Unamiliki nini katika Umri huu?

Unamiliki nini katika Umri huu?

Mimi mwamume umri 35,Namiliki wake wawili watoto wanne,vitanda 5 na godoro zake Sina nyumba sina gari sina kiwanja,sina kazi,sina pesa Natunzwa tu na wake zangu.Kwa sasa hivi natafuta mke wa tatu awe na miaka 30 anayejiweza.
Hahahahah.....

Mbavu sina
 
Nina Miaka 45.
Nina mke mmoja na watoto watatu. Nina kighorofa floo mbili hapa hapa Mapinga.
Nina Biashara zifuatazo
1. Nina duka la vipodozi hili analiendesha mke wang
2. Nina saloon ya kiume hii ni kwa matumiz madogo ya home
3. Nina kigari kidogo cha kuzugia Passo
4. Nina mashamba 50hekari
5. Mwakani naongeza mke wa pili
 
Nina miaka 23.

Namiliki grupu la whatsapp la PachuPachu, Msingi Kiuno, na ZaUchiZoteHapa.

Nina sabwufa limeharibika sehemu ya flash na pini ya waya imekatikia kwenye tundu.

Nasikia nilikabidhiwa viwanja kijijini kwetu ila sijawahi hata kuviona na kwenda kijijini sitaki.

Nina wanawake wanne wa kudumu na watatu ni occasional.

Sina chumba wala nyumba nalala kwa rafiki yangu Dilongele.

Nina elimu kidogo ya form six.

Pia nina nyege.

Wee jamaa sijui ulkua unafikiria nn kuandika hv
 
Mimi nina miaka 48 similiki chochote hata hii simu ninayotumia hapa nimeazima kwa mtu.
Wewe je, wamiliki nini?
Are you serious 48 ? So mimi na dogo janja kumbe hamna tofauti
Wote twalelewa
 
Mkuu nimeona hapo moja ya vitu ulivyonavyo ni "sander"
Vipi ushanunua na jeneza?
Kama bado njoo fasta pm tufanye biashara ntakupunguzia bei hasa kama ukilipia majeneza mawili nakupa offer ya jeneza moja la mtoto.
Nunua mzigo mkuu hii ni akiba maana hujui kesho yako.
Waungwana wa humu, hapa nina wazo la kijinga tu hapa. Lakini ndo JF ilivyo hata ukiwa na pumba watu wataisoma tu. Mfano mimi nimewaza niandike kila atakaye pitia uzi huu utaje kwanza Umri wako na mali ulizonazo hadi kufikia umri wako. Au kama ulishazipoteza kwa ujinga wako au bahati mbaya.
Kwangu mimi naanza hivi japo sijafanikiwa sana katika maisha kwa jinsi nilivyojipangia kuwa.

Nina umri wa miaka 42.
Nina mke na watoto watatu, japo nishakuwaga na michepuko, ila nshaipiga chini.
Nina kaduka ka mtaani kadogo japo kananiingizia kakipato kwa kula mboga na ugali.
Nina kagari kadogo ka kirikuu nilikaagizaga japan.
Nina pikipiki ya kijapan used inanisadia visafari vyangu vya hapa na pale.
Nishawahi kununua pikipiki pia za kichina kama Fekon na Sanlg.

Nimefanikiwa kujenga nyumba ambayo thamani yake imefika 32Mln.
Nina vitu vya nyumani vingi tu kama Set ya kochi za mbao za kizamani za mninga, vitanda kama vinne vya mbao, tv Samsung 32"flat panel HD, Sony 5.1channel hone theatre,Jiko la umeme na gas, fridge Juba la kikorea, ving'amuzi vya dstv vitatu, Azam kimoja na madish yake, nina dish kubwa la nchi 6, vifaa vya kazi kama grinder, drill sander, nina simu ya sumsung, ipad ya apple, laptop toshiba, printer ya samsung laserjet, na vungine vingi vidogo dogo kama blender, juice dispencer nk.
Huu ni ujinga wangu naojisikia kuandika kwa leo. Hebu tuletee na wakwako pia ili tujilinganishe mafanikio yako hadi katika umri ulio nao.

Maana wengine umri mdogo wana mali za mamilioni wengine umri mkubwa wana mali za maelfu na wengine hawana kabisa hela zinaishia kula.
Kwa kifupi mafanikio yangu yametokana na ubahili wangu, sinywi pombe wala kula bata. Hata pamba za bei mbaya za dukani sivai kwa sababu sina pesa za kufanya hayo, la sivyo nitachekwa. Nakomaa sana kwenye kazi lakini napata vihela vidogo sana
Natamani niweze kujenga ghorofa lenye swimming pool na kuendesha magari kama rangerover, au wagon yoyote kali. Natamani nipate mchongo utakaonipa pesa nika enjoy utalii sehemu mbali mbali ninazotaka duniani. Maana maisha ni mafupi afu duniani kuna raha sana.
 
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji115.png
emoji115.png

Wee jamaa sijui ulkua unafikiria nn kuandika hv
Binafsi umri miaka 29 sina nyumba yakwangu ila nimemjengea mama kijijini nyumba ya milion25 nina wadogo zangu wawili mmoja miaka 23 nimemnunulia machine tatu za kuchomelea machine ya kupulizia rangi na vifaa vyote vinavyoitajika kwenye kazi yake,mdogo wangu wa pili ana miaka 26 Yeye janja njanja nyingi nimemnunulia kamchomoko kamoja anapiga shantingi mjini mama nimemfungulia kiduka ja rejareja kijijini cha milioni nne nimefanya hvyo ili nikianza familia yangu dipendants wangu wawe wachache sasa hv najenga nyumba mjini na mwakani mungu akipenda nafungua kiduka changu cha kunisaidia, sijaajiliwa napiga mishe town japo nina kashaada kangu kafedha mipango na uwekezaji.
 
Mimi Nina umri Wa miaka 40.... Nina chumba kimoja cha kwngu mwenyewe,,RADIO YA PHILLIPS... na Maua ya plastics,,NGOMA NA STULI ZAKE,,pamoja na kabati LA mbao ,,,na NDOO ZA PLASTICS kwa ajili ya kuwekea maji
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom