Ukweli mtupu: Wananchi tunataka haki ya kumuondoa mbunge asiyefaa kabla hajamaliza muda. Kwanini wana-CCM wasiopenda haki mnaipinga?

Ni utaratibu mzuri tu ambao unatakiwa kuwekwa kwenye katiba ya JMT ili wananchi tusiporidhika na ahadi tulizopewa na mbunge tuliomchagua tuwe tuna uwezo kuweka azimio na likishapita huyo mbunge anatolewa kwenye nafasi hiyo na uchaguzi unaitishwa.

Wabunge wengi wanaunga mkono sera na hoja ambazo hazina maslahi kwa wananchi na taifa.

Wabunge wengi wanaishi nje ya majimbo yao ya uchaguzi zaidi ya miezi sita na wanakuja jimboni tu uchaguzi ukikaribia.

Hivyo ni wakati wa katiba yetu kufanyiwa mabadiliko haraka, kutungwa sheria namna wananchi watamuondoa mbunge asiyefaa na uchaguzi kufanyika.

Najua CCM imejaza bungeni wabunge lukuki wasiofaa na kazi yao ni kuunga mkono sera na hoja ambazo hazina maslahi kwa wananchi ndio maana wanaogopa sana.

Ndio unajua leo kuhusu hao wabunge mzigo wa ccm? Hao wabunge majizi ya kura hawawezi kukubali wananchi wawatoe maana hawajachaguliwi na wananchi, bali mfumo mbovu wa uchaguzi kupitia katiba outdated, inayolindwa kwa hila na mabavu chini ya viongozi walevi wa madaraka.
 
Ndio unajua leo kuhusu hao wabunge mzigo wa ccm? Hao wabunge majizi ya kura hawawezi kukubali wananchi wawatoe maana hawajachaguliwi na wananchi, bali mfumo mbovu wa uchaguzi kupitia katiba outdated, inayolindwa kwa hila na mabavu chini ya viongozi walevi wa madaraka.
Tafadhali ukijadili mada kama hii punguza jazba.
 
Jamani tufahamu tu kuwa sio rahisi kila jambo likawa suluhisho yake ni kubadili katiba.

Mambo mengine yanaweza kurekebishwa kwa kufanyia marekebisho sheria zinazohusiana na jambo husika,

Ama la, katika itakua kitabu kimoja kikubwa sana kuwahi kutokea.

Tatizo lote la katiba yetu liko kwenye madaraka ya urais yaliyo juu ya katiba. Kama rais anaweza kufanya lolote na kumteua yoyote, kwanini katiba isibadilishwe ili kila mtu aweze kushitakiwa kwa kukiuka sheria? Hakuna chochote unaweza kubadilisha bila rais kuridhia kwa mujibu wa katiba hii mbovu.
 
Back
Top Bottom