aaaaah subiri kwanza wewe ushoga unauonaje....
Mimi si suala la ushoga tu, mambo yote ambayo yanahusiana na watu wazima wawili ni juu yao. Falsafa yangu ni, mambo ya Ngoswe, muachie Ngoswe mwenyewe.
As long as mashoga hawanilazimishi mimi niwe shoga, sitaki kuwalazimisha wawe straight.
Hao wazungu/ wamagharibi wanaojidai wana mind sana haki za binadamu kuna namna ya kuwabana, lakini sijasikia bado kiongozi wa kiafrika akiwabana inavyotakiwa.
kwa mfano, sijawahi kusikia kiongozi wa Kiafrika akisema sisi kwetu Afrika mwanamme anaweza kuoa wake wawili au watatu au wanne (waislam) au hata zaidi katika mila zetu. Kwa nini nyie mnatukataza kuoa wake wawili na zaidi tukiwa kwenu?
Angalia ukewenza ulivyo kosa katika nchi nyingi za magharibi
Bigamy - Wikipedia, the free encyclopedia
Sasa kama mtu anataka kukataa cultural imperialism, kupewa utamaduni wa kuufuata, hili swali kama pale kwenye interview ya Kikwete na Amanpour ndipo lilikuwa sehemu yake.
Ningekuwa mimi Kikwete ningemuuliza Amanpour, haya mambo ni mambo ya utamaduni, mbona huku kwetu Afrika mwanamme anaweza kuoa wake wengi kisheria (rais wa South Africa ana wake zaidi ya mmoja, Rais Mwinyi alikuwa na wake wenza, mfalme Mswati ndiyo usiseme tena) halafu huko kwenu Marekani na Ulaya kuwa na wake wengi ni kosa la jinai na sisi hatuwalazimishi msilifanye kosa?
Kama mnataka kuhalalisha ushoga kwetu, basi na kwenu halalisheni ukewenza tujue mnachotaka si kututupia tamaduni zenu tu, bali mnataka kwenda na a progressive world (progressive in the sense kwamba mtu mzima yeyote asipangiwe cha kufanya )
Kwa hiyo kuna namna ya kuhoji haya mambo in a statesmanlike manner, sio Kikwete anaulizwa wewe unaonaje anajiumauma kama kigoli aliyejaa haiba.
Mimi ningekuwa na uamuzi, mtu mwenyewe awe na uamuzi wake. Akitaka kuwa shoga kivyake. Mwanamme akitaka kuoa wake kumi na nane kivyake. mwanamke akitaka kuolewa na wanaume kumi na nane kivyake. Mradi mtu mzima asipangiwe maisha.
Na huko Marekani wanakojifanya maliberali waruhusu wanaume kuoa wake wengi. na sie tunaotaka kuanzisha vyama vya kikomunisti Marekani tupewe uhuru wa kufanya hivyo.
Sio Mmarekani anajifanya mpenda uhuru wakati mtu hawezi kuoa wake wawili, au kuwa mwanachama wa chama cha Kikomunisti.
Hawa viongozi wa Afrika utawasikia sana kuongelea mambo kama haya ya ushoga kwa sababu hawana kingine cha kuongea.
Ukiwapeleka kwenye uchumi, elimu, maendeleo wengi wao ni failures.