Umaskini wa Tanzania Kimkoa

Umaskini wa Tanzania Kimkoa

Daah, lakini Umesahau kuwa Dodoma ina Muingiliano mkubwa wa watu daily,
Tafiti imebase kwenye mzunguko wa pesa kwa mtu mmoja mmoja sio chakula, kilimo wala nini.

Kwa mzunguko wa pesa Iringa bado sana kwa dodoma.
Mkoa wa Dodoma vs Iringa au Jiji la Dodoma vs Iringa Municipal? Tuliweke sawa hilo kwanza
 
Wanapitia kaya zilizo duni katika kata, na kufanya tafiti kwa kuuliza kipato chao, na matumizi waliyotumia siku nzima. Taarifa hizi huwa zinachukuliwa kila mwanzo wa mwezi kwa wiki mbili mfululizo katika kipindi cha mwaka mmoja.
Kwa kigezo hicho,lazima Dar iongoze kwa mbali. Sijui kama wanafika kule Pemba Mnazi,kijijini kabisa kwa hapa Dar
 
Watu wa pwan wao Ni ngoma tu uchumi wataujulia wap?
Tanga ni pwani,Dar es Salaam ni pwani,Mtwara ni Pwani hata Morogoro inaangukia eneo la pwani(ya mbali), lakini hazina huo umaskini. Determinant siyo upwani wala ubara!
 
Sawa ni vigezo vyako umeainisha huenda kwa iringa na Dom, sasa huenda wamezidiwa na wagogo na warangi usilazimishe kamanda, unajua kondoa pekeyake ianapato kubwa sana mpwampwa,ina pato kubwa sana, watu wa takwimu wanadurusu kila kona wewe umejaribu lakini takwimu inainyesha wamezidiwa
Pato kubwa lipi au kutoka wapi? Ukiacha Dom city wilaya zipi zina mapato huko kushinda Iringa
 
Mbona pana umbali tu? Magarini ipo mbele ya KIZIRAMUYAGA,umbali kutoka Magarini Hadi muganza Ni sh 2000 kwa hiace
Ni ajabu Soko likawe chato wakati mwalo upo muleba
Ulizia mkuu magarini palishafungwa kitambo.

Na sasa samaki wanauziwa chato.


Na naskia Meli kubwa inayobeba utakuwa inapitia bandari ya nyamilembe kabla ya kufika kemondo na Bukoba ports
 
Kumbe mkoa mpya wa songwe uko vizuri huko ndo kwa kukimbilia fursa sasa acheni kubishana.
Tunatumia vizuri fursa za kuwepo mpakani,kinachoibeba songwe ni mpaka wa Tunduma but hata hivyo ndani ya km 45 kuna miji mikubwa 3 is like conglomation ya miji kuanzia mlowo,Vwawa na Tunduma ni kama imeungana so biashara inanoga na mzunguko wa pesa ni mzuri
 
Mkuu umechangia kwa kuweka fact tupu. Pia mimi huwa napata tabu kubwa nikiona jiji la Mwanza lilivyo busy kwamba linazidiwa na Dodoma kwa makusanyo. Anyway,wanaokusanya data ndiyo wajuao.
Mko busy lakini mnauza nyanya mboga mboga etc mtaweza vipi kushindana na Dom yenye UDOM,Bunge na Serikali?
Hapo Dom kuna pesa sana hasa biashara za huduma na kumbuka bado haijawa full ko usishangae saizi Dom inashindana na Dar tuu nyie wengine akina mwanza shindana na Arusha,Mbeya na Tanga.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom