Unamhudumia wakati hujamuoa, Umerogwa??

Unamhudumia wakati hujamuoa, Umerogwa??

Ukiona mwanaume anatokwa povu kuhusu kuhonga tuna wasiwasi nae [emoji16][emoji16].

Kama mwanamke kanitongoza yeye hata sh simpi. Na imenitokea mara nyingi ila nikiona nakomaa dem mkali haeleweki mzee. Ndo hapo unatakiwa ujiongeze. Na(nakazia hili) ukikubaliwa fanya kweli ili usihangaike baadae kumpata. Ahangaike yeye, aone mautundu yako. Utakuwa huhongi tena maybe kidogo sana

[emoji2] [emoji2] [emoji2]

Ni kutokujiamini tuu kwa baadhi ya wanaume. Hivi unadhani kumpa hela ndio kuuteka moyo wa mwanamke?

Wanaume wa siku hizi hawajui elimu ya mahusiano. Mhudumie tuu mkeo full stop
 
Habarini za pasaka!!
Hakuna jambo baya Kama mwanaume kutokujitambua. Kuwa mwanaume ni heshima kubwa hakuna asiyejua. Si Wanyama si ndugu zetu wanawake hilo wanalijua.

Sasa wapo wanaume ambao sijui mafunzo hawakupata au vipi. Na hii ni sababu ya malezi na makuzi.

Mwanaume halisi hapaswi kuhonga mwanamke yoyote ambaye hajamuoa. Ipo Tabia kwa baadhi ya wanaume nadhani wasiojiamini ambao kutoa pesa kwao kwa wanawake ni jambo rahisi Sana. Kwa taarifa tuu ni kwamba unadhalilisha hulka ya kiume. Sio jukumu lako kumtunza mwanamke asiye mke wako.

Na ni dhambi kubwa kumhudumia mwanamke ambaye hujamuoa. Kiimani huitwa kutapanya mali kwa uasherati. Kiuchumi huo ni ubadhirifu. Kitababia huko ni kutokujiamini na ulofa. Jukumu la kumtunza mwanamke kabla ya ndoa ni la wazazi wake au yeye mwenyewe. Hiyo ndio tabia ya kihere here mwishoe unapiga mayoe ukija kuachwa.

Hivi wazazi wako wamekusomesha hadi umefika chuo na kupata kazi. Badala ya kulipa fadhila kwa Mama na Baba wewe unajitia penda penda. Hiyo ni dalili ya kulogwa. Kama ni nguo si umnunulie mama yako na Baba yako. Hivi mama yako kipindi akivaa magunia ili usome ulidhani hakutaka kujiremba. Mnunulie Mama yako mafuta na vipodozi apendeze uone Kama hutabarikiwa.

Wewe kazi kutapanya Mali Kwa mademu kama chizi. Kiukweli wanaume wenzangu wenye tabia hii huwaga mnatuangusha. Hata wanawake wanawadharau kwakweli. Binti unampa hela siku akienda kwenu kumcheki mama yako kajichokea. Kama unatabia hii wewe ni chizi na umelogwa.

Usimuhudumie mwanamke Kama hujamuoa. Kama unataka kumhudumia Kama mkeo si umuweke ndani. Unajifanya unajua kuhudumia. Wakati ukioa kuhudumia huko kwakushinda. Huu ni unafiki ambayo si tabia ya kiume.

Mwanamke akitaka pesa mwambie sina. Kama hakuelewi mwambie kila la kheri.
Sio lazima ung'ang'anie Kama hakuna wanawake wengi. Lipa kwanza fadhila kwa waliokufikisha hapo na sio kutapanya Mali mwishoe unajifia na maradhi Kama sio umasikini.

Wapo wale wajirembao Kama mademu.
Hivi mwanaume mzima unaanzaje kujiremba kwanza hata kufikiria unaanzaje.
Yaani mwanaume mzima nywele unatia dawa, make up Kama unaenda harusini.
Kuonyesha matako hadharani Kama unataka kuliwa tigo. Hivi unataka kushindana na wanawake utaweza.

Kwa taarifa yako wanawake hutawaweza wao hicho ndicho kilichowaleta duniani.
Na hata hao wanawake hivi ulidhani wanataka kuwa wanawake?
Embu wenye tabia hizi muache Mara moja. Mnatuangusha wanaume.

Kwa leo niseme basi. Nimeona tukumbushane wanaume wenzangu
100% kwa 100% mkuu
 
Kabisaa, wanakuwa kama kupe vile halfu mbaya zaidi hata ukisema huna hakuelewi!!
Pia tujue kuwa mwanamke hata ukimhudumia vzr leo akiwa na shida nyingine kesho usipo mhudumia atakulaum as if hujawahi mfanyia cha maana ktk maisha yake!!
Lkn wapo wanajitambua wachache sana
Ndio akili iingie kichani sasa.

Ushaambiwa wanawake hawaridhiki hasa wapenda pesa alafu mtu unajifanya kumpatie hela si kulogwa huku jaman
 
wa hivyo umuumbe mwenyewe
Wapo wengi Sana mkuu.
Sio wanawake wote wana umasikini wa mawazo.

Anayehudumiwa ni mke tuu au mwanamke uliyezaa naye basi. Zaidi ya hapo ni akili ya mwanaume imeingiza ushetani
 
Mleta thread ana mawazo ya watumia 'kiroba original',,,,,hivi kweli ushindwe kumpa mwanamke wako hata hela ya ped au panadol????!!!!!. Basi wewe ndo awe anakuhudumia tu.

Sent from my HUAWEI Y520-U22 using JamiiForums mobile app
Hunielewi mkuu.
Wewe hujiulizi yeye anashindwaje kujihudumia mwenyewe hata hivyo vidogo? Tena hawa ndio huwaga wananikomaga
 
Mbona nyie mnaomba game kwao???tena kwenye vifua vya wadada mpaka mnasimamia kucha kabisa,msigharamie na ndio maana hampati papuchi. Nashukuru wadada wenzangu nayo wameerimika now days,no money no honey..tusileteane ujambazi [emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]na Kama ushaielewa habari yake huwezi katu kumuacha kisa kakuomba ela. Na tutawaomba mpaka mbakiwe na sh. 50 mfukoni.
Wewe ndio wanakuona boya eti no money no game.
Wenzako tunacheza game na pesa hapati. Kama hataki kila mtu anameza njia yake.

Wanawake wanahitaji mwanaume mwenye akili za kuwashinda na si pesa.
Kaa chini utafakari
 
Sawa upo sahh, ila ilo linafanyika kwasababu ya ubinaadam tu... Bnafs naona c mpk awepo kwny ndoa ndo umsaidie, kwangu io ngum kdg... Pale akiwa n uhitaj ambao utakidh uwezo wangu, n kwakua ni bnaadam mwenzangu, bs ntamsaidia tu mkuu.. Au co?
Ukiona umefikia uwezo wa kumhudumia si umuoe?
Ninyi ndio mnawadanganya na kuwapotezea muda watoto wa watu
 
Tatizo moja ule uongo wa kumfuata na kumwambia nitakuoa ikiwa mwenzio anataka kuolewa kumbe ww ni papuchi tu bora kumuweka wazi kabisa kwa Dada kwako nataka mapenzi tu na kuumpa mwanamke pesa sio umehonga tunasaidiana tu hata ww atakusaidia siku umekwama
Kwa nini usimuoe Kama mnataka kusaidiana.
Kuhonga pia ni kusaidia mkuu au hujui?
Mke wako ndiye mnayesaidiana na ndio maana ya msaidizi huyo mwingine ni kumhonga kozi hakuna kanuni inayosema hivyo.

Hata akienda mahakamani watamshangaa.
 
Yn hao wachangiaji wa mwanzo lugha zao tu unajua hawa ni wanachuo..au la ni sekondari...mtu anatumia X badala ya S..halafu mwanaume aliyekomaa hawezi ongelea issue za hela ki namna hii
From wt i know matured man anajisikia tu raha yani kumuhudumia baby bila ht kuombwa .
Sasa hizi hela za boom mtu anazipigia mahesabu..kipapa atumie ht hela ya perfume usimpe eboo
Mwanaume aliyekomaa hawezi kumhudumia mwanamke asiyemke wake hata siku moja. Bali mke wake.

Sasa wewe unahudumiwa na kichwa maji unamuona amekomaa. Kama kakomaa mwambie akuweke ndani aone joto lake.

Wanaume wahongaji ndio hao hao siku akija kukuoa baada ya miaka mitano unashangaa Matumizi ya nyumbani yanapungua, kisa kapate kitoto cha nje. Mwanaume asiyemuhudumia mwanamke aliyemuoa na kumuhudumia asiyemuoa huyo akili hana yaano kalogwa.

Kama unaakili nzuri umenielewa lakini Kama unawaza Kama mwanamke mpumbavu huwezi nielewa.

Kwa ujumla sijakurupuka kupost mada hii.

Fikiria kwa mapana yake. Na usidhani nimekuja kumtukana Mtu au kutetea upande
 
aliyetoa maada hii atakuwa mwanafunzi, sisi kina liumba tunaonga mpaka magari, sembuze viguo vya 25000, ukikua utajua maana ya kuhonga
Ndio maana wazungu waliita waafrika manyani kwa akili hizi.

Yaani mtu mzima unajisifia kuhonga wakati unapaswa kusikia aibu.

Ndio ninyi mkipata vigari viwili mnajiona mnahela.
Una honga kwa hela gani ulizokuwa nazo. Nchi ni masikini unapaswa uwekeze zaidi na zaidi wewe unaishia kuhonga. Akili ndogo bhana utazijua
 
Raha ya mwanaume ni kuhonga, bila kuhonga unakuwa bado ujafikia kwy uanaume unakuwa mvulana.
Mwanaume ni yule aliyeoa mkuu. Sio wewe unayehonga kwa msimu ujiite mwanaume.

Kama unajua kuhonga si uoe.
 
Mimi hua na tabia ya kumsifia mpenzi wangu sasa Nina mda tunawasiliana tu sitoi hela zaidi ya vocha juzi nikasema ngoja nikamtembelee nikamkuta amependeza kuanzia nywele mpaka miguuni na hana kazi yeyote yaani sikumsifia hiyo siku nikajua hapa kuna mjanja ananisaidia nilicho kifanya ni kujifanya nina haraka ya kuondoka maana niliona aibu na nahisi hata yey alipendeza kwa makusudi kuonesha wapo wanao jali sasa kutunza chombo chako ni lazima
Mkuu Kama unataka kumtunza si umuoe tuu.
 
Naona kijana umeamua kutugusa sisi wanajeshi....[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

mm juz nimetoka muonga mtu toyota crown......

jas kidding.[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]...
 
Vijana mna mambo ya ajabu sana kwenye huu utawala wa baba Jesca...yan umekaa ukawaza sana na kuona ni dhambi kumuhumia mwanamke asiye mke wako.
Mi nilijua unazungumzia uzinifu kushiriki tendo la ndoa kabla ya kuwa mkeo....!! Kama hutaki kumuhudumia hakikisha hufanyi nae mapenzi mpka umuoe. Kama na wewe utaweza...! Sio mnaleta uzi kwa sababu umeamka asubuh umechelewa vitumbua vya foleni kwa shemeji yako hapo unaawaza hela uliyompa Mwajuma Jana. Ni haki yake c ulimchafua bwana.
Anzisha Uzi wako mkuu.
 
Back
Top Bottom