Unafiki huu wa wanaharakati (CHADEMA), kiboko

Unafiki huu wa wanaharakati (CHADEMA), kiboko

Chadema haijaletwa na mungu.hivyo inaweza pia kusambaratika.tafsiri nzuri kwa kauli ya nape ni kwamba chadema inapoteza imani miongoni mwa wananchi,wanachama na wasiowanachama.nadhani mtakumbuka kuna wapiga kura wengi sana wasio na vyama.baadhi kwa wameamua kutokua na vyama na wengine ni mashariti ya nafasi walizonazo.kwa hiyo wapiga kura wakijiuliza ni kina nani wapewe dola,hakika mgogoro huu unazoathari kubwa sana kwenye jibu la swali hilo.tazama mgogoro huu umedumu laivu kwa mda gani.nadhani ni miezi takribani miwili au mitatu.na bado pengine utaendelea kwa mda mrefu zaidi.agenda nyingi za kukijenga chama zimelala na hasa ile ya katiba mpya. Kwa hiyo tukitafsiri kwa faida yetu kauli ya nape ni kwamba chadema iwapo haitamaliza mgogoro huu mapema athari zipo tu, kwa chama na kwa maendeleo ya demokrasia hapa nchini.
 
Nyie wachukueni hao wanaofukuzwa huko CDM muwavumilie, ni kweli mna uwezo wa kuvumilia vijana na si wazee tumeona mliyemvua uanachama kule znz.

Mchukueni na huyo zitto, samson mwigamba na kitily wakashindane na mwigulu. Na vilevile ya ng'oswe mwachie ng'oswe we fanya yako yanayokuhusu.
 
Huwezi kumfukuza ZITTO bado kajifariji kuwa chama kiko imara

Kwani Zitto ni nani wa nchi hii?
Wamepita wanasiasa wengi sana maarufu na mahiri kuliko huyo. What is so special with him? Mambo ya Chadema tuwaachie Chadema. Kama Zitto ni wa muhimu sana basi CCM wamchukue na kumpa uanachama. NUKTA.
 
Tulipo jikwaa ni ZZk,na tunaanza kumtimua yeye ili tujenge safu imara... Tunajua Mnaumia kwa kumtimua Kibaraka wenu ambaye mlimuandaa avujishe Siri na Mikakati ya jinsi gani Tunajipanga kwa Uchaguzi.. sasa imekula kwenu!

Kutimuliwa huyu bwana nashangaa kumewakera sana CCM kuliko waathirika wa uhuni wake. Mambo ya Chadema kwa nini yawakere CCM? Ya Ngoswe wamuachie Ngoswe. Mbona wao walimpokonya uanachama ndugu Himid na upinzani hawakuingilia maamuzi yao?
 
Wewe kiboko yako ni Lowasa tu, na akiupata urahisi tafuta pa kukimbilia.
 
Haya ni mapito kwa chadema, kweli nyani haoni kundule, mbona nyie viongozi wenu wakienda kucheki afya wanakuja wakiwa maiti?
 
Nafikiri we we ndio mnafiki mkubwa maana kwa umri huo huijui familia yako zaidi ya kung'ang'ania familia za wenzako.
 
Nape, umefika wapi na kampeni yako ya kujivua gamba? tuambie mafanikio yako katika kampeni hiyo. Mangapi mmeyavua? huo nao ni unafiki
 
Subiri Lowassa achukue nchi kama utabaki sisiem (chama cha majangili) achilia mbali kubaki nchini.
 
Nape wasaidieni wakulima na wafugaji wanauwana kila siku ...
 
Naandika hili kwa masikitiko makubwa maana watani zangu CHADEMA siku zao zinahesabika kwa kasi inayonitisha sana. Mimi ni muumini wa uimara wa CCM kutegemea sana uimara na umakini wa upinzani nchini! Kwahiyo anguko la upinzani nchini si jambo zuri kwa CCM, nchi na demokrasia yetu, CHADEMA kikiwa moja ya taasisi muhimu kwenye ukiaji wa demokrasia hiyo!

Kilichonistua ni degree ya unafiki inayojidhihirisha kila kukicha ya viongozi wengi wa CHADEMA. Kupinga ufisadi kwa mdomo mpana halafu unaendesha Chama kwa pesa hizohizo huu ni unafiki wa ajabu! Tunajifunza nini kwa kiongozi wa Chama anayesema pesa ni pesa tu inategemea unaitumiaje!!? Ha! Kwahiyo unaweza kuuza nchi ilimradi unapewa pesa!!?

Niliwahi kutoa mfano mkubwa wa unafiki wa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Slaa (sikuhizi nasikia vijana wanamwita Mzee wa Gongo) akihubiri watu waichukie CCM.

Na wakati mwingine alihamasisha wachane na hata kuchoma kadi za CCM wakati yeye kabanisha yake tena kwa matunzo makubwa! Huu ni unafiki mkubwa! Vijana tunajifunza nini kwa unafiki huu!???!

Lakini niliwahi kusema Chadema kinaendeshwa kwa pesa kutoka nje, wakabwata wakinipa siku saba kukanusha, kabla mate hayajakauka, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Ndg. Zitto anakiri hadharani kuwa gazeti leo, ambacho ni chombo kikuu cha propaganda limeanzishwa kwa pesa kutoka nje!! Huwezi kujenga Chama kwa msingi wa uongo kuliko wa shetani halafu ukadhani chama kitadumu!!!

Utaratibu wa vyama kufukuza wanasiasa vijana kwenye vyama hivyo ni wa hovyo na unapaswa kukemewa! Vijana wasipokosea mnataka wakafanyie wapi makosa?? Vyama lazima vitumike kulea na kuwafumdisha vijana badala ya kuwafukuza. Toka watani zangu waanze kufukuza wamekuwa wakifukuza vijana tu hasa wanaohoji. Kuhoji ndani ya CHADEMA ni mwiko! Mtakumbuka ya Kafulila na vijana wengine wengi tu. Mtauliza we Nape!! Ndio mimi chama changu kilinisikiliza na ndio maana nipo sikufukuzwa! Ukomavu ni pamoja na kuwa tayari kusikiliza maoni tofauti na uliyonayo!!

Ushauri wa bure: Watani anzeni upya! Msione aibu fumua anza upya tutawasubiri mkomae msihofu kuachwa sana! Mmekutana na ajali ya kisiasa kutafuta mchawi sio dawa, tafuteni mmejikwaa wapi.

Isao lyiseka irhewa.
 
Baadhi ya washiriki wa mijadala hapa jamvini,ikiwemo ya kisiasa,wameendelea kudhihirisha ukosefu wa umakini usiokoma katika kujenga hoja kinzani.
Punde,hoja imetolewa na mwanachama wa chama "A" kwamba chama "B" kinapaswa kujitazama na kujitafakari upya ikiwa mwelekeo wa maamuzi yake unakisaidia kujiimarisha ama unachangia kukudhoofisha.
Wanachama wa chama "B" wanapaswa kujenga hoja kinzani dhidi ya hoja iliyotolewa na wala mantiki hairuhusu kujadili udhaifu,kama upo,wa mwanachama wa chama "A".
"Argue",alipata kuasa Nyerere,"dont shout".
Nakisi ya mantiki katika mijadala ni mwendelezo wa porojo mbazo si rahisi kuona faida zake katika katika mchakato wa kujenga utamaduni imara wa kidemokrasia.
 
Baada ya dhiki faraja; ipo siku kitaeleweka tu. Kimsingi napenda kuwajibishana bila kujali ni nani anawajibishwa. Utamaduni wa kutowajibishana umeua uzalendo wa nchi nyingi za kiafrika kwa kudhani kuwa kuna mtu/watu mhimu ambao bila wao nchi haiwezi kwenda! Tumekosea na tunavuna uharibifu wa uovu wa watu waovu kuachwa waendelee kufanya uovu ili kunusuru vyama au urafiki. Let Zitto fired halafu atadhihirisha umaarufu wake akianzisha chama kama Malema wa Afrika kusini
 
Sikumbuki rekodi ya CC kumvua mtu uanachama, japo mara kadhaa imewavua watu madaraka huku akiendele kuwa na uanachama, na baadhi baadaye walipewa nyadifa kwenye Chama na Serikali baada ya Kujirekebisha au adhabu zao kuisha,hata Slaa hakuwahi kufukuzwa CCM.....na hajawahi kurudisha Kadi ya CCM, kuhusu ahadi zipo zilizotekelezwa na zipo ambazo haziatekelezwa kutokana na muda mrefu wa miradi husika inaweza kuchukuwa miaka hata 20....mfano reli,meli nk......Pia sasa ni dhahiiri Chadema haiishi katika maneno yake........Dr.Slaa aliapa kutotumia shangingi akishinda uraisi kwa alisema shangingi moja ni sawa na zahanati nne...........angalia Mbowe,Slaa nk magari wanaoyatumia, pia waliahidi kutochukuwa posho angalia nini kinachotokea viongoizi wa CDM wananyukana juu ya posho huku 99.9% wakifagilia posho kinyume na ilani..........so hapa suala ni maadili kuporomoka kwa wa TZ na sio vyama.

Kutokukumbuka kwako hakumaanishi hicho kitu hakipo! Na whether ni kamati kuu ya ccm au chombo kingine kinachofukuza wanachama, the fact is: Kuna wanachama wa ccm waliowahi kufukuzwa uanachama. Of course wapo waliojitoa wenyewe - kama mimi.

It is obvious hukusoma post yangu kikamilifu - au umeshindwa kuielewa kwa makusudi au kwa kushindwa kuielewa - otherwise ungejua maana ya mimi kusema ahadi za ccm zilizotolewa 2010 na ambazo zitachangia ccm kuondolewa madarakani na kisha kuwa kama KANU na UNIP. Nae alielewa am sure!
 
Naandika hili kwa masikitiko makubwa maana watani zangu CHADEMA siku zao zinahesabika kwa kasi inayonitisha sana. Mimi ni muumini wa uimara wa CCM kutegemea sana uimara na umakini wa upinzani nchini! Kwahiyo anguko la upinzani nchini si jambo zuri kwa CCM, nchi na demokrasia yetu, CHADEMA kikiwa moja ya taasisi muhimu kwenye ukiaji wa demokrasia hiyo!

Kilichonistua ni degree ya unafiki inayojidhihirisha kila kukicha ya viongozi wengi wa CHADEMA. Kupinga ufisadi kwa mdomo mpana halafu unaendesha Chama kwa pesa hizohizo huu ni unafiki wa ajabu! Tunajifunza nini kwa kiongozi wa Chama anayesema pesa ni pesa tu inategemea unaitumiaje!!? Ha! Kwahiyo unaweza kuuza nchi ilimradi unapewa pesa!!?

Niliwahi kutoa mfano mkubwa wa unafiki wa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Slaa (sikuhizi nasikia vijana wanamwita Mzee wa Gongo) akihubiri watu waichukie CCM.

Na wakati mwingine alihamasisha wachane na hata kuchoma kadi za CCM wakati yeye kabanisha yake tena kwa matunzo makubwa! Huu ni unafiki mkubwa! Vijana tunajifunza nini kwa unafiki huu!???!

Lakini niliwahi kusema Chadema kinaendeshwa kwa pesa kutoka nje, wakabwata wakinipa siku saba kukanusha, kabla mate hayajakauka, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Ndg. Zitto anakiri hadharani kuwa gazeti leo, ambacho ni chombo kikuu cha propaganda limeanzishwa kwa pesa kutoka nje!! Huwezi kujenga Chama kwa msingi wa uongo kuliko wa shetani halafu ukadhani chama kitadumu!!!

Utaratibu wa vyama kufukuza wanasiasa vijana kwenye vyama hivyo ni wa hovyo na unapaswa kukemewa! Vijana wasipokosea mnataka wakafanyie wapi makosa?? Vyama lazima vitumike kulea na kuwafumdisha vijana badala ya kuwafukuza. Toka watani zangu waanze kufukuza wamekuwa wakifukuza vijana tu hasa wanaohoji. Kuhoji ndani ya CHADEMA ni mwiko! Mtakumbuka ya Kafulila na vijana wengine wengi tu. Mtauliza we Nape!! Ndio mimi chama changu kilinisikiliza na ndio maana nipo sikufukuzwa! Ukomavu ni pamoja na kuwa tayari kusikiliza maoni tofauti na uliyonayo!!

Ushauri wa bure: Watani anzeni upya! Msione aibu fumua anza upya tutawasubiri mkomae msihofu kuachwa sana! Mmekutana na ajali ya kisiasa kutafuta mchawi sio dawa, tafuteni mmejikwaa wapi.

Acheni porojo....mbowe kutoa mchango kwa ajili ya kampeni za mgombea flani...iwe wa ccm o chadema ni vitu vya kawaida....hata ulaya wako ivyooo......so yeye kuchangiwa pia ni kawaida na si ufisadi....ila Zzk ni msaliti wa chama. Na kumwadhibu ni lazima.
 
muulize mzee wasira na wengine ambao walisema chadema itakufa, sasa wewe unasikitika nini? si ndio haina za siasa mnazozitaka kuangamiza upinzani? ila itafika mahali ukweli utajulikana tu.
 
Back
Top Bottom