Kiongozi mzuri ni yule anaangaliwa kwa uongozi na matendo yake kwa ujumla na hasa kiuchumi na siyo kwa kudonoa donoa kwa maana kwamba, kama siasa ni safi basi zitapelekea hata jamii kuwa na uchumi endelevu.
Viongozi wengi wa nchi za Kiafrika wanaficha mapungufu yao ya kiuongozi kwa kusingizia nchi za Magharibi kama ndiyo chanzo cha matatizo au mapungufu yao.
Yes, Nchi za Magharibi zinaweza zikawa wamechangia matatizo katika taifa la Zimbabwe lakini huwezi kuzilaumu katika matatizo hayo kwa vile lilikuwa ni jukumu la viongozi wa Zimbabwe kuyakataa au kuyakubali.
Ni ajabu kumwita kiongozi ana msimamo mzuri au shujaa kwa maswala ambayo ni uamuzi wa binadamu ndani ya vyumba vyao kwa kiwango ambacho mpaka yanasahaulika maswala ambayo niya msingi kabisa nchini kama vile mwenendo wa kiuchumi kwa kila raia.
Sisi Waafrika ni wazuri sana katika kazi ya kushughurika (kushadadia) na mambo ambayo hayana maana katika kipimo cha umuhimu kitaifa na kimataifa.
Ni jambo la kusikitisha kuwa kwa nchi za Kiafrika kuwa masikini siyo tatizo kubwa na kwa maana hiyo, kuondoa umasikini siyo jukumu la kwanza kwa hizi nchi. Maswala ya unyumba (mapenzi) ndiyo swala muhimu sana na kwa maana hiyo, hili ni jukumu la kwanza kupambana nalo. Haishangazi kwa Rais Mugabe kuitwa mpambanaji (hero)kwa sababu anapambana na swala ya unyumba (mapenzi)
Mfano halisi uko hapa kwenye vijiwe vya Jamiiforums. Ukileta thread ya mwanasiasa kuhusu mapenzi, itapata wachangiaji wengi sana lakini ukileta thread ya mwanasiasa kuhusu uchumi, hiyo itakuwa kwenye ignore list na wengi.
Usishangae hiyo sentensi inaweza kumfanya Rais Mugabe kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Zimbabwe.
Matatizo yetu ni makubwa na yako ndani kabisa na ndiyo hayo yanayo akisi utendaji wa viongozi wetu.