simu ya sumsung, ipad ya apple, laptop toshiba, printer ya samsung laserjet, na vungine vingi vidogo dogo kama blender, juice dispencer nk.
Huu ni ujinga wangu naojisikia kuandika kwa leo. Hebu tuletee na wakwako pia ili tujilinganishe mafanikio yako hadi katika umri ulio nao.

Maana wengine umri mdogo wana mali za mamilioni wengine umri mkubwa wana mali za maelfu na wengine hawana kabisa hela zinaishia kula.
Kwa kifupi mafanikio yangu yametokana na ubahili wangu, sinywi pombe wala kula bata. Hata pamba za bei mbaya za dukani sivai kwa sababu sina pesa za kufanya hayo, la sivyo nitachekwa. Nakomaa sana kwenye kazi lakini napata vihela vidogo sana
Natamani niweze kujenga ghorofa lenye swimming pool na kuendesha magari kama rangerover, au wagon yoyote kali. Natamani nipate mchongo utakaonipa pesa nika enjoy utalii sehemu mbali mbali ninazotaka duniani. Maana maisha ni mafupi afu duniani kuna raha sana.
''napata vihela vidogo sana'' ''na vungine vingi vidogo vidogo'' WEWE NI MHAYA,TENA INAWEZEKANA HUNA HATA KIMOJA ULIVYOTAJA.misifa at work.
wagiramayooo,wasibhayota,walalamo!!!!!!! bhojooooooooo,yani kwakweliiiiiiii! inyaaaaa
 
Nina 30, namiliki nyumba mbili moja ipo kibaha kwa mathias, nyingne ipo morogoro nane nane, nina gari nne (ranger nyeusi, harrier, noah , na spacio), sina mke, sina mtoto, sasa hvi najenga ghorofa moja kimara, nina mashamba ekari 22, nina biashara yangu kubwa tu ambayo inasogeza siku, ni machine za kusaga za kukoboa, nina viwanja viwili. Katika elimu nina degree moja, na sasa hv ninatarajia kusoma masters kwaajili ya sifa tu, si unajua sisi wahaya. Ni hayo tu.
Nimechekaaa mnoeti si unajua wahaya sie kwa sifa
 
Nina 30, namiliki nyumba mbili moja ipo kibaha kwa mathias, nyingne ipo morogoro nane nane, nina gari nne (ranger nyeusi, harrier, noah , na spacio), sina mke, sina mtoto, sasa hvi najenga ghorofa moja kimara, nina mashamba ekari 22, nina biashara yangu kubwa tu ambayo inasogeza siku, ni machine za kusaga za kukoboa, nina viwanja viwili. Katika elimu nina degree moja, na sasa hv ninatarajia kusoma masters kwaajili ya sifa tu, si unajua sisi wahaya. Ni hayo tu.
Hongeraa aisee
 
Binafsi umri miaka 29 sina nyumba yakwangu ila nimemjengea mama kijijini nyumba ya milion25 nina wadogo zangu wawili mmoja miaka 23 nimemnunulia machine tatu za kuchomelea machine ya kupulizia rangi na vifaa vyote vinavyoitajika kwenye kazi yake,mdogo wangu wa pili ana miaka 26 Yeye janja njanja nyingi nimemnunulia kamchomoko kamoja anapiga shantingi mjini mama nimemfungulia kiduka ja rejareja kijijini cha milioni nne nimefanya hvyo ili nikianza familia yangu dipendants wangu wawe wachache sasa hv najenga nyumba mjini na mwakani mungu akipenda nafungua kiduka changu cha kunisaidia, sijaajiliwa napiga mishe town japo nina kashaada kangu kafedha mipango na uwekezaji.
Una akili sana ,maana ukiwatelekeza hao wote watakutazama
 
Nina 30, namiliki nyumba mbili moja ipo kibaha kwa mathias, nyingne ipo morogoro nane nane, nina gari nne (ranger nyeusi, harrier, noah , na spacio), sina mke, sina mtoto, sasa hvi najenga ghorofa moja kimara, nina mashamba ekari 22, nina biashara yangu kubwa tu ambayo inasogeza siku, ni machine za kusaga za kukoboa, nina viwanja viwili. Katika elimu nina degree moja, na sasa hv ninatarajia kusoma masters kwaajili ya sifa tu, si unajua sisi wahaya. Ni hayo tu.
Aisee una bahati sana miaka 30 wewe millionia duh.....ebu tuone uligraduate ukiwa na miaka 24 kwahiyo hivyo vitu vyote kama sio vya kurithi ulivitafuta dani ya miaka sita, tu tena kumbuka kuna hi mitatu ya magufuri ambayo biashara iko low sana
Nyumba 2
Gari 4
Ghorofa kimara 1.
Ekari za aridhi 22
Mashine y
Za kusaga 2
Viwanja vingine viwili
Duh wewe utakuja umpite hata Mo ukiwa 42.....duh hongera sana
 
Binafsi umri miaka 29 sina nyumba yakwangu ila nimemjengea mama kijijini nyumba ya milion25 nina wadogo zangu wawili mmoja miaka 23 nimemnunulia machine tatu za kuchomelea machine ya kupulizia rangi na vifaa vyote vinavyoitajika kwenye kazi yake,mdogo wangu wa pili ana miaka 26 Yeye janja njanja nyingi nimemnunulia kamchomoko kamoja anapiga shantingi mjini mama nimemfungulia kiduka ja rejareja kijijini cha milioni nne nimefanya hvyo ili nikianza familia yangu dipendants wangu wawe wachache sasa hv najenga nyumba mjini na mwakani mungu akipenda nafungua kiduka changu cha kunisaidia, sijaajiliwa napiga mishe town japo nina kashaada kangu kafedha mipango na uwekezaji.
Wow,uko vizuri mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom