JF Toons

Digital Art by JF
Feb 19, 2024
32
66
Habari,

Dk.PNG

Afya ni miongoni mwa huduma muhimu na msingi katika katika Jamii yoyote. Katika kupata Huduma za Afya kuna michakato na mambo mengi katikati yake.

Je, umeshawahi kukutana na kero gani katika kupata Huduma za Afya Kishingo akusaidie kuisemea?
 
Folen kubwa,

Milango ya Daktari mitano ila milango miwili ndiyo ina madaktari.

Ukiwaambia unahisi kuumwa wanachojua wao
Ni kukupima MARALIA, UTI, TYPHOID basi.

Ndiyo maana watu wengi sana Tanzania kansa wanakutwa nayo stage ya mwisho maana ukienda hospital ni kupimwa maralia na UTI.
 
Yaani unakuta mhudumu anamchoma mtu sindano bila kuvaa glovu.

Licha ya hilo pale inapobidi kutoa ushauri wa awali kabla ya kupima VVU wanaongea blaa blaa tu wakati ni jambo muhimu ambapo usipokuwa makini kumuandaa mpokeaji majibu anaweza kuzimia.

Halafu nyingine zahanati unakuta haina kipimo cha kundi la damu na uwingi wa damu, wanakwambia uende maabara ya mtu binafsi.
 
Folen kubwa
Milango ya daktar mitano ila milango miwili ndio ina madaktari

Ni kukupima MARALIA,UTI ,TYPHOID basi ndio maana watu wengi sana Tz kansa wanakutwa nayo stage ya mwisho maana ukienda hospital ni kupimwa maralia na uti😂😂
Kwenye kupima afya ya uzazi kuna mambo mengi kama VVU na magonjwa mengine ya ngono, lakini ini hawapimi.
 
Habari,

Afya ni miongoni mwa huduma muhimu na msingi katika katika Jamii yoyote. Katika kupata Huduma za Afya kuna michakato na mambo mengi katikati yake.

Je, umeshawahi kukutana na kero gani katika kupata Huduma za Afya Kishingo akusaidie kuisemea?
Vyoo vichafu si hospitali wala stendi maji tiririka hakuna,ndoo moja kikombe cha kuchotea maji kimoja.kwa hali hii tunatibu afya na kuangamiza afya.
Habari,

Afya ni miongoni mwa huduma muhimu na msingi katika katika Jamii yoyote. Katika kupata Huduma za Afya kuna michakato na mambo mengi katikati yake.

Je, umeshawahi kukutana na kero gani katika kupata Huduma za Afya Kishingo akusaidie kuisemea?
 
Hata ini mh
Folen kubwa
Milango ya daktar mitano ila milango miwili ndio ina madaktari
Ukiwaambia unahisi kuumwa wanachojua wao
Ni kukupima MARALIA,UTI ,TYPHOID basi ndio maana watu wengi sana Tz kansa wanakutwa nayo stage ya mwisho maana ukienda hospital ni kupimwa maralia na uti😂😂
 
Yaani unakuta mhudumu anamchoma mtu sindano bila kuvaa glovu.

Licha ya hilo pale inapobidi kutoa ushauri wa awali kabla ya kupima VVU wanaongea blaa blaa tu wakati ni jambo muhimu ambapo usipokuwa makini kumuandaa mpokeaji majibu anaweza kuzimia.

Halafu nyingine zahanati unakuta haina kipimo cha kundi la damu na uwingi wa damu, wanakwambia uende maabara ya mtu binafsi.
😭😭😭😭
 
Mimi niliwahi kwenda Tena hospital ya mkoa nasumbuliwa na macho lakini pia Nina ya masikio nienda toka asbh wakanipima nikaambiwa subri ,,nikaa mpka jioni baada ya hapo nikaambiwa toka hayyupo ,,asee nipiumia sanaa mpkaa basii😥😥
 
Folen kubwa,

Milango ya Daktari mitano ila milango miwili ndiyo ina madaktari.

Ukiwaambia unahisi kuumwa wanachojua wao
Ni kukupima MARALIA, UTI, TYPHOID basi.

Ndiyo maana watu wengi sana Tanzania kansa wanakutwa nayo stage ya mwisho maana ukienda hospital ni kupimwa maralia na UTI.
Very sad kwa Kweli 😢
 
Mimi kuna kipindi nilienda kwenye kituo kimoja cha Afya hapo Dar,

Sikuwa nafahamiana na mtu kabisa, sikuhiyo nilikuwa very smart! wamenitangulia watu kadhaa akaja nesi pale akaniuliza na wewe unatibiwa?

Nilivyomwambia ndio akaenda kwa daktari alivyotoka akaniambia niingie , bila kujali kuna waliokuwa wamenitangulia.

Sikujua kwa nini
 
Nilifiwa na mgonjwa MOI kizembe zembe tu, alipata ajali ya kuanguka. Alikuwa ni mtu ambaye aliwekewa vyuma miaka minne nyuma baada ya kupata ajali ya kuangukiwa na ukuta. Alipona vizuri tu ila aliwekewa chuma mguuni akawa anaishi nacho. Mwaka jana akaja kuanguka akiwa mazoezi. MOI wakasema anatakiwa kufanyiwa upasuaji, maana pale kwenye chuma palivunjika tena. Baada tu ya kulipia gharama za upasuaji wakaanza kujizungusha wakidai wanahitaji kumfanyia vipimo kabla ya upasuaji. Alikaa MOI wiki mbili akipewa panadol tu, hakuna kipimo chochote alichofanyiwa. Mara hali ikaanza kubadilika mpaka kufariki. Siku yake ya mwisho ndio wakajifanya wanampeleka ICU ila ndio ikawa too late
 
Mimi nilienda kuchoma sindano cha ajabu nurse aliyenichoma sindano sijui aliweka sumu kwenye sindano maana baada ya pale nilipofika home nikaanza kuhisi kuishiwa nguvu mara nahisi kutapika yaani nikawa naona kabisa kuzimu inaniita. Aisee nilikimbia fasta kununua maziwa nikanywa ndipo nikaanza kujihisi ahueni mpaka hari kutengamaa, aisee yule Nurse sijui aliniwekea nini kwenye sindano alidhamiria kuniuwa kabisa

Note: ilikua zahanati ya kata yaani ya serikali.
 
Nilifiwa na mgonjwa MOI kizembe zembe tu, alipata ajali ya kuanguka. Alikuwa ni mtu ambaye aliwekewa vyuma miaka minne nyuma baada ya kupata ajali ya kuangukiwa na ukuta. Alipona vizuri tu ila aliwekewa chuma mguuni akawa anaishi nacho. Mwaka jana akaja kuanguka akiwa mazoezi. MOI wakasema anatakiwa kufanyiwa upasuaji, maana pale kwenye chuma palivunjika tena. Baada tu ya kulipia gharama za upasuaji wakaanza kujizungusha wakidai wanahitaji kumfanyia vipimo kabla ya upasuaji. Alikaa MOI wiki mbili akipewa panadol tu, hakuna kipimo chochote alichofanyiwa. Mara hali ikaanza kubadilika mpaka kufariki. Siku yake ya mwisho ndio wakajifanya wanampeleka ICU ila ndio ikawa too late
Wanauzembe wakati fulani na wanajiona kazi yao very unique
 
Back
Top Bottom