Uliza ujibiwe Kisayansi kuhusu viumbe pori

Uliza ujibiwe Kisayansi kuhusu viumbe pori

mkuu munira..hawa dinosours ilikuwaje wakatoweka?? na je ni kweli hapakuwah kutokea binadamu kuwahi kuwaona?? mana inasadikiwa waliishi miaka miiingi kabla ya ujio wa binadamu duniani...hii fact ni kweli??
 
pia ni kwa nini hawa nyoka wakubwa kabisa wajulikanao kama anaconda wanapatikana zaid misitu ya amazon na si kwingineko?? je nature ya hyo misitu ina nin mpaka wawepo huko tu??alafu ni kweli ana uwezo huo tunaouona kwenye movies?? au ni chai tu??
 
pia kwenye thread ya "je wajua special thread" kuna mdau alisema mnyama ajulikanae kwa jina la kicheche ana uwezo wa kufanya mapenzi mara26 kwa siku..hii ndo mana imepelekea hata binadamu mzinzi sana kuitwa jina hilo..sasa je kisayansi hiyo tabia ya huyo mnyama kupenda kugegeda kwa idadi hizo ni kweli?? na kama ni kweli hapa lengo ni kuzaana au starehe tu?? kama ni kuzaana naimagine wangekuwa wengi mno...nitoe utata huu
 
duuhh nina maswali mengi mkuu usinichoke
lingine ni kweli mdudu tandu au centipede ana sumu kali sana kuliko sumu aliyonayo nge??
 
kwa macho ya binadam ni ngumu kutofautisha kati ya fisi dume na fisfisi jike lakin waKwa wao wanajuana. Hii nilisoma kwenye dailymail uk online newspaper kwenye zoo huko japan waliaagiza fisi wakidhan dume na jike na ikumbukwe hao walikuwa wataalam. Cha kushanga yote yalikuwa madume na hayakuthubutu kugegedana. Walishanga iliwachukua muda sana kutafit

DN asante kwa hints am humbled!

Suala la jinsia ya fisi ni mada inayovutia kwakweli! Fisi unlike other mamalia especially carnivores anageuka kuwa very interesting!
Lakini cha kushika hapa ni uwepo wa kitu kinaitwa 'Pseudopenis' au false penis kwa fisi jike which has become a huge controversy among many researchers! ni jukumu letu sasa kuwasoma wanyama wetu na tuache zile zana za hadithi mbalimbali.
 
mkuu munira..hawa dinosours ilikuwaje wakatoweka?? na je ni kweli hapakuwah kutokea binadamu kuwahi kuwaona?? mana inasadikiwa waliishi miaka miiingi kabla ya ujio wa binadamu duniani...hii fact ni kweli??

Viumbe hawa walianza kutoweka takribani miaka milioni 66 ilopita na katika tafiti nyingi inasadikiwa kuwa vyanzo vya kutoweka kwao vinatofautiana kati ya mtafiti mmoja na mwingine huku pia wakipigana sana! Kwa faida yetu ni vema tukajua tu kuwa ishu ya saizi 'body size' ilichangia sana hasa ukizingatia kuwa dinors walikuwa wakubwa mno kulipotokea majanga ya asili walishindwa kujificha na hivyo kupelekea kufa kwa wingi huku viumbe kama wadudu wakipona kutokana na kuwa na uwezo wa kupenyeza na kujificha kukwepa majanga hayo ambayo yaweza kuwa baridi au joto ilizidi na kuhatarisha uhai wao! hata hivyo kupona kwa wadudu kwa wingi kulichangia kuinuka kwa viumbe wengine walioepuka majanga hayo kwa kuwa sasa wadudu walitumika kama chakula.
 
Kwa nini simba hawezi fanya mapenzi na ndugu yake (family member) lakini kuna binadamu wanaduu na watoto wao?

Kwanza tufahamu kuwa simba ni wanyama jamii ya paka ambao wao pekee ndio wanaishi kwa makundi ama kitaalamu tunaita 'pride' kundi moja linamilikiwa na dume mmoja 'dorminant male' na majike kadhaa
Watoto madume wanafukuzwa kundini kati ya miaka 2-4 wanakuwa
bachelor males ambapo watazurura na kwenda kupigania nafasi ya kumiliki pride nyingine! Watakapomuua dorminant male wa kundi jingine, kundi jipya huundwa kati ya mshindi na wajane! Hali hii hutokea kati ya miaka 3-5 ndipo bachela mmoja ataweza kupata mwenza! Kuna muda mfupi sana kati ya jike kuzaliwa na kukuwa na kuweza kuzaa na baba yake kwakuwa itamlazimu jike afikishe miaka 4 aweze kuwa tayari kwa kuzaliana! Wakati huo kumbuka kuna madume yanakuja kupigana na baba yake! Mara nyingi dorminant male anaangushwa madarakani huku mabinti zake wakiwa wadogo au ikitokea wameweza kujamiana watatoa viumbe dhaifu kwakuwa hakutakuwa na mchanganyiko wa vinasaba tofauti tofauti vya kuwakinga na majanga hapo baadae!

Zipo sababu za msingi behind this ila ukipitia hapa utafaidika zaidi http://cc.ysu.edu/~helorime/inbred.html

Kwa upande wa binadamu ni ubishi tu hakuna tija
 
Naomba niulize swali. Je ni kweli Rhino/kifaru anakula nyama na mimea pia? Maana nimesoma somewhere wamesema ni Omnivore animal.
Na kama ni kweli mechanism ya digestion inakuaje? Na je ana meno ya kutafunia hiyo nyama?

Si kweli kuwa Rhino ni Omnivires unless utupe hicho chanzo tukifanyie kazi! Rhino ni mla majani au "herbivore" na mechanism ya digestion iko kawaida kama herbivores wengine isipokuwa wana uwezo wa kuchachusha chakula kupitia utumbo wa nyuma 'hindgut' hivyo kuwafanya kuweza kula vyakula vigumu (fibrous foods)

Hata hivyo kwa aina ya Rhino waliopo Afrika, wanakosa meno ya mbele hivyo kuwafanya wawe na the so called prehensile lips inayowawezesha kuweza kula vizuri majani ya mwituni.

Samahani kwa kuchelewa kujibu nilikuwa napitia baadhi ya facts kuwa na hakika na kile nachokujibu
 
Katika tafiti zilizofanyika maeneo mengi duniani ikiwemo Tz magonjwa kama trichinosis,
filariasis, sarcoptic mange, pentastomiasis,
echinococcosis, taeniasis, hepatozoonosis,
anthrax, babesiosis na rickets yamebainika kuwa na athari kubwa kwa Simba hivyo kutishia uwepo wao wa baadae na hata mengine huweza kuhamia kwa binadamu! Nikimaanisha magonjwa 6 kati ya nilotaja hapo juu huweza kumpata binadamu kwa njia ya maambukizi

tuje kwenye zonosis je ni kwa extent gani magonjwa ya wanayama yamekuwa yanaathiri binadamu kutokana na mwingiliano wetu kimaisha na wanyama hao?
hapa naongelea zaid wanyama waasili ya nyani, ngedere, tumbili and the like
 
tofauti ya hao mijusi na dinosaurs ni nini?

imeniwia ngumu kujibu but nadhani utakuwa na knowledge kidogo kupitia vyanzo mbalimbali

majibu ya tofauti ya ........na .........ni vema tuki gugo plz
 
tuje kwenye zonosis je ni kwa extent gani magonjwa ya wanayama yamekuwa yanaathiri binadamu kutokana na mwingiliano wetu kimaisha na wanyama hao?
hapa naongelea zaid wanyama waasili ya nyani, ngedere, tumbili and the like

Asante

Wildlife diseases au magonjwa ya wanyamapori yamekuwa na madhara makubwa especially kwa jamii za watu waishio pembezoni mwa hifadhi za kitaifa! Ikiwa kuna possibility ya kuambukiza binadamu, yaweza pia kuathiri mifugo yao kwa mfano mbwa mwitu mwenye ugonjwa akimuuma mbuzi atamwachia ugonjwa na mbuzi akiliwa na binadamu the same!

Lakini pia rejea ishu ya ugonjwa wa ebola unaodhaniwa chanzo chake kinatokana na nyamapori ambapo hadi sasa ebola imeua takribani watu 15000 Magharibi mwa Afrika
 
Shukran munirah kwa elimu nzuri. Allah Barik
 
Last edited by a moderator:
Asante

Wildlife diseases au magonjwa ya wanyamapori yamekuwa na madhara makubwa especially kwa jamii za watu waishio pembezoni mwa hifadhi za kitaifa! Ikiwa kuna possibility ya kuambukiza binadamu, yaweza pia kuathiri mifugo yao kwa mfano mbwa mwitu mwenye ugonjwa akimuuma mbuzi atamwachia ugonjwa na mbuzi akiliwa na binadamu the same!

Lakini pia rejea ishu ya ugonjwa wa ebola unaodhaniwa chanzo chake kinatokana na nyamapori ambapo hadi sasa ebola imeua takribani watu 15000 Magharibi mwa Afrika

hivi sasa huoni kwamba kuna haja ya kuwepo na isolation ili sasa kusiwe na muingiliano kati ya wanyama wa porini na wanadamu?
nasem ahivyo manake naona elimu ya zonosis inayotolewa haina jibu la moja kwa moja juu ya magonjwa haya yatokayo kwa wanyama wa porini.
 
Unapowinda unaweza kuwakamata wanyama kama swala na sungura kwa kutumia mbwa,kwanini unapomfukuzia mbweha huwa mbwa anakuwa mpole,anaweza kumfuata halafu akifika wanaangaliana tu au kunusana then kila mtu anaenda zake
 
Kwanini popo akiwa kwenye mti anakuwa kichwa chini miguu juu?
Kwanini hata wakati wa kula anakaa kichwa chini miguu juu?
Jee wakati wa kwenda haja yaani kutoa kinyesi hukaa kichwa chini miguu juu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom