Habari, kuna kitu kimoja rafiki labda hukifahamu kuhusu Iringa, kaka Wahehe hawana hela. Mkoa wa Iringa una Wahehe tu na hawa wahehe wanategemea kilimo cha Mahindi tu. Mafinga Wenye hela ni Wakinga kwenye miti na Wabena, wahehe pale ni kama wageni. Chai Mufindi Wahehe ni Vibarua tu, kumbuka Mufindi ni mpaka wa Njombe na Iringa watu wa kule wengi wametokea Njombe, kwahiyo wanajenga Makambako Njombe. Iringa Mjini uchumi upo kwa Wahindi waarabu kina ASASI, Huwel na wenzao. Mtera, Ruaha Mbuyuni, Ilula kuna makabila ya kuja kama wagogo, Zungwa na Mengine. Iringa wazawa wana taabu sana, nina ndugu uko kaka. Njombe wanalingia mseto wa biashara kutoka Bonde la Usangu Mbarali, Mlimba (Treni Tazara) na Miti ya Mufindi, maana kiwanda cha Karatasi Mufindi, Magari ya Kubeba karatasi yanatoka Njombe Makambako(Jah People), Kuni za kiwandani zinatoka Njombe TANWAT.