Unamiliki nini katika Umri huu?

Unamiliki nini katika Umri huu?

JF huwa patamu sana,kila mtu huwa ana pesa,viwanja, nyumba ,mke mzuri na elimu yake nzuri tu na kajiajiri ....Anyways mimi namiliki simu Tecno tu
Kila mtu kivipi mkuu mbona wapo wengi wapo broke na wamefunguka
 
Nina 30, namiliki nyumba mbili moja ipo kibaha kwa mathias, nyingne ipo morogoro nane nane, nina gari nne (ranger nyeusi, harrier, noah , na spacio), sina mke, sina mtoto, sasa hvi najenga ghorofa moja kimara, nina mashamba ekari 22, nina biashara yangu kubwa tu ambayo inasogeza siku, ni machine za kusaga za kukoboa, nina viwanja viwili. Katika elimu nina degree moja, na sasa hv ninatarajia kusoma masters kwaajili ya sifa tu, si unajua sisi wahaya. Ni hayo tu.
Duh kweli kaka we muhaya upo vzr
 
Mimi namiliki majumba kama yote huko cheka u'ngatwe pia namiliki shamba la veve eka moja
 
Nijibu kwanza, unamiliki nini?
Mimi nina miaka yangu 45
Nina mke na watoto wanne (Binti wawili na waume wawili)
Nina kigari kimoja cha kutembelea (Mark ll)
Nina kimini bus (Coaster Delux Box)
Nina kijumba hakijakamilika ujenzi wake, (on final touch stage)
Nina vyumba viwili vya biashara ya Nguo special za wanawake na watoto (anasimamia wife)
Nina, (hivi vingine nashindwa kuvitaja kwasababu ni vile minor things), kama 32" Sumsung Flat screen HD, 24" LG Flat screen HD
HP Laptop, HP Printer, Sony Radio, Sony Digital Camera 3, Sony MP3 Sub woofer, Kuku wa kienyeji na Bata (kwa ajili ya kitoweo)
 
Waungwana wa humu, hapa nina wazo la kijinga tu hapa. Lakini ndo JF ilivyo hata ukiwa na pumba watu wataisoma tu. Mfano mimi nimewaza niandike kila atakaye pitia uzi huu utaje kwanza Umri wako na mali ulizonazo hadi kufikia umri wako. Au kama ulishazipoteza kwa ujinga wako au bahati mbaya.
Kwangu mimi naanza hivi japo sijafanikiwa sana katika maisha kwa jinsi nilivyojipangia kuwa.

Nina umri wa miaka 42.
Nina mke na watoto watatu, japo nishakuwaga na michepuko, ila nshaipiga chini.
Nina kaduka ka mtaani kadogo japo kananiingizia kakipato kwa kula mboga na ugali.
Nina kagari kadogo ka kirikuu nilikaagizaga japan.
Nina pikipiki ya kijapan used inanisadia visafari vyangu vya hapa na pale.
Nishawahi kununua pikipiki pia za kichina kama Fekon na Sanlg.

Nimefanikiwa kujenga nyumba ambayo thamani yake imefika 32Mln.
Nina vitu vya nyumani vingi tu kama Set ya kochi za mbao za kizamani za mninga, vitanda kama vinne vya mbao, tv Samsung 32"flat panel HD, Sony 5.1channel hone theatre,Jiko la umeme na gas, fridge Juba la kikorea, ving'amuzi vya dstv vitatu, Azam kimoja na madish yake, nina dish kubwa la nchi 6, vifaa vya kazi kama grinder, drill sander, nina simu ya sumsung, ipad ya apple, laptop toshiba, printer ya samsung laserjet, na vungine vingi vidogo dogo kama blender, juice dispencer nk.
Huu ni ujinga wangu naojisikia kuandika kwa leo. Hebu tuletee na wakwako pia ili tujilinganishe mafanikio yako hadi katika umri ulio nao.

Maana wengine umri mdogo wana mali za mamilioni wengine umri mkubwa wana mali za maelfu na wengine hawana kabisa hela zinaishia kula.
Kwa kifupi mafanikio yangu yametokana na ubahili wangu, sinywi pombe wala kula bata. Hata pamba za bei mbaya za dukani sivai kwa sababu sina pesa za kufanya hayo, la sivyo nitachekwa. Nakomaa sana kwenye kazi lakini napata vihela vidogo sana
Natamani niweze kujenga ghorofa lenye swimming pool na kuendesha magari kama rangerover, au wagon yoyote kali. Natamani nipate mchongo utakaonipa pesa nika enjoy utalii sehemu mbali mbali ninazotaka duniani. Maana maisha ni mafupi afu duniani kuna raha sana.
Mali pekee ulizo nazo ni hizi: kaduka ka mtaani kadogo; kagari kadogo ka kirikuu; na pikipiki ya kijapan used. Komaa navyo, ukiona kamoja kanachakaa, unanunua kengine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom