Umemsikia MUGABE alichomwambia OBAMA.?

Umemsikia MUGABE alichomwambia OBAMA.?

When People Are Too Open Minded,Their Brains Fall Out.......
 
Mnamsifia mjinga huyo alichukuwa nchi ikiwa first world kaifanya third world na nusu ya wananchi wake wameishia ukimbizini kuwa manamba..poleni kwa ujinga

Kwa sababu kayatamka hayo mtu mweusi ni ujinga. Angeyatamka mzungu yangekuwa ya maana. Da kweli tunajidharau wenyewe. Hapo Mugabe ameonyesha ni jinsi gani anachukia ndoa za jinsia moja na si vinginevyo.
 
Mnamsifia mjinga huyo alichukuwa nchi ikiwa first world kaifanya third world na nusu ya wananchi wake wameishia ukimbizini kuwa manamba..poleni kwa ujinga

Hivi tanzania ikiwa first world huku uchumi wake umeshikiliwa na wageni na zaidi ya 90% ya watanzania hawajui kesho watakula nini, yaani wakiwa watumwa...manamba, na ikiwa Tanzania ikiwa "middle" mwa "world" huku asilimia 90% wanamaisha bora, huku wakiwa wanaongoza uchumi wa nchi yao wakishirikiana na wageni kwa kiasi kidogo sana...KIPI BORA?

Kwa taarifa yako...Mugabe alichukua optional ya pili...iliyowajali wazimbabwe wengi!

Mzee (Mugabe) naye upungeze ukali wa maneno! Hata hivyo safi kwa za 'usoni' kwa hao waeneza uovu.
 
Hapa sasa ndio nimeamini wewe ni Punga zeze, tulia dawa anayokupa Prof. mjasiria ikuingie vizuri, shwain.
Wewe huwezi kunipa dawa hadi umtegemee mjasiria?
Jenga hoja acha kutukana, Mwalimu Nyerere alishawahi kusema "argue, dont shout".
 
Ngoja mimi nikubaliane na wewe. Je hao wanawake wakishavaa mavazi kwa kutumia vigezo vyako wanapatiwa haki zao za kimsingi za kibinadamu au kutambuliwa mchango wao katika jamii?
Mkuu hilo suala la kutambuliwa mchango na kupewa haki zao ni suala linalojitegemea na halitegemei wamevaaje. Kimsingi mimi sipingi wanawake kupatiwa haki zao. Na ikitokea wanawake wananyimwa haki zao kwa kuwa tu ni wanawake nipo tayari, na nitakuwa mstari wa mbele kupinga.
 
Si ndiyo hicho!!!.
Mimi sijapotosha chochote, unachosema ndicho ninachosema, hoja kuu hapa ni kuonekana unawapinga wakubwa wa dunia, basi.
Mugabe alishasoma saikolojia ya waafrika, huhitaji kuumiza kichwa. Sema tu hapana kwa wanachosema wazungu, bila kujali hiyo hapana inawasaidiaje wananchi wako, you win Africans, utaonekana kidume. "Kambishia Obama"
Mugabe ataendelea kung'ang'ania madaraka na kuifukarisha nchi, huku yeye na familia yake wakiishi maisha mazuri.
Kwa taarifa yako hilo si suala la waafrika tu. Ni suala la binadamu yeyote anayejiona kuwa yu mnyonge. Ndiyo maana waafrika hawa hawa wakiona mchina kamvimbia mmarekani huwa wanashangilia pia. Na hii sio Afrika tu nenda hata Amerika ya kusini ni hivyo hivyo. Sema kwa kuwa wewe labda unaishia kusoma habari za hapa Afrika tu ndiyo maana hujui!!!!!
 
Dalili za kushindwa hoja hizi! Mambo ya uchi umeyaleta mwenyewe halafu sasa unanambia niachane nayo. Unaanza kuhaha na kubadili magoli. Hamna shobo. Twende hivyo hivyo tu.
Uchi tafsiri yake inategemea mtu mmoja hadi mwingine, niliposema uchi mara ya kwanza nilimaanisha kwa maana ya kuweka wazi vitu ambavyo vimekatazwa na hiyo sheria ya Uganda. Hii ina maana kwamba mapaja, vitofu, matiti na vingine kama vipo. Sasa wewe kwa kuwa umeshaendelea zaidi kwenye suala la uchi, hivyo kwako sio uchi na mimi kwa kuliona hilo sikuona umuhimu wa kuanza kujadili maana ya uchi, ndiyo maana nikasema basi isiwe tabu tuachane na habari za uchi, tuzungumzie hata hilo la mapaja.

Kama wapo ambao hawatopenda kuona vivyo hivyo tupo ambao tunapenda kuona mapaja. Wasiopenda, kama nilivyosemaa (andika) awali wana hiari ya kutoangalia. Wanaweza wakafumba macho, wakageuza vichwa kuangalia mengine, au hata kuinamisha kichwa kama hawana kingine cha kutazama.
Nimeshakupa tofauti ya kuona na kutazama, hakuna hiyari kwenye kuona au hujaelewa bado??!!!!

Sasa ukigeuza shingo na kwa bahati mbaya ukaona kitu ambacho hakikupendezi machoni ya nini tena kuendelea kuangalia? Si ugeuze tu shingo yako kwingine. We vipi wewe?
Tatizo ndio liko hapo unakuwa ushaona wakati hutaki na hapo ndio umeingilia uhuru wa mtu wa kuona, we vipi wewe?

Unavyoamua kutazama runinga au kuangalia runinga? Unaanza kujichanganya mwenyewe kwa maneno yako!!

Unachofanya sasa ni kutenganisha unywele tu!!
Kwa hiyo kwako kuangalia na kuona ni sawa??
 
Swahili is not wide enough to express deep wisdom.
Unaona sasa, kwa maneno haya unaonesha ni jinsi gani umetudharau waswahili. Ushaona sisi hatuna busara kwa hiyo umeamua kuja kutuletea busara za wazungu sio. Sasa kwa taarifa yako waswahili wana busara za kutosha tu na wanaweza kuamua kuishi wanavyoona wao inafaa hata kama wewe na busara zako za kizungu utawaona wajinga!!!!

Aisee......mambo mengine uwe unafikiri kabla ya kuandika!!!
 
Kwa taarifa yako hilo si suala la waafrika tu. Ni suala la binadamu yeyote anayejiona kuwa yu mnyonge. Ndiyo maana waafrika hawa hawa wakiona mchina kamvimbia mmarekani huwa wanashangilia pia. Na hii sio Afrika tu nenda hata Amerika ya kusini ni hivyo hivyo. Sema kwa kuwa wewe labda unaishia kusoma habari za hapa Afrika tu ndiyo maana hujui!!!!!
Sasa mkuu hatutakiwi kufuata mob psychology tu, tunatakiwa tujiulize, huyo Mmarekani tunayetaka kumvimbia tunamvimbia kwa mambo ya maana na tunatoa hoja za msingi tunapomvimbia, au tunaropoka upuuzi tu kama Mugabe?

Je, kumvimbia kwetu kunaleta tija katika mataifa yetu au tunaishia kumvimbia tu huku tukisababisha SUPERHYPERINFLATION katika nchi zetu kama alivyofanya Mugabe hadi kufikia kiasi cha mayai matatu ya kuku kununuliwa kwa ZimDollar bilioni mia moja?( sio utani, imetokea kweli Zimbabwe).

Na la muhimu kuliko yote, kwa nini tunaacha kuvimbia vitu vya msingi tunavimbia vitu vya kipuuzi tu(kama hili la maisha binafsi ya mahusiano ya watu).

Kwa nini kwa mfano, hatuwavimbii wachina ambao kwa sasa ndiyo wanyonyaji wakubwa wanaochuma rasilimali za Afrika?
Wachina sasa wanaingia mikataba mingi ya kilaghai kama enzi zile za akina Karl Peters na wenzake, kwa nini hatupingi hii mikataba ya miaka mia moja isiyokuwa na tija kwa nchi zetu na badala yake tunakuwa wakali kupitiliza kwenye mambo ya ushoga na nguo fupi?
 
Unaona sasa, kwa maneno haya unaonesha ni jinsi gani umetudharau waswahili. Ushaona sisi hatuna busara kwa hiyo umeamua kuja kutuletea busara za wazungu sio. Sasa kwa taarifa yako waswahili wana busara za kutosha tu na wanaweza kuamua kuishi wanavyoona wao inafaa hata kama wewe na busara zako za kizungu utawaona wajinga!!!!

Aisee......mambo mengine uwe unafikiri kabla ya kuandika!!!
Tafsiri isiyo rasmi ya sentensi hiyo ni kuwa Kiswahili hakijitoshelezi katika kujadili baadhi ya mambo ya kitaaluma kiundani. Naomba unielewe, hapa sizungumzii watu nazungumzia lugha.
Kusema ukweli sio dharau, ni kwa nia njema tu, kiswahili kimekopa maneno mengi ya kibantu, kiarabu, kichina na katika hali ya kuonyesha kuwa kiswahili sio kipana na hakijitoshelezi, hata Mtukufu rais, Kikwete, pamoja na His excellency Pinda, wakitaka kusisitiza jambo huwa muda mwingine wanalazimika kutumia maneno ya kiingereza.

Maprofesa waliambiwa watafsiri vitabu vya kitaaluma ili viwe katika lugha ya kiswahili wameshindwa, nitaweza mimi!!??
Na matokeo yake sasa, kuna mpango wa kutumia lugha ya kiingereza mashuleni kama lugha ya kujifunzia kuanzia shule za msingi na baadhi ya shule za serikali jijini Dar es salaam zimeshaanza.
 
Sasa mkuu hatutakiwi kufuata mob psychology tu, tunatakiwa tujiulize, huyo Mmarekani tunayetaka kumvimbia tunamvimbia kwa mambo ya maana na tunatoa hoja za msingi tunapomvimbia, au tunaropoka upuuzi tu kama Mugabe?
Kuna mambo ambayo kusema kuwa ni la maana au sio hutegemea na jamii husika. Ukienda India kwa mfano, mwanamke kuolewa akiwa bikra ni jambo la maana sana lakini ukiwa Marekani ni kitu ambacho watu hata hawafikirii. Kwa hiyo inabidi ujifunze kuielewa jamii husika kabla ya kurukia kuamua kuwa jambo fulani ni la maana au sio.

Je, kumvimbia kwetu kunaleta tija katika mataifa yetu au tunaishia kumvimbia tu huku tukisababisha SUPERHYPERINFLATION katika nchi zetu kama alivyofanya Mugabe hadi kufikia kiasi cha mayai matatu ya kuku kununuliwa kwa ZimDollar bilioni mia moja?( sio utani, imetokea kweli Zimbabwe).
Hapa kuna mambo mawili. Kuna suala la ushoga ambalo kwako halina maana ila kwa wengi waliosoma huu uzi lina maana. Halafu kuna suala la uchumi. Kimsingi kukubaliana au kutokubaliana na ushoga hakuna uhusiano na hiyo "super hyper inflation" (Japokuwa kuna watu wanaweza kujenga hoja kuwa kuna uhusiano, kutokana na ukweli kuwa wanaamini maadili na uchumi wa jamii husika vinahusiana). Kwa hiyo utaona kuwa suala la Mugabe kusababisha tatizo la kiuchumi halina uhusiano wowote na yeye kupinga ushoga. Kwa mtu ambaye anaamini ushoga ni kosa, hawezi kukaa kimya kwa kuwa amevurunda kwenye uchumi (hususan kama kweli anaamini hivyo na zaidi ya hivyo, kupinga kwake kunaendelea kumpa nguvu ya kisiasa). Kwa hiyo mkuu hata kama suala hili Mugabe analitumia kisiasa sio tatizo maana ndivyo jamii inavyotaka.

Na la muhimu kuliko yote, kwa nini tunaacha kuvimbia vitu vya msingi tunavimbia vitu vya kipuuzi tu(kama hili la maisha binafsi ya mahusiano ya watu).
Nimeshakujibu hapo juu kuhusu ni kwa vipi jambo fulani linaweza kuwa la msingi au la! Tatizo kubwa naloliona ni kujaribu kutumia viwango vya wazungu kuamua lipi ni la msingi au si la msingi. Na ndiyo maana ukiangalia wengi wa wale wanaoona masuala ya mavazi na ushoga si ya msingi ni watu ambao wanaishi au wameishi ughaibuni kwa muda mrefu. Hawa hufikia mahali hufikiria kuwa maadili ya jamii zote yanatakiwa kufuata mifumo ya kiliberali (mfano mzuri ni Kiranga na Ngabu, sina hakika sana kama wewe sio "mghaibu" pia).

Kwa nini kwa mfano, hatuwavimbii wachina ambao kwa sasa ndiyo wanyonyaji wakubwa wanaochuma rasilimali za Afrika?
Wachina sasa wanaingia mikataba mingi ya kilaghai kama enzi zile za akina Karl Peters na wenzake, kwa nini hatupingi hii mikataba ya miaka mia moja isiyokuwa na tija kwa nchi zetu na badala yake tunakuwa wakali kupitiliza kwenye mambo ya ushoga na nguo fupi?
Mkuu kuamua kuwavimbia au kutowavimbia wachina hakuondoi umuhimu wa kukataa ushoga kama jamii inaona hivyo. Wewe ulitakaje tuachane na ushoga tukomae na wachina kwanza?
 
Tafsiri isiyo rasmi ya sentensi hiyo ni kuwa Kiswahili hakijitoshelezi katika kujadili baadhi ya mambo ya kitaaluma kiundani. Naomba unielewe, hapa sizungumzii watu nazungumzia lugha.
Kusema ukweli sio dharau, ni kwa nia njema tu, kiswahili kimekopa maneno mengi ya kibantu, kiarabu, kichina na katika hali ya kuonyesha kuwa kiswahili sio kipana na hakijitoshelezi, hata Mtukufu rais, Kikwete, pamoja na His excellency Pinda, wakitaka kusisitiza jambo huwa muda mwingine wanalazimika kutumia maneno ya kiingereza.

Maprofesa waliambiwa watafsiri vitabu vya kitaaluma ili viwe katika lugha ya kiswahili wameshindwa, nitaweza mimi!!??
Na matokeo yake sasa, kuna mpango wa kutumia lugha ya kiingereza mashuleni kama lugha ya kujifunzia kuanzia shule za msingi na baadhi ya shule za serikali jijini Dar es salaam zimeshaanza.
labda useme hujui kiswahili utaeleweka. Kiswahili kinaweza kisijitosheleze kwa baadhi ya mambo hususani ya kiteknolojia lakini nina hakika haya tunayojadili hapa yanajadilika kwa kiswahili bila shida yeyote.
 
Huyu ni kidume haswaa, hizo takwimu za wamagharibi zinakufaa wewe, Mugabe sio kama Kagame.
Baba V
Siku hizi umekomaa kisiasa; hakuna kiongozi ambaye ni 100%; Mugabe anasiamamia mila na desturi za kiafrika; mambo ya kulazimishwa kukubali taratibu za maisha ya mtu mwingine kwasababu ya umaskini hicho ndicho anachokataa; hao wanaongelea kuanguka uchumi wa Zimbwabwe ni waongo sababu kubwa ni kutoafikiwa kwa makubaliano ya Lancaster; sio kila linalofanyika nchi za magharibi ni jema kwa waafrika; kuiga kuna mipaka yake; siamini kama Nyani Ngabu atafurahia iwapo mtoto wake wake kiume amletee mwanaume ati anataka kumuoa!
 
Last edited by a moderator:
"If Obama wants me to allow gays marriage in Zimbabwe,I should marry him first to show the good example"-Robert Mugabe..

Ndio huyu huyu mzee,ambaye alipoulizwa na wanahabari wa Uingereza kuwa kwanini asiachie ngazi ilhali ameshazeeka, aliwauliza kama walishawahi kumuuliza swali kama hilo malkia wao..

Salute kwako uncle mugabe..

Namkubali sana Mugabe.
 
Hakuna mtu amesema muwe mashoga ,tatizo ni pale mnapoanza kuwanyanyasa na kuwafunga for a reason they are gay,hii haikubaliki na mtabadilika kwa nguvu hata kwa kukatiwa misaada ikibidi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom