Umemsikia MUGABE alichomwambia OBAMA.?

Umemsikia MUGABE alichomwambia OBAMA.?

Kwa hiyo kutohadaiwa ni kukubaliana na kile unachofikiri wewe kuwa ni sahihi??!!! Kama wanawake wanamuunga mkono wewe unashangaa nini?? Umeambiwa kuwa wanawake wote ni lazima waunge mkono uvaaji wa vimini??!! Kwani kama unaona kuvaa chupi barabarani ni sawa, kuna tatizo gani mwingine akiona si sawa?? Iweje utake watu wote wawe na maoni kama yako??
Hicho ndicho tunachokipinga, kulazimisha maoni yako yafuatwe hadi unaweka kuwa ni sheria. Utampangiaje mtu mzima namna ya kuvaa!??
 
Kwani ushoga ni nini?
Mbona wanaume kibao wanawafanya wake zao kinyume na maumbile hamuoni kama ni kitu cha ajabu?
Kuonyesha kuwa waafrika akili zina hitlafu, wanamuona shoga ni muovu kuliko mwizi na hata muuaji.

Mijadala kibao ilishafanyika bungeni kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo ufisadi na vitu kem kem, lakini Wenje alipoibua hoja kuwa chama kimoja cha siasa nchini, itikadi yake inatambua haki za mtu mmoja mmoja wakiwemo mashoga moto uliwaka haijawahi kutokea, Wenje akazuiwa kusoma hadi atoe hicho kipengele. Mwandishi Ezekiel Kamwaga alishawahi kuuliza katika makala zake iwapo ushoga ni mbaya kuliko ufisadi.

Ni ufinyu wa fikra unaoashiria hitlafu katika akili kuamini kuwa ushoga ni jambo baya kuliko yote katika nchi na ni kitu ambacho watawala wanatakiwa kutoa kipaumbele katika kupambana nacho.
Tatizo unajadili haya mambo bila kujali kuwa kuna mambo ya kiroho. Of coz ukiondoa mambo ya kiroho na maadili ushoga, uzinzi, kutembea uchi (nina maana bila ya nguo), sio tatizo kabisa. Ila kumbuka hata kama wewe huamini mambo ya kiroho na kimaadili, jamii inayoamini mambo hayo inayapa uzito mkubwa. katika jamii hizi, ni kawaida kuamini kuwa inawezekana nchi nzima ikageuzwa juu chini kwa kuwa tu kuna watu wana tabia za kishoga. Kwa maana hiyo kwa binadamu yeyote mwenye akili hawezi kuangalia tu wakati anaona kuna watu wanataka kuangamiza jamii yake. Ni sawa na wewe uone mtu anawasha kibatari pembeni ya nyumba ya nyasi, ni wazi huwezi kukaa kimya!!!Kwa hiyo usikurupuke ukidhani kuwa kila mtu anaangalia ushoga kwa namna unavyoona wewe, vinginevyo wewe usiyeelewa jamii hizi ndio utakuwa kiroja.

Kumbuka werevu mwingi huondoa maarifa.
 
Inawezekana kweli una hitilafu kichwani. Ninyi watu mna tatizo gani na watu kuamua jinsi ya kuishi katika jamii??!!! Kama hampendi si mseme tu, eti tuna hitilafu!!!
Unapoweka sheria kuwa usivae hivi, vaa vile au usifanye mapenzi ya aina fulani, fanya ya aina fulani ndio kuzuia watu kuamua jinsi ya kuishi katika jamii, mtu mzima anatakiwa awe huru kuishi anavyotaka, ili mradi tu asiingilie uhuru wa mtu mwingine, hutakiwi kumtungia mtu sheria ya namna ya kuvaa, au kufanya mapenzi, una swali hapo?
 
Hicho ndicho tunachokipinga, kulazimisha maoni yako yafuatwe hadi unaweka kuwa ni sheria. Utampangiaje mtu mzima namna ya kuvaa!??
Kwa nini usimpangie kama ni jambo linalokubalika na wengi??!! Hivi haujui kuna watu hawataki kuwe na serikali, sasa kwa kufuata uhuru wa kila mtu kuishi anavyotaka unaonaje serikali nazo zisiwepo kabisa. Kwa sababu ukiuliza suala la kumpangia mtu namna ya kuvaa, mwingine atauliza kwa nini umpangie mtu kulipa kodi!!! Kwa nini umpangie sehemu ya kujenga na namna ya kujenga? Kwa nini umpangie sehemu ya kuweka biashara yake? Kwa nini umpangie utaratibu wa elimu? Na mengineyo siwezi kumaliza hapa...
 
Naona ukisikia rocket launcher unaogopa sana, ila kwa bahati mbaya wewe ndiye umeidandia. Wewe kule juu si umechangia kwa kuwananga waafrika, halafu baada ya kuona watu wanahoji eti na wewe unajidai umeliona hilo. We kubali tu umekumbuka shuka asubuhi. Tatizo lako unadhani huwezi kukosea.

Wapi nimewananga Waafrika? Kivipi?

Kuhoji source za habari sijaanza leo, utasemaje najidai nimeliona hilo?

Post ya kwanza, ile niliyoitoa kabla ya kuhoji uhakiki wa habari hii, ilihusu habari ilivyopokelewa hapa JF, which is a fact regardless of the veracity of the news.

Baada ya kusema watu wanakuwa sidetracked kuacha kuangalia mambo muhimu kwa habari za ushoga, nikazama zaidi kuanza kuangalia kama hata hizo habari zenyewe ni za kweli au zimepandikizwa tu, katika jibu langu kwa Mjuni Lwambo.

Ningesema "Mugabe mpuuzi sanan kwa kutoa kauli hii" ungeweza kusema kwamba nimeikubali kauli kwamba imetolewa na Mugabe, which is far from the case.

Nimeobserve tu kwamba waafrika wengine wanapenda sarakasi zaidi ya maendeleo. Kitu ambacho wewe kwa kichwapanzi chako huwezi kutofautisha kati ya waafrika wengi na waafrika.

Kuhusu mimi kutokukosea hiyo ni inferiority complex yako tu.
 
Unapoweka sheria kuwa usivae hivi, vaa vile au usifanye mapenzi ya aina fulani, fanya ya aina fulani ndio kuzuia watu kuamua jinsi ya kuishi katika jamii, mtu mzima anatakiwa awe huru kuishi anavyotaka, ili mradi tu asiingilie uhuru wa mtu mwingine, hutakiwi kumtungia mtu sheria ya namna ya kuvaa, au kufanya mapenzi, una swali hapo?
Uhuru wa mtu mwingine unaanzia na kuishia wapi? Hauoni kuwa kunionesha mimi uke wako au uume wako ni kuingilia uhuru wangu wa kuona?? Unaongea kama vile uhuru wa mtu ni jambo lenye tafsiri moja inayokubalika na kila mtu!! Tafakari kijana, kuna mambo yanatokea na kupangwa kulingana na maoni ya jamii husika, wewe kama unaona kutembea uchi ni sawa na hauingilii uhuru, kuna wengine wanaona si sawa na pia wanaona ni kuingilia uhuru wa watu wengine
 
Hapo ndipo mnapochanganya, unasema najadili bila kujali mambo ya kiroho, na mimi nitakuuliza, kwa nini na wewe unajadili bila kujali mambo yasiyo ya kiroho?, kwani siku hizi ni lazima kufuata mambo ya kiroho!??, wasiyoamini katika hayo mambo yako ya kiroho hawana haki kwenye nchi hii!??

Na hata hayo mambo ya kiroho, yanafundisha dhambi ni ushoga tu!??, mbona hampigi marufuku wazinzi?, au uzinzi umehalalishwa kiroho?, wakristo wao ni mke mmoja tu, mbona husemi wake wengi nao wapigwe marufuku kama tunaishi kwa kufuata mambo ya kiroho?
Tatizo unajadili haya mambo bila kujali kuwa kuna mambo ya kiroho. Of coz ukiondoa mambo ya kiroho na maadili ushoga, uzinzi, kutembea uchi (nina maana bila ya nguo), sio tatizo kabisa. Ila kumbuka hata kama wewe huamini mambo ya kiroho na kimaadili, jamii inayoamini mambo hayo inayapa uzito mkubwa. katika jamii hizi, ni kawaida kuamini kuwa inawezekana nchi nzima ikageuzwa juu chini kwa kuwa tu kuna watu wana tabia za kishoga. Kwa maana hiyo kwa binadamu yeyote mwenye akili hawezi kuangalia tu wakati anaona kuna watu wanataka kuangamiza jamii yake. Ni sawa na wewe uone mtu anawasha kibatari pembeni ya nyumba ya nyasi, ni wazi huwezi kukaa kimya!!!Kwa hiyo usikurupuke ukidhani kuwa kila mtu anaangalia ushoga kwa namna unavyoona wewe, vinginevyo wewe usiyeelewa jamii hizi ndio utakuwa kiroja.

Kumbuka werevu mwingi huondoa maarifa.
 
Huyo Koba anaongea tu! Sijui ardhi Yeye anaifikiriaje?

Nkwingwa...

Koba ni mtetezi namba moja wa Ushoga hapa JF..Ni mtetezi wa haki za mashoga tangu enzi na enzi na hana matatizo na ndoa za jinsia moja so si ajabu akamponda Bob Mugabe kwa nguvu zake zote...
 
Last edited by a moderator:
Kwa nini usimpangie kama ni jambo linalokubalika na wengi??!! Hivi haujui kuna watu hawataki kuwe na serikali, sasa kwa kufuata uhuru wa kila mtu kuishi anavyotaka unaonaje serikali nazo zisiwepo kabisa. Kwa sababu ukiuliza suala la kumpangia mtu namna ya kuvaa, mwingine atauliza kwa nini umpangie mtu kulipa kodi!!! Kwa nini umpangie sehemu ya kujenga na namna ya kujenga? Kwa nini umpangie sehemu ya kuweka biashara yake? Kwa nini umpangie utaratibu wa elimu? Na mengineyo siwezi kumaliza hapa...
Naona una shida katika kutofautisha mambo binafsi na yale yasiyo binafsi, swala la mapenzi au kuvaa ni jambo binafsi, kuwa na serikali au kupangiwa sehemu ya kufanyia biashara sio jambo binafsi.
 
Mkuu wangu Mjuni hiyo kauli ya Mugabe mpinga ushoga kutaka kuonesha anavyopinga ushoga kwa kumtaka Obama awe gay partner wake imenipa maswali mpaka nikajiuliza kwamba ingawa Mugabe ni controversial, lakini hii kauli kaisema yeye au ni watu tu wamemlisha maneno?

I don't see any major news website carrying this story. I would like to see some links from reputable sources before giving this news proper credibility.

Inawezekana ni yale yale ya watu kutengeneza habari halafu forums zinawaka moto.

Or maybe that's just the natural skeptic in me.

Wapi nimewananga Waafrika? Kivipi?

Kuhoji source za habari sijaanza leo, utasemaje najidai nimeliona hilo?

Post ya kwanza, ile niliyoitoa kabla ya kuhoji uhakiki wa habari hii, ilihusu habari ilivyopokelewa hapa JF, which is a fact regardless of the veracity of the news.

Baada ya kusema watu wanakuwa sidetracked kuacha kuangalia mambo muhimu kwa habari za ushoga, nikazama zaidi kuanza kuangalia kama hata hizo habari zenyewe ni za kweli au zimepandikizwa tu, katika jibu langu kwa Mjuni Lwambo.

Ningesema "Mugabe mpuuzi sanan kwa kutoa kauli hii" ungeweza kusema kwamba nimeikubali kauli kwamba imetolewa na Mugabe, which is far from the case.

Nimeobserve tu kwamba waafrika wengine wanapenda sarakasi zaidi ya maendeleo. Kitu ambacho wewe kwa kichwapanzi chako huwezi kutofautisha kati ya waafrika wengi na waafrika.

Kuhusu mimi kutokukosea hiyo ni inferiority complex yako tu.
Kwani kusema unawananga waafrika maana yake ni waafrika wote??!! Kiranga wewe kiswahili unakifahamu vizuri iweje ushindwe kuelewa maana ya sentesi rahisi kama hiyo??!! Kuwananga unawananga sana tu, ukichanganya na maneno ya hao wazungu wako wa kirusi ambao umewakariri vizuri ndio balaa.

Tukija kwenye suala la kuimeza habari, kama ungeuliza kwanza kuhusu usahihi wa hii habari kabla ya kutoa dukuduku lako ningeweza kusema hukuimeza. Wewe umekimbilia kutoa dukuduku lako hapa halafu baadaye baada ya kumsoma Mujuni ndio unakumbuka kuuliza halafu unataka tuamini kuwa hukuimeza!!!!??? Kama nilivyosema mwanzo tatizo lako unadhani una akili sana ndiyo maana una vitusi vyako vya reja reja (eti kichwa panzi). Pili unadhani huwezi kukosea. Kwa taarifa yako tu hata uwe na akili vipi, kuna siku lazima utakosea tu, ndivyo binadamu walivyo.

Acha uhuni wa kutukana matusi yako ya reja reja kumbuka akili nyingi huondoa maarifa.
 
Naona una shida katika kutofautisha mambo binafsi na yale yasiyo binafsi, swala la mapenzi au kuvaa ni jambo binafsi, kuwa na serikali au kupangiwa sehemu ya kufanyia biashara sio jambo binafsi.
Binafsi kwa tafsiri ya nani? Wewe ndiye unatafsiri ya mambo binafsi? Nimekwambia tatizo lako unadhani tafsiri yako wewe ya jambo fulani ndiyo inatakiwa kuwa tafsiri ya dunia. Wewe unaweza kuona mapenzi ni jambo binafsi, sawa hukatazwi, sasa nani kakwambia kuwa kila mtu anaona hivyo?
 
Hapo ndipo mnapochanganya, unasema najadili bila kujali mambo ya kiroho, na mimi nitakuuliza, kwa nini na wewe unajadili bila kujali mambo yasiyo ya kiroho?, kwani siku hizi ni lazima kufuata mambo ya kiroho!??, wasiyoamini katika hayo mambo yako ya kiroho hawana haki kwenye nchi hii!??

Na hata hayo mambo ya kiroho, yanafundisha dhambi ni ushoga tu!??, mbona hampigi marufuku wazinzi?, au uzinzi umehalalishwa kiroho?, wakristo wao ni mke mmoja tu, mbona husemi wake wengi nao wapigwe marufuku kama tunaishi kwa kufuata mambo ya kiroho?
Kwa hiyo unataka kusema kwa kuwa kuna mtu aliiba juzi hakukamatwa na wewe uliyeiba leo uachiwe?? Wewe sasa ndio unatakiwa useme jamani eeh, tusiishie kwenye ushoga tu, tupige marufuku na uzinzi pamoja na ubazazi wote.

Mkuu anzisha tu kupinga uone kama hujaungwa mkono.
 
Kwani kusema unawananga waafrika maana yake ni waafrika wote??!! Kiranga wewe kiswahili unakifahamu vizuri iweje ushindwe kuelewa maana ya sentesi rahisi kama hiyo??!! Kuwananga unawananga sana tu, ukichanganya na maneno ya hao wazungu wako wa kirusi ambao umewakariri vizuri ndio balaa.

Tukija kwenye suala la kuimeza habari, kama ungeuliza kwanza kuhusu usahihi wa hii habari kabla ya kutoa dukuduku lako ningeweza kusema hukuimeza. Wewe umekimbilia kutoa dukuduku lako hapa halafu baadaye baada ya kumsoma Mujuni ndio unakumbuka kuuliza halafu unataka tuamini kuwa hukuimeza!!!!??? Kama nilivyosema mwanzo tatizo lako unadhani una akili sana ndiyo maana una vitusi vyako vya reja reja (eti kichwa panzi). Pili unadhani huwezi kukosea. Kwa taarifa yako tu hata uwe na akili vipi, kuna siku lazima utakosea tu, ndivyo binadamu walivyo.

Acha uhuni wa kutukana matusi yako ya reja reja kumbuka akili nyingi huondoa maarifa.

Awali ya yote, nilitoa dukuduku langu kuhusu habari au kuhusu waafrika wengi walivyoipokea habari?

Ni kweli au si kweli (regardless kama habari imetolewa na Mugabe au wahuni tu) kwamba Waafrika wamekimbilia kusifia ushujaa wa Mugabe wakati huyu mpuuzi kaua Wandebele 20,000 kama anachinja kuku?

Ni kweli au si kweli kwamba huyu mpuuzi kafanya inflation ya Zimbabwe iipite inflation tuliyokuwa tunajifunzia shule kama kichekesho kikubwa, ile ya Ujerumani baada ya vita vikuu? Kuna mkuu kaweka picha ya mayai matatu hapa yanauzwa kwa Zim dola bilioni mia huko.

Habari hizi ndizo nilizozileta awali ya yote, kwamba huyu mpuuzi mtu mwenye kufikiri hawezi kumsifia kwa sababu ana ma scandal makubwa sana.

Sasa utataka kubisha kwamba hizo objections zangu za Waafrika kumshangilia Mugabe, regardless kama hizi habari za kumuoa Obama ni za kweli au si za kweli, hazikuwa na msingi?

Ningeweza ku comment kwamba Mugabe ni mshenzi kwa kusema anataka kumuoa Obama tangu kwenye post ya kwanza, lakini kwa sababu nilikuwa sijaiona hiyo kauli katika any major news website, na aliyetuletea habari hajatoa source, sikutaka kufanya hivyo kabla ya uchunguzi kidogo.

Ila niliyoamua kusema yatabaki kuwa ni ya msingi, regardless ya hizi habari za kumuoa Obama ni za kweli au si za kweli.

Sasa wewe unayekosoa sehemu ambapo hakuna cha kukosoa na mimi ninayekuelewesha, nani anafikiri ana akili sana?
 
Uhuru wa mtu mwingine unaanzia na kuishia wapi? Hauoni kuwa kunionesha mimi uke wako au uume wako ni kuingilia uhuru wangu wa kuona?? Unaongea kama vile uhuru wa mtu ni jambo lenye tafsiri moja inayokubalika na kila mtu!! Tafakari kijana, kuna mambo yanatokea na kupangwa kulingana na maoni ya jamii husika, wewe kama unaona kutembea uchi ni sawa na hauingilii uhuru, kuna wengine wanaona si sawa na pia wanaona ni kuingilia uhuru wa watu wengine
Kama nilivyosema hapo juu, shida yako ni kwenye kutofautisha mambo, wewe unapomuangalia mtu aliyevaa nguo fupi, huwezi kusema ameingilia uhuru wako wa kuona kwa sababu hajakulazimisha, umehiari mwenyewe kumuangalia.

Waarabu wameenda na falsafa ya mavazi hadi inataka kuwafikisha pabaya, wanajifanya wao wana ashki sana, wanasema hata nywele za mwanamke ni utupu, hivyo azifunike, mwishowe wakabaini macho ya mwanamke nacho ni kishawishi, nayo wakamtaka aweke wavu, mwisho wamegundua hata akijifunika mwili mzima hadi macho, bado ni kishawishi. Saudia wameamua kujenga mji ambao wanawake watakaa huko peke yao ili wasionekane kabisa. Ni ujinga tu, vishawishi vinaanzia kwrnye fikra zako mwenyewe.
 
Mosi, tunarudi pale pale kuwa unaamini kile unachojua wewe ndio ukweli. Eti huwezi kusema!!! Kwa mujibu wa nani?? Wewe?!!. Pili, naomba unithibitishie hiyo kauli kwenye nyekundu hapo au na wewe ndio kama huyu jamaa na Mugabe wake?
 
Awali ya yote, nilitoa dukuduku langu kuhusu habari au kuhusu waafrika wengi walivyoipokea habari?

Ni kweli au si kweli (regardless kama habari imetolewa na Mugabe au wahuni tu) kwamba Waafrika wamekimbilia kusifia ushujaa wa Mugabe wakati huyu mpuuzi kaua Wandebele 20,000 kama anachinja kuku?

Ni kweli au si kweli kwamba huyu mpuuzi kafanya inflation ya Zimbabwe iipite inflation tuliyokuwa tunajifunzia shule kama kichekesho kikubwa, ile ya Ujerumani baada ya vita vikuu? Kuna mkuu kaweka picha ya mayai matatu hapa yanauzwa kwa Zim dola bilioni mia huko.

Habari hizi ndizo nilizozileta awali ya yote, kwamba huyu mpuuzi mtu mwenye kufikiri hawezi kumsifia kwa sababu ana ma scandal makubwa sana.

Sasa utataka kubisha kwamba hizo objections zangu za Waafrika kumshangilia Mugabe, regardless kama hizi habari za kumuoa Obama ni za kweli au si za kweli, hazikuwa na msingi?

Ningeweza ku comment kwamba Mugabe ni mshenzi kwa kusema anataka kumuoa Obama tangu kwenye post ya kwanza, lakini kwa sababu nilikuwa sijaiona hiyo kauli katika any major news website, na aliyetuletea habari hajatoa source, sikutaka kufanya hivyo kabla ya uchunguzi kidogo.

Ila niliyoamua kusema yatabaki kuwa ni ya msingi, regardless ya hizi habari za kumuoa Obama ni za kweli au si za kweli.

Sasa wewe unayekosoa sehemu ambapo hakuna cha kukosoa na mimi ninayekuelewesha, nani anafikiri ana akili sana?
Hayawezi kuwa ya msingi kwa kuwa hawa jamaa hawajamshangilia Mugabe katika hayo unayotaka kusema wewe. Wamemshangilia kwa sababu ya hiyo habari ya mleta mada. Kumbuka hapa hatujadili historia ya Mugabe, tunajadili hiyo habari.
 
Hayawezi kuwa ya msingi kwa kuwa hawa jamaa hawajamshangilia Mugabe katika hayo unayotaka kusema wewe. Wamemshangilia kwa hiyo kauli, hapa hatujadili historia ya Mugabe, tunajadili hiyo habari.

Ni ya msingi precisely kwa sababu wamemshangilia Mugabe yule yule. Huyu si mtu mwingine.

Huwezi kumtenganisha Mugabe na matendo aliyotenda.

Ni ya msingi kwa sababu yanaonesha kwamba Afrika unaweza kuua raia wako 20,000 kama kuku, ukashusha hela yenu thamani kiasi mayai matatu yanunuliwe kwa dola zenu bilioni mia moja, halafu ukiona huna cha kusema kwa sababu ushavurunda kila sehemu, mshambulie Obama na habari zake za mashoga na watu watakushangilia tu.

Hapo ndipo utakapoona ujinga wa baadhi yetu na kwa nini objections zangu ni za msingi.

Ila kama alivyosema Nyani Ngabu , baadhi yetu tuna standards ziko so low kiasi kwamba Mugabe yule yule aliyeua watu 20,000 katika "Ndebele Massacre" na kuifanya hela ya Zimbabwe iwe a laughingstock of the world, akija na sarakasi za kukandia ushoga tu watu wanampigia makofi kwa kumuita "kidume cha Afrika" na upuuzi mwingine kibao kama huo.
 
Binafsi kwa tafsiri ya nani? Wewe ndiye unatafsiri ya mambo binafsi? Nimekwambia tatizo lako unadhani tafsiri yako wewe ya jambo fulani ndiyo inatakiwa kuwa tafsiri ya dunia. Wewe unaweza kuona mapenzi ni jambo binafsi, sawa hukatazwi, sasa nani kakwambia kuwa kila mtu anaona hivyo?
Kabla ya kwenda mbali kwenye kuuliza ni binafsi kwa tafsiri ya nani, naomba nikuulize, wewe unaona kuwa mapenzi ni suala la public?
Tunajuaje kwamba hiki ni sahihi na hiki sio sahihi?, au hiki ni public na hiki ni private?, tafsiri ni ya nani?, naomba nitumie kiingereza.

There are universal fundamental principles to define things which are obtained due to intuitive judgements, ndio maana tunasema, kila mtu anao uhuru wa kuwa na maoni na mtazamo wake lakini hakuna mtu mwenye haki ya kuwa na ukweli wake peke yake.
 
Kama nilivyosema hapo juu, shida yako ni kwenye kutofautisha mambo, wewe unapomuangalia mtu aliyevaa nguo fupi, huwezi kusema ameingilia uhuru wako wa kuona kwa sababu hajakulazimisha, umehiari mwenyewe kumuangalia.

Waarabu wameenda na falsafa ya mavazi hadi inataka kuwafikisha pabaya, wanajifanya wao wana ashki sana, wanasema hata nywele za mwanamke ni utupu, hivyo azifunike, mwishowe wakabaini macho ya mwanamke nacho ni kishawishi, nayo wakamtaka aweke wavu, mwisho wamegundua hata akijifunika mwili mzima hadi macho, bado ni kishawishi. Saudia wameamua kujenga mji ambao wanawake watakaa huko peke yao ili wasionekane kabisa. Ni ujinga tu, vishawishi vinaanzia kwrnye fikra zako mwenyewe.

Hili suala la ushoga limepamba moto miaka ya karibuni. Mugabe yupo madarakani kwa zaidi ya miaka 30. Kama yeye ni kiongozi mahiri basi angetatua matatizo ya wananchi wake kabla suala ushoga alijaanza.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom