Mtazamo wangu: Misamaha ya matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya ndio chanzo cha huduma kuzorota

Buzi Nene

Senior Member
Feb 10, 2020
139
310
Katika vituo vya kutolea huduma za afya za msingi kwa yaani vituo vyote ambavyo vipo chini ya Tamisemi yani, Zahanati,vituo vya Afya, Hospitali za wilaya kuna utaratibu wa misamaha kwa makundi watoto chini ya miaka 5, wajawazito ikijumlisha na huduma ya kujifungua,na wazee wasio na "uwezo " zaidi ya miaka 60,watu wenye magonjwa ya kudumu etc.

Ukiangalia kwa makini hayo ndio makundi yenye watu wengi nchini lakini ndio yanapata huduma kwa msamaha.

Madhara yake ni vituo kukosa dawa na sisi serikali kutumia gharama kubwa katika kuendesha vituo hivyo.

Kwanini utaratibu huu usiondolewe maana mimba sio ugonjwa na mtu akitaka kuzaa inamaana amejipanga sasa kwanini apewe msamaha.

Hapo kwa wazee angalau panajieleza mana umri umeenda, lakini kwanini walishindwa kujipanga tangu ujanani?

Serikali ibadilishe utaratibu huku chini ifanye kama hospitali za mikoa na zile za kanda
 
Kama tukiwa tunajielewa hicho ndio inatakiwa kifanyike, ila shida ukifanya hivo, kundi la pili wataitumia hio kama hoja ya kisiasa hivyo haitakuwa nzuri,

Ila kama tunataka kuboresha huduma za afya
FUTA uzazi bure,
Futa matibabu ya U5 bure .
Uzee utambuliwe kuanzia miaka 80

Hapo hela zitapatikana
 
Kama tukiwa tunajielewa hicho ndio inatakiwa kifanyike, ila shida ukifanya hivo, kundi la pili wataitumia hio kama hoja ya kisiasa hivyo haitakuwa nzuri,

Ila kama tunataka kuboresha huduma za afya
FUTA uzazi bure,
Futa matibabu ya U5 bure .
Uzee utambuliwe kuanzia miaka 80

Hapo hela zitapatikana
Ni kweli kabisa upo sahihi
 
Back
Top Bottom