munirah
JF-Expert Member
- Mar 13, 2015
- 551
- 224
- Thread starter
- #161
kwanini nguo mpya ama nguo safi ukivaa kwa muda ukivaa kwa muda mrefu bila kubadlisha baadae unakuta hyo nguo ina viumbe hai? maarufu kwa jina CHAWA? wanatokea wapi? ama uchafu unabadlikaje kua CHAWA?
source mimi mwenyewe na nguo zangu!!
Umeuliza kimasihara lakini naomba nikujibu kitaalamu!
Chawa kwa kingereza huitwa Louce (Umoja) au Lice (Wingi). Ni kundi la Spishi za wadudu wasio na mabawa zaidi ya 3000!
Wanagawanyika kulingana na maeneo wanayoleta madhara na husababisha magonjwa tofauti kulingana na aina ya chawa husika!
Mfano ugonjwa wa pediculosis angalia hapa http://en.m.wikipedia.org/wiki/Pediculosis
Chawa hupenda kuishi katika maeneo yaliyojificha kama kwenye mikunjo ya mwili (scalps) au katika nywele za sehemu za siri (pubic hairs)
Sasa unaweza kuona ni maeneo ambayo yanakaribisha uchafu kwa kiwango kikubwa!
Nguo mpya haina uchafu! hivyo nguo chafu ni mwenyeji mzuri wa chawa kwa maana nyingine!
Muhimu kujua ni kwamba uchafu haubadiliki kuwa chawa bali una waalika chawa!
Na njia bora ya kuwazuia chawa ni kuzingatia usafi hasa maeneo tajwa hapo juu!