Ukweli mtupu: Wananchi tunataka haki ya kumuondoa mbunge asiyefaa kabla hajamaliza muda. Kwanini wana-CCM wasiopenda haki mnaipinga?

chagu wa malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,284
2,000
Ni utaratibu mzuri tu ambao unatakiwa kuwekwa kwenye katiba ya JMT ili wananchi tusiporidhika na ahadi tulizopewa na mbunge tuliomchagua tuwe tuna uwezo kuweka azimio na likishapita huyo mbunge anatolewa kwenye nafasi hiyo na uchaguzi unaitishwa.

Wabunge wengi wanaunga mkono sera na hoja ambazo hazina maslahi kwa wananchi na taifa.

Wabunge wengi wanaishi nje ya majimbo yao ya uchaguzi zaidi ya miezi sita na wanakuja jimboni tu uchaguzi ukikaribia.

Hivyo ni wakati wa katiba yetu kufanyiwa mabadiliko haraka, kutungwa sheria namna wananchi watamuondoa mbunge asiyefaa na uchaguzi kufanyika.

Najua CCM imejaza bungeni wabunge lukuki wasiofaa na kazi yao ni kuunga mkono sera na hoja ambazo hazina maslahi kwa wananchi ndio maana wanaogopa sana.
 

Bunsen Burner

Senior Member
Feb 25, 2009
170
225
Yaani hiyo ingekuwa nzuri sana...' soma sort of Mid- term Election' ili kuondoa 'non performing parliamentarian' ambao wao wakiingia bungeni tu, baasi wanajua wanauhakika wa 250 m.. wanasinzia tu bungeni, wanasubiri miaka 5 uishe wapate pesa ya uhakika, wakati performance kwa wananchi wao ni zero, na hamuwezi wafanya chochote.

Maana yake hata mbunge akihudumu one term, tayari atakuwa anachelewa kuwazidi nyie wengine, mnaosubiri pension ya uzeeni kiduchu , mtakayopata after 60 years za kazi... tafakari..
 

Ng'wanamalundi

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
662
1,000
Hii ni mada yenye hoja inayostahili kujadiliwa. Tatizo ni kwamba mtoa mada ana yake. Hapo hapo kwenye kichwa cha habari anauliza kwa nini wana-CCM msiopenda haki mnapinga hili, kabla hata mtu hajajadili hoja yake.

Ni dhahiri nia yake ni kuweka uwanja wa mapambano kati ya CCM na Upinzani, bila kujali mawazo binafsi ya wana-CCM na wana-Upinzani.

Mimi binafsi naipinga hoja. Ahadi zinazotolewa na mbunge ni kwamba katika miaka mitano nitafanya kadha wa kadha. Huwezi kumtimua mtu baada ya miaka miwili tu kwa kigezo cha kutotimiza aliyoahidi kuyafanya katika miaka mitano. Kwanza, mtaanza kumjadili mbunge baada ya muda gani? Miaka mitatu? Miwili? Mmoja? Itakuwa fujo tu.

Aidha, kwa nini iwe kwa mbunge tu na si kwa Rais au mkuu wa shirika anayepewa uongozi kwa mkataba wa miaka kadhaa? Kwa nini mkuu wa Air Tanzania, au Shirika la Reli, au Vice-Chancellor wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam aachiwe amalize muda wa mkataba wake bila kujali ufanisi wake wakati mheshimiwa mbunge anathibitiwa kabla ya kumaliza miaka yake mitano?

Jambo zuri ni kutathmini utendaji wa mtu baada tu ya kipindi alichopewa. Hapo ndipo wananchi wataamua kwa mbunge kumrudisha au sivyo.
 

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
7,610
2,000
Bado mfumo tulio nao siyo rafiki kwa mabadiliko yoyote kwenye katiba, mwananchi hana ruhusa kudai wala kupeleka hisia zake panapo husika ili watawala wajue kilicho nafsini mwa raia.

Utasikia interijensia inaonyesha hakutakuwa na usalama.
 

chagu wa malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,284
2,000
Hii ni mada yenye hoja inayostahili kujadiliwa. Tatizo ni kwamba mtoa mada ana yake. Hapo hapo kwenye kichwa cha habari anauliza kwa nini wana-CCM msiopenda haki mnapinga hili, kabla hata mtu hajajadili hoja yake. Ni dhahiri nia yake ni kuweka uwanja wa mapambano kati ya CCM na Upinzani, bila kujali mawazo binafsi ya wana-CCM na wana-Upinzani...
Unawajua wanaCCM wasiopenda haki? Mtu hajali maslahi ya wananchi wake, hayupo jimboni zaidi ya miezi sita alafu tumsubiri amalize miaka mitano?
 

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
30,693
2,000
Bunge linamamlaka ya kumuondoa rais kama atakuwa hafai.
Bunge lililowekwa madarakani na Rais kupitia wizi wa kura ulioratibiwa na TISS linamtoa vipi Rais madarakani? Kwa nini unaandika vitu kama mtoto wa chekechea? Unafikiri ya kuwa tunaweza kutatua matatizo yetu kwa kujidanganya kuwa hayapo? Yaani unajidanganya kuwa tuna bunge?
 

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
41,288
2,000
Unapataje madarakana ya kumuondowa mbunge ambaye hukumuweka wewe bungeni?

Tueleze kwenye bunge hili ni mbunge yupi ulimpigia kura ambaye yupo bungeni?

Angalau hata wajumbe wa CCM waliinjoy uchaguzi huu kwenye primary vote wamepiga spana za nguvu kutuondolea mpaka kelele za Makonda hapa mjini.
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
41,304
2,000
CCM kimekuwa ni chama cha kutetea vitu vya ajabu kabisa. Wamelewa kwa mvinyo wa madaraka, wamekuwa wavivu wa kufikiri na kutenda pia, na mbaya zaidi hawataki kuwajibishwa
Sababu ni moja hawakuchaguliwa na wananchi mbali ni wabunge wa NEC
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
41,304
2,000
Bado mfumo tulio nao siyo rafiki kwa mabadiliko yoyote kwenye katiba, mwananchi hana ruhusa kudai wala kupeleka hisia zake panapo husika ili watawala wajue kilicho nafsini mwa raia.

Utasikia interijensia inaonyesha hakutakuwa na usalama.
Hatuna katiba mkuu tuna andiko pekee
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom