Hivi Huduma za Afya za Bure kwa Wazee zinatolewa kwenye Hospitali gani? Mbona kila napoenda nakuta Wazee wanalipishwa tu

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
1700721436817.png

Licha ya Serikali kutoa maelezo kuwa Huduma za Afya kwa Wazee zinatolewa Bure kwenye Vituo vya Afya, uhalisia katika utekelezaji wake umekuwa haueleweki na hivyo, kusababisha kero kwa Wazee wanaofika katika baadhi ya Vituo kupata Huduma.

Mamlaka zitoe maelekezo sahihi kuhusu Huduma hizo kwa Wazee ili ziwe Wazi na zisizo na Milolongo kwa lengo la kuepusha vishawishi na mazingira ya Rushwa. Kinyume na hapo, Huduma zitakuwa chini ya Kiwango au kusababisha usumbufu unaoweza kuepukika.
 
Ilikuwa enzi za kikwete watoto walitibiwa bure mwisho umri wa miaka mitano
 
Hakuna kitu cha bure ndugu ukiweka kitu bure huduma nyingi zitacolapse sana maanmaanbongo wengi wanapenda vitu vya bure kwenye mambo ya msingi hawajali ila kwenye ujinga wanatoa pesa mfano angalia harusi watu wanatoa michango sana ila mtu akiumwa ukiwaambia watu watoe michango hawatoi unaweza kuona ujinga wa kiwango gani upo ktk vichwa vyao narudia hakuna tena kitu cha bure.
 
Hakuna bure mzee
Wanasiasa wanawadanganya sana
Njoo field hakuna bure
 
Unampeka mzee wa miaka 85 hospitali wanakwambia uanzie serikali ya mtaa uje na utambulisho kama kweli ni mzee
 
Vya bure vipo mbinguni. Makazi ya bure. Na kila kitu bure. Huku duniani hakuna cha bure.
 
Licha ya Serikali kutoa maelezo kuwa Huduma za Afya kwa Wazee zinatolewa Bure kwenye Vituo vya Afya, uhalisia katika utekelezaji wake umekuwa haueleweki na hivyo, kusababisha kero kwa Wazee wanaofika katika baadhi ya Vituo kupata Huduma.

Mamlaka zitoe maelekezo sahihi kuhusu Huduma hizo kwa Wazee ili ziwe Wazi na zisizo na Milolongo kwa lengo la kuepusha vishawishi na mazingira ya Rushwa. Kinyume na hapo, Huduma zitakuwa chini ya Kiwango au kusababisha usumbufu unaoweza kuepukika.
Hiyo sera iko midomoni mwa viongozi wa Serikali na CCM. Ila, kiuhalisia hakuna kitu kama hicho nchi hii.
 
Back
Top Bottom