Mtoboasiri
JF-Expert Member
- Aug 6, 2009
- 5,100
- 1,955
Asante sana Zinduna kwa kuleta maada hii. Nimesoma michango ya watu wengi hapa - mingine ikiwa imejaa kejeli - lakini wengi wanaokupinga wameshindwa kutofautisha Mtanzania na msomi wa Kitanzania. Ukweli ni kuwa Watanzania wakipewa elimu sahihi wengi wataweza kumudu ushindani wa kimataifa (mifano iliyoletwa hapa mingi ni ya Watanzania waliobahatika kupata elimu nje ya Tanzania LAKINI si ya Watanzania waliosomea hapa hapa nchini na kwa "elimu" hiyo ya Kitanzania wakapata kazi nje ya nchi.