Mtego wa Umaskini na Dhana ya Kujitegemea

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,714
Reaction score
7,813
Leo ngoja niwape madini ya kwa nini familia nyingi zinabaki masikini, tunajikwamua lakini bado tunarudi pale pale, unakuta Baba kapambana kapata vimali, lakini badae miaka mbeleni unakuta bado familia ina struggle pale pale kwenye umasikini.

Dhana kubwa hipo katika hoja ya "Ukajitegeme" au " Ukatafute vya kwako" Huu ni mtego wa umaskini ambao umeimarishwa zaidi na unazidi kuwa na kasi kubwa sana. Mtego huu umezificha nyuma ya elimu ya kujitegemea. Kwamba mtu anapomaliza shule akiwa nyumbani baba yake anamwambia "ondoka nyumbani, toka uende, kajitegemee, kawe na vya kwako." Hekima hii imeonekana kwamba ndio njia nzuri ya kumfanya mtu aweze kufanikiwa atoke mwenyewe. Kitu ambacho ni uongo na ndio sababu ya umaskini wenyewe.

Nisikilize nikwambie. Kujitegemea haimaanishi kwenda peke yako, haimaanishi kuwa mwenyewe, haimaanishi kuanzisha wewe. Kujitegemea ni uwezo wa akili kutambua kwamba wewe ni nani, uko wapi, unapaswa kufanya nini, na unapaswa kutumikia wajibu gani kwa namna gani. Huko ndiko kujitegemea. Kujitegemea sio kutengeneza kitu chako peke yako, kujitegemea sio kufanya wewe kama wewe.

Kujitegemea ni uwezo wa kuchakata mambo katika jamii na kuweza kutafsiri matatizo na kupata solution ya hayo matatizo. Wenzetu wametuficha kwenye maeneo ambayo wanawatangaza matajiri wao kwa majina na kuweka figure: Elon Musk ana utajiri wa dola trilioni moja. Mark Zuckerberg ana utajiri wa dola bilioni 200 na ushee. Jeff Bezos, hivyo. Lakini watakuambia kuhusu hata mataifa yao. Marekani leo hii inao uchumi wa dola trilioni 30 plus.

Lakini angalia matajiri wake walivyo. Katika top 10 ya matajiri duniani 70% plus ya matajiri wote duniani ni wa Marekani. Asilimia karibia zaidi ya 5% ya top 20 ya matajiri duniani... wa Marekani, hebu jiulize swali. Unajua kuna nini hapo? Kuna siri usiyoijua. Siri hii ni kwamba wenzetu matajiri wao wanawafanyia backup. Wakati wanamtanguliza mmoja mbele nyuma yake kuna zaidi ya watu 100 ambao wanachochea moto, wanafanya kazi, wana- bring ideas lakini kuna icon inayotangulia mbele kwa ajili ya kufanya mambo kama hayo.

Nimekuwa nikimfahamu Mzee Gulam Dewji akiwa mfadhili wa Simba. Moja kati ya matajiri wakubwa katika nchi yetu. Lakini makampuni yake ya MeLT leo yako chini ya Mo Dewji, mwanae. Anayetangazwa kuwa tajiri ni Mo. Yeye anaitwa tajiri namba 12 Afrika. Ukirudi kuangalia utajiri wake ni wa familia. Na hakuna yeyote katika familia ambaye ana-complain. Kwa nini? Kwa sababu yeye ndiye alifaa kuwa hapo. Siku chache zilizopita alim-introduce mwanae. Maandalizi ya nani mrithi wa kiti kinachokuja. Kama ambavyo baba yake alimwachia kiti ndivyo ambavyo na yeye anaachia kiti.

Nisikilize nikwambie. Hakuna njia yoyote wala principle yoyote unayoambiwa na watu wote itakufanya kuwa tajiri wa tishio. Isipokuwa utakuwa moja kati ya watu wanao hangaika. Ndio maana ukiangalia watu wengi wenye stress kubwa ni wale wenye mitaji ya kuanzia bilioni tano, kumi, ishirini. Wanapambana kila siku, wanapambana na uchawi, wanapambana na uaminifu, wanapambana na vitu vingi sana. Kwa nini? Kwa sababu mfumo wao hauna watu nyuma ambao wana uchungu na hicho ambacho wanapigania. Hawana watu ambao wanatoka katika base ya kwao. Na wakiwachukua watu wa kwao, wanawachukua kama watu ambao wanawasindikiza. Wale ndugu zao wanapokuja pale wanaona kabisa kwamba hawako katika mfumo.

Kwa hiyo na wenyewe wakifika wanaiba ili waende kwenda kujitegemea kurudia mgumo ule ule. Utaratibu huu umetengenezwa makusudi ili tuendelee kuwa maskini. Mataifa ya wenzetu yanawajali sana matajiri wao. Na familia za wenzetu zinajali sana watu wao. Ni lazima kujua temperament ya mtu na watu walioko nyuma yake. Sio kila mtu anaweza kuwa mfanyabiashara. Na wala sio kila mtu anaweza kuwa muuzaji. Na wala sio kila mtu anaweza kuwa na nguvu za kubeba. Tuna tofautiana. Ikiwa kwenye familia tutakubali kwamba kila kipaji tutakipa heshima yake na kuanza kutumika pamoja kama walivyo Mchwa lazima tutajenga kichuguu cha ajabu. Lakini tatizo kila mmoja anataka aoneakae. Kila mmoja anataka attention. Na hakuna mtu anataka ku-respect career ya mtu mwingine. Hilo ni tatizo tuliyotengeneza.

Hata unawaona mabepari wako katika makundi yao. Wanafanya kazi kwa pamoja, wameshikamana. Usisikie tu bépari ukafikiri kwamba ni individual. Hapana. Donald Trump ameshikamana na watoto wake. Kila tajiri unayemfahamu duniani anatisha ameshikamana na familia yake. Kama sio familia kuna kundi lingine ambalo liko pamoja naye ambalo wameshikilia vitu. Ndivyo maana unaona wanakwenda. Usidanganywe ndugu yangu kusema kwamba wewe unapambana, utatoka. Utakufa na kihoro, utakufa umechoka sana. Unaumia sana. Unahitaji watu, unahitaji umoja, unahitaji kukubali kwamba kuna mahali wewe umepungua, mwingine anaweza kujazia. Hapo ndipo kuna ukombozi wa kweli. Hakuna cha kusema kwamba "nenda ukajitengemee, nenda akajitafutie" huko ni kwenda kusambaza umaskini. Hii mnayosema kwamba "nenda ukajitegemee, nenda kapambane" huko ndio kusambaza umaskini. Daktari mmoja kule, sijui nesi kule, mwalimu kule, umeona? Askari magereza, umeona? Uwezo wa kutatua jambo ni kuchanga pesa za msiba. Lakini kuna kingine kinachowezekana. Zaidi ya kuzikana.

Mkuu umetumia hizi principles kujitengenezea utajiri wa kiasi gani?
 
View attachment 3684915
Waafrika ni selfish, so hayo unayoyaonq wewe hayatekezeki kwa namna yoyote ile
 
Huo ujinga hatuna , yaani uache nyumba ya mzee wako ukaanze kulipa kodi eti unaenda kuanza kwako ni ujinga ..Mbaya kuna watu wana fikra hizo .
 
Mkuu umetumia hizi principles kujitengenezea utajiri wa kiasi gani?
Mimi ndio naanza, ila point hiyo ina maana.... utajiri wa kuanzia chini mgumu tofauti na wa kuuendeleza
 
Waafrika ni selfish, so hayo unayoyaonq wewe hayatekezeki kwa namna yoyote ile
Ndio maana Waafrika kuwa matajiri ni uongo, matajiri wengi wakifa ndio utajiri wao umeishia hapo, hawana successor... mfano mengi, successor wao ni nani
 
Back
Top Bottom