Uliza ujibiwe Kisayansi kuhusu viumbe pori

Uliza ujibiwe Kisayansi kuhusu viumbe pori

Kuna hadithi mbali mbali zimekuwa zikitoka kuelezea wanyama wa mwituni na tabia zao wakiwamo hao ndege wakubwa! Yapo makosa makubwa na zipo faida as well!

TUFAHAMU KUWA
Kwa Afrika yetu ndege mkubwa anayepaa ni ndege aitwaye Kori bustard (Ardeotis kori) ambae hawezi kubeba mbuzi na kidunia ndege mkubwa kabisa ni Mbuni ( Struthio camelus)

Nimeshuhudia ndege kama Martial Eagle akibeba wanyama wadogo kama sungura na swala wadogo ambao ni jamii ya mbuzi
lakini wamepotea sana siku hizi ....kisayansi ni kwa sababu gani?
 
Attachments

  • ego.jpg
    ego.jpg
    14.1 KB · Views: 604
Asante mkuu ila niongeze kidogo,je kuna wanyama wenye jinsia mbili?

Back from Noah period! Mungu aliamrisha waingizwe wanyama wake kwa waume! Je alimaanisha nini? Je viumbe kama Tunicates na Snails ambao hawana uti wa mgongo walitoka wapi?

Kuna wanyama wenye jinsia mbili kitaalamu huitwa 'hermaphrodites' ambapo kiumbe kimoja chaweza kuwa jike au dume kulingana na wakati! Hata hivyo hermaphroditism inaegemea sana kwa viumbe wasio na uti wa mgongo au ' invertebrates' lakini pia inajitokeza kwa aina flani ya samaki ambapo jike anaweza kujibadili na kuwa dume pale ambapo madume wanapokuwa wachache au kufa!
 
Kwa nini simba hawezi fanya mapenzi na ndugu yake (family member) lakini kuna binadamu wanaduu na watoto wao?
 
Kuna wanyama wanaitwa Dingo wako Australia, je wana tofauti gani na hawa mbwa mwitu wa Afrika?
 
munirah, Napenda kujuwa hawa Komodo wanapatika ktk mapori yetu hapa TZ ? au (Africa in general)
_44729273_lizard66.jpg

Kwanza samahani kwa kuchelewa kukujibu

Komodo (Varanus komodoensis) ni aina ya mjusi ambae ndio mkubwa zaidi duniani akiitwa Komodo dragon anatokea familia ya mijusi iitwayo VARANIDAE. Aina hii ya mijusi ni maarufu sana nchini Indondesia katika baadhi ya visiwa kikiwemo kisiwa cha Komodo!

Hapa kwetu hatuna aina hii ya mijusi na wala hakuna rekodi inayoonyesha walikuwepo isipokuwa kuna aina nyingine za mijusi kenge sehemu mbali mbali na ukifanikiwa kupita Chuo kikuu cha Dar es Salaam utaweza kubahatika kuona mjusi kenge mkubwa maeneo ya Academic bridge nimekuwa nikimuona sana kipindi nipo pale. Chanzo: Mtandao
 
Last edited by a moderator:

Mashkurra (thank you) kwa majibu muwafaqa... Mie nawafuatilia hao komodo na athari zao!!
BarakaAllah-fikum.
 
Unaposema "viumbe pori" nadhani unamaanisha wanyama na mimea.swali langu ni hili 'kwanini unapovuta bangi iliyopandwa sehemu kame inakuwa ni kali kuliko iliyopandwa kwe udongo we kila mahitaji ya mmea"?

Acha' kula' bange ndugu si kitu kizuri.
 
lakini wamepotea sana siku hizi ....kisayansi ni kwa sababu gani?

Sababu kubwa za kupotea kwa kiumbe chochote kwa zama hizi ni ukuaaji wa shughuli za kibinadamu zinazominya maeneo yao makhusi kwa kuzaliana! bado nasisitiza ndege wakubwa wengine bado wapo na ni jukumu letu kuwatunza
 
Unaruhusiwa kutoa mchango wako pale ambapo nimejibu ndivyo sivyo
 
Inategemea na aina husika ya kinyonga ambapo tunawatenga katika makundi makuu mawili yaani kitaalamu tutawaita OVIPAROUS ambao wanataga mayai siku 3-6 baada ya jike kupandwa na OVOVIVIPAROUS ambao kimtazamo anaonekana anazaa lakini kiuhalisia anataga mayai na kuyahifadhi katika ngozi laini baada ya kurutubishwa na baada ya muda mayai yale yatapasuka pamoja na ngozi ile laini halafu watoto watatoka (hatchling) kwa hali hii utaona wanazaa lakini siyo.

Mkuu nilisikia kinyonga akishamaliza kuzaa anapasuka na kufa hapohapo je ni kweli?
 
Kwa heshima kuu mkuu mara utakapomaliza kujibu swali la miss chagga nikuombe utuondolee utata kuhusu jinsia ya mnyama fisi,je ni kweli kuwa wote ni multisexes?pili ni je kwa hali ya kawaida mnyama kama chui anaweza kufugika? Hayo kwanza.
kwa macho ya binadam ni ngumu kutofautisha kati ya fisi dume na fisfisi jike lakin waKwa wao wanajuana. Hii nilisoma kwenye dailymail uk online newspaper kwenye zoo huko japan waliaagiza fisi wakidhan dume na jike na ikumbukwe hao walikuwa wataalam. Cha kushanga yote yalikuwa madume na hayakuthubutu kugegedana. Walishanga iliwachukua muda sana kutafit
 
Last edited by a moderator:
Kwanza samahani kwa kuchelewa kukujibu

Komodo (Varanus komodoensis) ni aina ya mjusi ambae ndio mkubwa zaidi duniani akiitwa Komodo dragon anatokea familia ya mijusi iitwayo VARANIDAE. Aina hii ya mijusi ni maarufu sana nchini Indondesia katika baadhi ya visiwa kikiwemo kisiwa cha Komodo!

Hapa kwetu hatuna aina hii ya mijusi na wala hakuna rekodi inayoonyesha walikuwepo isipokuwa kuna aina nyingine za mijusi kenge sehemu mbali mbali na ukifanikiwa kupita Chuo kikuu cha Dar es Salaam utaweza kubahatika kuona mjusi kenge mkubwa maeneo ya Academic bridge nimekuwa nikimuona sana kipindi nipo pale. Chanzo: Mtandao

tofauti ya hao mijusi na dinosaurs ni nini?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom