Umemsikia MUGABE alichomwambia OBAMA.?

Umemsikia MUGABE alichomwambia OBAMA.?

Kuna mambo ambayo kusema kuwa ni la maana au sio hutegemea na jamii husika. Ukienda India kwa mfano, mwanamke kuolewa akiwa bikra ni jambo la maana sana lakini ukiwa Marekani ni kitu ambacho watu hata hawafikirii. Kwa hiyo inabidi ujifunze kuielewa jamii husika kabla ya kurukia kuamua kuwa jambo fulani ni la maana au sio.


Hapa kuna mambo mawili. Kuna suala la ushoga ambalo kwako halina maana ila kwa wengi waliosoma huu uzi lina maana. Halafu kuna suala la uchumi. Kimsingi kukubaliana au kutokubaliana na ushoga hakuna uhusiano na hiyo "super hyper inflation" (Japokuwa kuna watu wanaweza kujenga hoja kuwa kuna uhusiano, kutokana na ukweli kuwa wanaamini maadili na uchumi wa jamii husika vinahusiana). Kwa hiyo utaona kuwa suala la Mugabe kusababisha tatizo la kiuchumi halina uhusiano wowote na yeye kupinga ushoga. Kwa mtu ambaye anaamini ushoga ni kosa, hawezi kukaa kimya kwa kuwa amevurunda kwenye uchumi (hususan kama kweli anaamini hivyo na zaidi ya hivyo, kupinga kwake kunaendelea kumpa nguvu ya kisiasa). Kwa hiyo mkuu hata kama suala hili Mugabe analitumia kisiasa sio tatizo maana ndivyo jamii inavyotaka.


Nimeshakujibu hapo juu kuhusu ni kwa vipi jambo fulani linaweza kuwa la msingi au la! Tatizo kubwa naloliona ni kujaribu kutumia viwango vya wazungu kuamua lipi ni la msingi au si la msingi. Na ndiyo maana ukiangalia wengi wa wale wanaoona masuala ya mavazi na ushoga si ya msingi ni watu ambao wanaishi au wameishi ughaibuni kwa muda mrefu. Hawa hufikia mahali hufikiria kuwa maadili ya jamii zote yanatakiwa kufuata mifumo ya kiliberali (mfano mzuri ni Kiranga na Ngabu, sina hakika sana kama wewe sio "mghaibu" pia).


Mkuu kuamua kuwavimbia au kutowavimbia wachina hakuondoi umuhimu wa kukataa ushoga kama jamii inaona hivyo. Wewe ulitakaje tuachane na ushoga tukomae na wachina kwanza?

Nimeeleza ni jinsi gani Waafrika wanaweza kuhakikisha raia wao wanapata human rights zao na Wamagharibi hawaendelezi "cultural imperialism".

Hunisomi, kama unanisoma hunielewi, kama unanielewa ni mbishi tu.

Quite possibly hunisomi, hunielewi na ni mbishi tu pia!
 
Nimeeleza ni jinsi gani Waafrika wanaweza kuhakikisha raia wao wanapata human rights zao na Wamagharibi hawaendelezi "cultural imperialism".

Hunisomi, kama unanisoma hunielewi, kama unanielewa ni mbishi tu.

Quite possibly hunisomi, hunielewi na ni mbishi tu pia!

Kiranga umekurupuka hapa, nadhani umekosea ku-quote, hebu jaribu tena.
 
Mnamsifia mjinga huyo alichukuwa nchi ikiwa first world kaifanya third world na nusu ya wananchi wake wameishia ukimbizini kuwa manamba..poleni kwa ujinga

Sipendi na nalaani ushoga, sipendi kutawaliwa na nalaani kutawaliwa, sipendi kunyanyaswa na nalaani mtu kunyanyasika kwa sababu yeyote Ile (mimi si Mungu nitapata wapi haki ya kumhukumu mtu ikiwa mimi si mkamilifu) LAKINI PAMOJA NA HAYO YOTE NAAMINI MUGABE NI MSALITI WA UHURU WA AFRIKA!
 
Kiranga umekurupuka hapa, nadhani umekosea ku-quote, hebu jaribu tena.

Hapana, wewe ndiye umekosea kufikiri nimekosea ku quote.

Umetaja jina langu in vain.

Lazima nikublast.

Soma post yako mwenyewe.

Kama nilivyoandika, hunisomi, hunielewi halafu mbishi.
 
"Inferiority Complex"??!! Endelea kuota....(Unajiona ukoo juu sana eeh?!!!!!)

Turudi kwenye mada. Ngoja nikupe mfano wa kawaida kabisa labda utaelewa, Chukulia una baba ambaye ni bazazi haswa, kuacha hela ya msosi nyumbani ni majanga pamoja na kuwa anakulimisha, saa nyingine anakupiga na pengine akinunua chakula anakusimanga. Kwa upande mwingine kuna bazazi jingine mtaani tuliite Bzk lina nguvu sana kiasi kwamba likiamua linamlawiti yeyote bila ridhaa yake hata kama yeye na familia yake yote watapinga. Sasa chukulia kwamba imefika kipindi imeshazoeleka kiasi kwamba kila mtu anaogopa kupinga na huyu Bzk anafanya anachotaka bila upinzani.

Kwa maana hiyo basi siku yoyote Bzk anaweza kugonga mlango wenu na kutaka huduma ya 0713 kutoka kwako wewe Kiranga, chukulia kuwa hupendelei wala hutaki kusikia hizi habari (kwa kifupi huwezi hata kufikiria kufanyiwa hivyo). Lakini kwa nguvu alizonazo Bzk unajua kuwa akigonga mlango na kuomba mzigo lazima utatoa japo hupendi. Bahati nzuri kwako au mbaya kwa Bzk, baba yako ambaye naye ana ubazazi wake anatangaza hadharani kuwa, nyumbani kwake hawezi kuruhusu Bzk afanye chochote na akijaribu ama zake ama za Bzk. Wewe Kiranga hutamshangilia baba yako japokuwa ni bazazi?

Kama hutamshangilia baba yako kwa mfano huu hapo juu basi, ninakubaliana nawe kuwa wanaoshabikia hii habari hawako sahihi.

Nashangaa kwanini watu hawahoji kwanini Obama atuamulie misimamo ya ushoga kwenye nchi zetu matokeo yake wanamshambulia Mugabe kwa kauli yake (Kama ni ya kweli).

Mugabe ana matatizo yake, haimaanishi apingwe kwa kila kitu kwa sababu ameshindwa kutatua matatizo Zimbabwe.
 
Nimeeleza ni jinsi gani Waafrika wanaweza kuhakikisha raia wao wanapata human rights zao na Wamagharibi hawaendelezi "cultural imperialism".

Kuna njia nyingi sana za kufanukisha hilo lengo mkuu, Mugabe huenda akawa na approach mbovu lakini anachoonyesha kwenye hii kauli yake ni msimamo wake kuhusu "Cultural imperialism".
 
Hivi kwanini hizi european nations na Marekani siwaskii viongozi wao wakitaka kuleta hizi habari za gay rights uarabuni lakini wanazipigia debe zaidi huku kwetu maskini! Why?
 
"If Obama wants me to allow gays marriage in Zimbabwe,I should marry him first to show the good example"-Robert Mugabe..

Ndio huyu huyu mzee,ambaye alipoulizwa na wanahabari wa Uingereza kuwa kwanini asiachie ngazi ilhali ameshazeeka, aliwauliza kama walishawahi kumuuliza swali kama hilo malkia wao..

Salute kwako uncle mugabe..

Ha haaaaaa uyo mzee ni kiboko yao Africa asee kanifurahishajee
 
Kuna njia nyingi sana za kufanukisha hilo lengo mkuu, Mugabe huenda akawa na approach mbovu lakini anachoonyesha kwenye hii kauli yake ni msimamo wake kuhusu "Cultural imperialism".

Huwezi kuwa na maana kama unapinga cultural imperialism kutokwa magharibi wakati unaendeleza internal imperialism kutoka Ikulu.

Mugabe anazuga tu, na kama nilivyosema, hawezi kusema kafanya vizuri kwenye uchumi wala maendeleo, anabakia kubweka kuhusu habari za ushoga kama smokescreen ili waafrika wasiofikiri sana wamuite "kidume" wakati wananchi wake wanakufa kwa njaa, UKIMWI na kupigwa na askari wake.
 
Nashangaa kwanini watu hawahoji kwanini Obama atuamulie misimamo ya ushoga kwenye nchi zetu matokeo yake wanamshambulia Mugabe kwa kauli yake (Kama ni ya kweli).

Mugabe ana matatizo yake, haimaanishi apingwe kwa kila kitu kwa sababu ameshindwa kutatua matatizo Zimbabwe.

Kuna watu wana credibility na moral high ground ya kuwabana wamagharibi (kwenye reciprocity na authenticity, siyo gay rights, gay rights are human rights), sio Mugabe. Mugabe at this point kwa wafuatiliaji wa mambo watamuona ni "trapeze artist" tu anaye capitalize kwenye ujinga wa waafrika.

By "watu" unamaanisha nani?

Mimi nishahoji hapo awali kwenye thread hii hii, kwamba kama wamagharibi wako concerned sana na human rights, wasiishie tu kutaka waafrika wahalalishe ushoga, bali pia na wao wamagharibi wahalalishe ukewenza ili kusudi waafrika wanaotaka kuoa wake wengi magharibi waweze kufanya hivyo bila kuvunja sheria as long as wanakubaliana na wake zao.

This is a legitimate question which I have never heard raised.

Kama wamagharibi lengo lao ni haki za binadamu tu, na sio kutaka waafrika wafuate wanachotaka wao, bila wao kufuata utamaduni wa waafrika, there should be a mutual exchange of cultures and mores.

Waafrika wakubali kuhalalisha ushoga ili kutowabania mashoga haki zao za binadamu, na wamagharibi wakubali habari za ukewenza ili kutowabania wanaotaka ukewenza haki zao za binadamu.

Marekani kuna sehemu wazungu wanaoa wakewenza kisirisiri kwa sababu sheria ya nchi hairuhusu mtu mmoja kuwa na mke zaidi ya mmoja.

Sasa rais Mwinyi akiamua kwenda kukaa Marekani afundishe wanafunzi Boston College hapo kwenye fellowship ya marais wa zamani wa Africa na yeye ana wake zake wawili, akitaka aende na wake zake wote, atakuwa anavunja sheria za Marekani kimsingi.

Nilishambana mama mmoja Mmarekani kwa nini Marekani inasemekana kuwa na uhuru sana lakini hairuhusu ndoa za zaidi ya watu wawili, alishindwa kunijibu. Hakutegemea kabisa swali kama hilo. Kwake yeye ndoa ni mtu mmoja na mwingine axiomatically. Which is a huge fallacy anyway kwa sababu wao wana practice serial monogamy. Unaoa mmoja, unamuacha unaoa mwingine unaacha etc, sisi (baadhi) tuna practice bigamy, unaoa wake wengi kwa wakati mmoja. Whether the distinction has a difference or not is highly questionable.

Kwa nini viongozi wa Afrika wanashindwa kuongelea hili suala na mengine kama haya kuonesha kwamba haya masuala ya haki za binadamu si lazima yawe yanatoka magharibi kuja Afrika tu? Kwamba kuna sheria nyingine za magharibi zinaminya haki ya za binadamu kuliko tamaduni za kiafrika?

Hapo ndipo naona hawa viongozi wetu katika vikao vingi sana hawawezi ku negotiate on an equal footing kama viongozi wa sovereign nations.

Kikwete kahojiwa na Christian Amanpour mpaka anatia huruma alivyokuwa anajibu maswali.

Anaulizwa kuhusu kukubalika kwa ushoga anasema watu wetu hawawezi kukubali haya mambo leo lakini wakipewa muda watakubali tu. Anaulizwa wewe vipi unakubali? Anajibu hawezi kusema kwa sasa.

Rais mzima anakuwa anajiuma uma kama kigori mwenye haya!

NB: Kwa vile mimi naamini katika usawa wa wanawake na wanaume kwa kiwango kinachowezekana kwa maumbile, habari zote za "ukewenza" zichukuliwe pia kumaanisha "umewenza" kwa mujibu wa maelewano ya watu wazima watakaohusika.
 
Hata kama sitafurahia haina maana nitamchagulia au kumpangia namna ya kuishi ilhali akiwa ni mtu mzima.

kama upo kwenye game poa kwenye hatuoni kosa la Mugabe; tatizo sio kumpangia ni kumfundisha mtoto maadili kulingana na taratibu na mila za ulipotoka! Waafrika tuna mila na tamaduni zetu; Obama alipokwenda Senegal alipewa ujumbe huo na raisi wa Senegal; Waafrika tuna mengi sana ya kujifundisha kutoka kwenye nchi zilizoendelea; hili la ushoga halituhusu!
 
kama upo kwenye game poa kwenye hatuoni kosa la Mugabe;

Hold up, hold your horses for a minute. Kama nipo kwenye game gani? Maana mimi sikubaliani na Mugabe wala Museveni katika hiyo misimamo yao ya kupangia watu wazima namna ya kuishi.

tatizo sio kumpangia ni kumfundisha mtoto maadili kulingana na taratibu na mila za ulipotoka!

Mimi nilidhani tunazungumzia watu wazima wenye utashi wa kuamua jinsi ya kuishi maisha yao wapendavyo wao. Ya watoto yamekujaje tena hapa?

Waafrika tuna mila na tamaduni zetu;

Zipi hizo?

Obama alipokwenda Senegal alipewa ujumbe huo na raisi wa Senegal; Waafrika tuna mengi sana ya kujifundisha kutoka kwenye nchi zilizoendelea; hili la ushoga halituhusu!

Ushoga mbona upo Afrika tokea enzi na enzi. Kwa hiyo siyo kwamba ni jambo geni ambalo tunajifunza kutoka kwenye nchi zilizoendelea.

Na kama kuna jambo jema la kujifunza kutoka kwenye hizo nchi zilizoendelea basi ni hilo la kuacha watu waishi watakavyo ili mradi hawaingilii maisha ya wengine.

Haingii akilini kabisa kujinaisha (criminalize) maamuzi ya mtu mzima yanayomhusu yeye mwenyewe. Ushoga wa mtu wewe unakuhusu nini?

Ila pia niseme kwamba hizo nchi zilizoendelea nazo zina mapungufu vile vile. Kuna kipindi huko Uingereza ushoga ulikuwa ni kosa la jinai. Majuzi tu hapa malkia Elizabeti katoa msamaha posthumuosly kwa Alan Turing, mwanahisabati wa Kiingereza ambaye pia anajulikana kama baba wa kompyuta za kisasa na aliyeweza kuzivunja code za Wajerumani za Enigma, jambo ambalo wanahistoria wanadai lilipelekea kumalizwa kwa vita vikuu vya pili vya dunia.

Huyo bwana baada ya kupatikana na hatia ya kosa la matendo ya kishoga alihasiwa (castrated) mwaka 1952. Miaka miwili baadaye akajiua.

Mwezi ulopita malkia kampa msamaha. Sijui hata kwa nini hata ilichukua muda wote huo kumpa msamaha achilia kupatikana na hatia ya kosa ambalo kwa kweli si kosa hata kidogo.

Lakini, kinachotafautisha wenzetu na sisi ni kwamba wao huwa wanakiri makosa yao na kurekebisha pale wanapoweza. Uingereza imeshaifutilia mbali hiyo sheria iliyokuwa inajinaisha ushoga na viongozi wa hiyo nchi wanakiri kuwa hiyo sheria haikuwa ya haki hata kidogo.
 
Ditto!

Kwa siku mbili tatu hizi Museveni kapewa plaudits na watu humu kwa kinachodaiwa kutia saini muswada wa sheria inayokataza wanawake nchini Uganda kuvaa nguo fupi.

Kaitwa mfano wa kuigwa, kiongozi imara, na sifa nyinginezo kama hizo.

Watu hawaoni ubaya wowote wa hiyo sheria na ghafla bin vuu ni kama wamesahau kama lijamaa ni lidikteta na just like that, with the stroke of a pen, limegeuka kuwa shujaa!!

Viwango vya Waafrika ni vya chini sana aisee.

MIAFRIKA ndivyo Mlivyo...
 
kama upo kwenye game poa kwenye hatuoni kosa la Mugabe; tatizo sio kumpangia ni kumfundisha mtoto maadili kulingana na taratibu na mila za ulipotoka! Waafrika tuna mila na tamaduni zetu; Obama alipokwenda Senegal alipewa ujumbe huo na raisi wa Senegal; Waafrika tuna mengi sana ya kujifundisha kutoka kwenye nchi zilizoendelea; hili la ushoga halituhusu!

PUNGUZA mahaba Mgando wewe!
Kama ushoga Tanzania upo kabla ya hao weupe kuja Afrika.Tunapishana nao kila leo kwenye Masherehe,kumbi za Starehe nk.

Tena watu kama nyie ndio wateja wao .
 
Kule kwao hawa watu
mugabe, kagame, na museveni hawamwagiwi sifa kama wanazopataga humu JF so naamini hata Rais wetu kuna wat huko nje wanatamani angekuwa anawaongoza.Jiwe walilolikataa waashi! Endeleeni kumwaga sifa za Mugabe..........
 
Mugabe anatakiwa aongoze na tz wenye mikataba ya kishenzi awatoe.
 

Attachments

  • 1393126993649.jpg
    1393126993649.jpg
    17.8 KB · Views: 35
Hapana, wewe ndiye umekosea kufikiri nimekosea ku quote.

Umetaja jina langu in vain.

Lazima nikublast.

Soma post yako mwenyewe.

Kama nilivyoandika, hunisomi, hunielewi halafu mbishi.
Haya mkuu kama hauko kwenye lile kundi nililokuweka samahani sana. Tunajadili tu hapa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom