Ukweli mtupu: Wananchi tunataka haki ya kumuondoa mbunge asiyefaa kabla hajamaliza muda. Kwanini wana-CCM wasiopenda haki mnaipinga?

Hii ni mada yenye hoja inayostahili kujadiliwa. Tatizo ni kwamba mtoa mada ana yake. Hapo hapo kwenye kichwa cha habari anauliza kwa nini wana-CCM msiopenda haki mnapinga hili, kabla hata mtu hajajadili hoja yake. Ni dhahiri nia yake ni kuweka uwanja wa mapambano kati ya CCM na Upinzani, bila kujali mawazo binafsi ya wana-CCM na wana-Upinzani.

Mimi binafsi naipinga hoja. Ahadi zinazotolewa na mbunge ni kwamba katika miaka mitano nitafanya kadha wa kadha. Huwezi kumtimua mtu baada ya miaka miwili tu kwa kigezo cha kutotimiza aliyoahidi kuyafanya katika miaka mitano. Kwanza, mtaanza kumjadili mbunge baada ya muda gani? Miaka mitatu? Miwili? Mmoja? Itakuwa fujo tu.

Aidha, kwa nini iwe kwa mbunge tu na si kwa Rais au mkuu wa shirika anayepewa uongozi kwa mkataba wa miaka kadhaa? Kwa nini mkuu wa Air Tanzania, au Shirika la Reli, au Vice-Chancellor wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam aachiwe amalize muda wa mkataba wake bila kujali ufanisi wake wakati mheshimiwa mbunge anathibitiwa kabla ya kumaliza miaka yake mitano?

Jambo zuri ni kutathmini utendaji wa mtu baada tu ya kipindi alichopewa. Hapo ndipo wananchi wataamua kwa mbunge kumrudisha au sivyo.
Umeeleza vizuri. Wananchi wakiruhusiwa kumtimua mbunge kabla ya muda wake kuisha kutafungua uwanja kwa fitna, rushwa na uchaguzi uisha.

Wananchi wanapewa fursa kila baada ya miaka mitano kumtathmini mwakilishi na kama wataona anapwaya kumtimia na kumpa nafasi hiyo mtu mwengine.

Inashangaza kuwa pamoja na kuonekana wazi kuwa wanapwaya, wanaendelea kuwarudi hao hao bungeni. Na wale wanaosimama kidete kuwatetea ndio wanao timuliwa.

Aidha, inabidi kuondokana na dhana ya kuwa mbunge wajibu wake ni kuleta maendeleo ambapo wajibu huo ni wa serikali. Wsjibu wa mbunge ni kuisimamia ilete hayo maendeleo.

Kama, pamoja na mbunge kupigania watu wake, serikali ikakataa kuleta hayo maendeleo, wananchi watakuwa na haki ya kuiadhibu kwa kuiondoa madarakani.

Dhana hii potofu ndio inafanya wabunge kutumia muda mwingi kufanya vituko kama kutoa mapipa ya taka kama ishara ya utendaji kazi wao.

Amandla....
 
Kwa tabia zetu hilo wazo halifai kabisa, kwa kuwa wakati mwingine kwa sababu ya fitina tu, tunaanza kujenga hoja za kumfitini mtu na wapiga kura wake ili kumkomoa.
 
Ni utaratibu mzuri tu ambao unatakiwa kuwekwa kwenye katiba ya JMT ili wananchi tusiporidhika na ahadi tulizopewa na mbunge tuliomchagua tuwe tuna uwezo kuweka azimio na likishapita huyo mbunge anatolewa kwenye nafasi hiyo na uchaguzi unaitishwa.

Wabunge wengi wanaunga mkono sera na hoja ambzazo hazina maslahi kwa wananchi na taifa.

Wabunge wengi wanaishi nje ya majimbo yao ya uchaguzi zaidi ya miezi sita na wanakuja jimboni tu uchaguzi ukikaribia.

Hivyo ni wakati wa katiba yetu kufanyiwa mabadiliko haraka, kutungwa sheria namna wananchi watamuondoa mbunge asiyefaa na uchaguzi kufanyika.

