Uliza ujibiwe Kisayansi kuhusu viumbe pori

Uliza ujibiwe Kisayansi kuhusu viumbe pori

munirah

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2015
Posts
551
Reaction score
224
Je ungependa kujua jambo gani kuhusu viumbe pori waliopo Tanzania na popote duniani ikiwezekana! Lengo ni kupata elimu ya maswala tata yanayohusu wanyama mwitu tukijumuisha maisha yao, tabia zao na mambo mengine mengi!

Karibu tushirikiane kujibu pale ambapo tuna elimu japo kidogo.
 
Samahani kama swali langu litakuwa na ukakasi.
Mimi napenda kufahamu, ikiwa mbwa(jike) yuko kwenye joto(heat) na kupandwa na madume zaidi ya mmoja,
je, jike huyo ataweza kushika mimba ya madume kadhaa waliompanda?
 
Ningependa kujua unazungumzia jike wa mbwa gani? je ni mbwa mwitu (L. pictus) au?

Lakini kimantiki yai la jike la mnyama yeyote hurutubishwa mara moja tu na mbegu za dume husika na baada ya yai kurutubishwa kuna mechanism hutokea kuzuia multisperms au yai kurutubishwa zaid ya mara moja!

Zipo sababu nyingi za majike ya viumbe vingi duniani kukutana kimwili na dume zaidi ya mmoja katika kipindi cha kuzaana au mating season hasa kwa wanyama kama jamii ya nyani!

Sababu mojawapo ni mama kuhakikisha kuwa anapata ulinzi kwa madume yale pindi atakapozaa watoto maana kila baba atahisi anahusika moja kwa moja katika malezi na ulinzi wa watoto hao huku ukweli utabaki kuwa wa kwanza kuingia ndio ana higher probability of mating success.
 
ugonjwa gani unashambuliwa majike porini?

Labda sikueleweka kuwa tunazungumza mada zinazohusu wanyama wote wa mwituni kama fisi mbwa mwitu swala simba nk

Swali lako sijajua linaegemea wapi maana magonjwa ya wanyama ni mengi sana
 
yale madenge makubwa yaliyokuwa na uwezo
wa kunyanyua mbuzi au watoto wadogo
siku hizi yako wapi?
 
Labda sikueleweka kuwa tunazungumza mada zinazohusu wanyama wote wa mwituni kama fisi mbwa mwitu swala simba nk

Swali lako sijajua linaegemea wapi maana magonjwa ya wanyama ni mengi sana

magonjwa ya wanyama pori jike..
 
kinyonga anataga au anazaa??
Inategemea na aina husika ya kinyonga ambapo tunawatenga katika makundi makuu mawili yaani kitaalamu tutawaita OVIPAROUS ambao wanataga mayai siku 3-6 baada ya jike kupandwa na OVOVIVIPAROUS ambao kimtazamo anaonekana anazaa lakini kiuhalisia anataga mayai na kuyahifadhi katika ngozi laini baada ya kurutubishwa na baada ya muda mayai yale yatapasuka pamoja na ngozi ile laini halafu watoto watatoka (hatchling) kwa hali hii utaona wanazaa lakini siyo.
 
yale madenge makubwa yaliyokuwa na uwezo
wa kunyanyua mbuzi au watoto wadogo
siku hizi yako wapi?

Kuna hadithi mbali mbali zimekuwa zikitoka kuelezea wanyama wa mwituni na tabia zao wakiwamo hao ndege wakubwa! Yapo makosa makubwa na zipo faida as well!

TUFAHAMU KUWA
Kwa Afrika yetu ndege mkubwa anayepaa ni ndege aitwaye Kori bustard (Ardeotis kori) ambae hawezi kubeba mbuzi na kidunia ndege mkubwa kabisa ni Mbuni ( Struthio camelus)

Nimeshuhudia ndege kama Martial Eagle akibeba wanyama wadogo kama sungura na swala wadogo ambao ni jamii ya mbuzi
 
Mbuni hapai kamwe! na hakuna ndege anayepaa ataweza kumbeba mbuzi mkubwa labda tu abebe kitoto cha mbuzi au mnyama jamii ya mbuzi kwa kuzingatia uzito wa mzigo na mbebaji husika!

Lakini pia kama walikuwepo ndege hao zamani, kutoweka kwao ni matokeo ya athari za kibinadamu katika mazingira, kuwindwa, magonjwa nk
 
magonjwa ya wanyama pori jike..

Napenda sana nikujibu ipasavyo hasa pale utakapokuwa specific maana majike wapo wengi porini na wanashambuliwa na magonjwa tofauti tofauti!

Sidhani kama nitaweza kukuelezea kiujumla. Tafadhali sana
 
Napenda sana nikujibu ipasavyo hasa pale utakapokuwa specific maana majike wapo wengi porini na wanashambuliwa na magonjwa tofauti tofauti!

Sidhani kama nitaweza kukuelezea kiujumla. Tafadhali sana
basi tuanze na simba jike
 
basi tuanze na simba jike

Katika tafiti zilizofanyika maeneo mengi duniani ikiwemo Tz magonjwa kama trichinosis,
filariasis, sarcoptic mange, pentastomiasis,
echinococcosis, taeniasis, hepatozoonosis,
anthrax, babesiosis na rickets yamebainika kuwa na athari kubwa kwa Simba hivyo kutishia uwepo wao wa baadae na hata mengine huweza kuhamia kwa binadamu! Nikimaanisha magonjwa 6 kati ya nilotaja hapo juu huweza kumpata binadamu kwa njia ya maambukizi
 
Unaposema "viumbe pori" nadhani unamaanisha wanyama na mimea.swali langu ni hili 'kwanini unapovuta bangi iliyopandwa sehemu kame inakuwa ni kali kuliko iliyopandwa kwe udongo we kila mahitaji ya mmea"?
 
Kwa heshima kuu mkuu mara utakapomaliza kujibu swali la miss chagga nikuombe utuondolee utata kuhusu jinsia ya mnyama fisi,je ni kweli kuwa wote ni multisexes?pili ni je kwa hali ya kawaida mnyama kama chui anaweza kufugika? Hayo kwanza.
 
Last edited by a moderator:
Katika tafiti zilizofanyika maeneo mengi duniani ikiwemo Tz magonjwa kama trichinosis,
filariasis, sarcoptic mange, pentastomiasis,
echinococcosis, taeniasis, hepatozoonosis,
anthrax, babesiosis na rickets yamebainika kuwa na athari kubwa kwa Simba hivyo kutishia uwepo wao wa baadae na hata mengine huweza kuhamia kwa binadamu! Nikimaanisha magonjwa 6 kati ya nilotaja hapo juu huweza kumpata binadamu kwa njia ya maambukizi

duh haya hayo magojwa unaweza elezea dalili zake ,cure
 
munirah, Napenda kujuwa hawa Komodo wanapatika ktk mapori yetu hapa TZ ? au (Africa in general)
_44729273_lizard66.jpg
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom