Ningependa kujua unazungumzia jike wa mbwa gani? je ni mbwa mwitu (L. pictus) au?
Lakini kimantiki yai la jike la mnyama yeyote hurutubishwa mara moja tu na mbegu za dume husika na baada ya yai kurutubishwa kuna mechanism hutokea kuzuia multisperms au yai kurutubishwa zaid ya mara moja!
Zipo sababu nyingi za majike ya viumbe vingi duniani kukutana kimwili na dume zaidi ya mmoja katika kipindi cha kuzaana au mating season hasa kwa wanyama kama jamii ya nyani!
Sababu mojawapo ni mama kuhakikisha kuwa anapata ulinzi kwa madume yale pindi atakapozaa watoto maana kila baba atahisi anahusika moja kwa moja katika malezi na ulinzi wa watoto hao huku ukweli utabaki kuwa wa kwanza kuingia ndio ana higher probability of mating success.
Je ungependa kujua jambo gani kuhusu viumbe pori waliopo Tanzania na popote duniani ikiwezekana! Lengo ni kupata elimu ya maswala tata yanayohusu wanyama mwitu tukijumuisha maisha yao, tabia zao na mambo mengine mengi!
Karibu tushirikiane kujibu pale ambapo tuna elimu japo kidogo.
Niliwahi kuwakuona Twiga wakizungushiana shingo, nikafuatilia kidogo nikakuta inaitwa 'necking'.. ni kwanini wanafanya hivyo?
Binadamu hufanya sexual intercourse ili kuzaliana na pia ili kujiliwaza (pleasure)..kuna kiumbe pori kinafanya sexual intercourse kwa ajili ya pleasure??
Kuna aina nyingi ya vinyonga #SPECIES ambapo kwa kila aina....rangi ya ngozi inatofautiana kwa hiyo siwezi kusema rangi moja tu kwamba ni wanjano au bluu! inategemea na aina ya kinyonga unayozungumzia
hivi hakuna uwezekano wa baba wa mtoto huyo wa nyani kugundua kuwa yeye ndio baba mzazi kwa njia ya harufu au kumnusa?
Ningependa kujua kuhusu nyoka wenye sumu kali kwa undani mkuu
Ni ngumu! kwakuwa kikubwa kinachotokea ni yai la jike kurutubishwa na kuzuia mbegu zingine zisipenye sasa ungekuwa dume anaingiza mtoto kwa jike ndo tungeona yafaa kunusa! na kusema huyu ni mwanangu
Ndege kama mwewe huzunguka angani wakiwa umbali mrefu na kuangalia ardhini kutafuta chakula, jicho lake lina uwezo mkubwa kuliko la binadamu??
Acha' kula' bange ndugu si kitu kizuri.
Ok mkuu nisaidie wewe kujibu
Je kuna ukweli wowote kuhusu Nungunungu kurusha miba yake.