Najua CCM imejaza bungeni wabunge lukuki wasiofaa na kazi yao ni kuunga mkono sera na hoja ambazo hazina maslahi kwa wananchi ndio maana wanaogopa sana.
Kosa kubwa mlilolifanya ni kufikiri Bunge la chama kimoja linafaa !!. Na kudhani serikali isipokuwa exposed ktk mapungufu yake, eti ni maendeleo. Nchi zote zilizopiga hatua endelevu ni zile za ki democracy

Pili kulinyima Bunge mamlaka yake ya kibunge la kuielekeza serikali nini cha kuwatendea wananchi. Leo hii Bunge na wabunge badala kupereka hoja za maendeleo ya wananchi. Wamebaki kushindana kusifu na kuabudu .
 
Hili suala tuliliweka kwenye ile rasimu ya katiba ya Tume ya Warioba. Kwa kuwa tulishindwa kuipitisha kwa kujali sana u vyama, acha tushike adabu. Lakini naunga mkono suala la wananchi kuwa na mamlaka ya kumuondoa mbunge wao madarakani kama kawajibiki kwa kadri ya kiapo chake
 
Kosa kubwa mlilolifanya ni kufikiri Bunge la chama kimoja linafaa !!. Na kudhani serikali isipokuwa exposed ktk mapungufu yake, eti ni maendeleo. Nchi zote zilizopiga hatua endelevu ni zile za ki democracy

Pili kulinyima Bunge mamlaka yake ya kibunge la kuielekeza serikali nini cha kuwatendea wananchi. Leo hii Bunge na wabunge badala kupereka hoja za maendeleo ya wananchi. Wamebaki kushindana kusifu na kuabudu .
Ndio maana tunataka tuwe na Katiba ambayo ikitokea mbunge akazingua anaondolewa na wananchi

Ila sikubaliani na wewe kuwa bunge ni la chama kimoja.
 
Hivi wewe chagu wa malunde . Katiba mpya utaipataJe wakati CCM haitaki katiba yenye maslahi ya wananchi dhidi ya watawala ?!

Kwamba leo, wewe hujui kwanini rasimu ya Jaji Warioba ilipokwamia ?!.

Kulikuwa na ahadi ya kulimia meno. Wacha tuipate wote
 
Ni utaratibu mzuri tu ambao unatakiwa kuwekwa kwenye katiba ya JMT ili wananchi tusiporidhika na ahadi tulizopewa na mbunge tuliomchagua tuwe tuna uwezo kuweka azimio na likishapita huyo mbunge anatolewa kwenye nafasi hiyo na uchaguzi unaitishwa.

Wabunge wengi wanaunga mkono sera na hoja ambazo hazina maslahi kwa wananchi na taifa.

Wabunge wengi wanaishi nje ya majimbo yao ya uchaguzi zaidi ya miezi sita na wanakuja jimboni tu uchaguzi ukikaribia.

Hivyo ni wakati wa katiba yetu kufanyiwa mabadiliko haraka, kutungwa sheria namna wananchi watamuondoa mbunge asiyefaa na uchaguzi kufanyika.

Najua CCM imejaza bungeni wabunge lukuki wasiofaa na kazi yao ni kuunga mkono sera na hoja ambazo hazina maslahi kwa wananchi ndio maana wanaogopa sana.
Dawa ni kpatikana kwa katiba mpya itakayozingatia jambo hili.
 
Pambaneni na magalasa yenu ,time will tell hatutaki mlielie wengine ni darasa la 3
 
Hivi wewe chagu wa malunde . Katiba mpya utaipataJe wakati CCM haitaki katiba yenye maslahi ya wananchi dhidi ya watawala ?!

Kwamba leo, wewe hujui kwanini rasimu ya Jaji Warioba ilipokwamia ?!.

Kulikuwa na ahadi ya kulimia meno. Wacha tuipate wote
Jaduong kukwama kwa rasimu ya Jaji Warioba sio sababu ya kukata tamaa. Sio wana Ccm wote wanakataa katiba mpya.
 
Jamani tufahamu tu kuwa sio rahisi kila jambo likawa suluhisho yake ni kubadili katiba.

Mambo mengine yanaweza kurekebishwa kwa kufanyia marekebisho sheria zinazohusiana na jambo husika,

Ama la, katika itakua kitabu kimoja kikubwa sana kuwahi kutokea.
 
Mataga wakikujib naomba uniTAG

Back
Top Bottom