Kwanini popo akiwa kwenye mti anakuwa kichwa chini miguu juu?
Kwanini hata wakati wa kula anakaa kichwa chini miguu juu?
Jee wakati wa kwenda haja yaani kutoa kinyesi hukaa kichwa chini miguu juu?
Popo ni mamalia pekee anayepaa angani! Viumbe hawa hawana uwezo wa kutembea kabisa hasa ukizingatia miguu yao haijakuwa imara kuwawezesha kutembe nikiwa na maana ni mifupi na haina nguvu!
Hata hivyo popo wameendelea kuwepo katika uso wa dunia kwa sababu tu wana uwezo wa kupaa tena wanaanza kupaa wakiwa tayari wananing'inia juu ya sehemu kama mapango; madaraja nk
Katika mabawa yake kuna vishikizo 'claws' anavyotumia kumwezesha kujishika juu ya paa au roofs.
Haimchukui nguvu sana wakati wa kuanza kupaa au 'take-off' kama inavyowakuta ndege ambao inabidi kwanza akimbie kwanza ndo apae!
Kulala vile kunawasaidia mambo mengi ikiwemo kujikinga na maadui!
Kwa upande wa kula mara nyingi popo hula usiku (Nocturnal) hivyo hutoka pale tu giza linapoingia kwenda kutafuta chakula kama wadudu matunda na damu! Inategemea na aina ya popo!
Mfano vampire bat yeye hutoka kwenda kufyonza damu za viumbe wengine ambao wamelala usiku na baada ya kutosheka anarudia makazi yake 'roosting site' kupumzika na kuruhusu mmeng'enyo wa chakula.
Hivyo basi sidhani kama popo anakula chakula akiwa RS.
Popo wanajisaidia wakiwa RS mara nyingi au wakiwa wanapaa angani na hii inatokana na wingi wa vinyesi vyao maeneo ya RS ambao wanaishi kwa makoloni