KWANINI NYANI HAWAOGOPI JINSIA YA KIKE KAMA ILIVYO KWA JINSIA YA KIUME?
Kwakweli nimetafuta points nijibu swali hili nikagundua kuwa sitajibu sawasawa!
Isipokuwa tujue tu kuwa uoga (fearness) hutokea katika sehemu ya Ubongo iitwayo AMYGDALA na tafiti zinaonyesha ukiondoa sehemu hiyo...mnyama atashindwa hata kutambua kuwa umefika wakati anapaswa kuogopa! (nimenukuu pahala)
Lakini huko Kenya...Nyani wamegeuka tishio kwa kuwashambulia wanawake ambao mara nyingi ndio hufanya shughuli za shamba! Na hata mama hao wakivaa nguo za waume zao bado nyani hawachoki kuwasumbua! Hii ni ajabu iliyozua mjadala na vicheko katika bunge la Kenya!
Nyani wagomvi huko Kenya pitia hapa:
BBC NEWS | Africa | Monkey misery for Kenyan women villagers
Naomba nijiridhishe kwanza kusoma makala mbalimbali halafu nitakujibu kwa fasaha.