Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,120
- 879
Mjadala unaoendelea kuhusu Godbless Lema kutuma salamu za pole kwa Rais Samia Suluhu Hassan, kufuatia msiba wa mumewe unaonyesha tofauti kubwa kati ya msimamo wa chama na misukumo ya baadhi ya wanaharakati. Lema amekumbana na matusi na lawama nzito kutoka kwa baadhi yao, wakiona kitendo hicho kama usaliti wa msimamo wao.
Lakini ni muhimu kutenganisha mambo mawili chama kina mfumo, viongozi na taratibu zake na wanaharakati wana misimamo, maslahi na namna yao ya kuendesha mambo. Chama hakiwezi kuongozwa kwa kila kelele inayotoka mitandaoni au kwa kila shinikizo kutoka kwa watu wanaojitambulisha kama wanaharakati.
Inapofikia hatua mtu anatukanwa kwa kutoa pole kwa aliyefiwa, tunapaswa kujiuliza kama hawa wanaharakati hakuna hata mmoja mwenye akili timamu kujua kwamba salamu zilianza kutolewa na Tundu Lissu na akataka salamu zifikishwe, sasa kosa la Lema lipo wapi?
CHADEMA wanatakiwa wajue wana katiba, viongozi na utaratibu wao, wanaharakati hawapaswi kuteka nafasi ya taasisi, viongozi au taratibu za chama. Kiongozi anayesimamia taasisi lazima aangalie picha pana zaidi kuliko presha ya mitandao na makundi yenye maslahi yao binafsi.
Kwa hiyo, ujumbe ni mmoja, CHADEMA ikiendelea kutaka kuwakumbatia hawa wanaojiita wanaharakati itakula kwao vibaya sana, kwani hao waaojiita wanaharakati wana maslahi yao binafsi na hawapo kwa ajili ya CHADEMA.