Ukweli mchungu: Wasomi wetu hawauziki…!

Ukweli mchungu: Wasomi wetu hawauziki…!

Zinduna

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2011
Posts
2,377
Reaction score
3,394
Najua kauli yangu hii itawakera wengi hususan hao wanaojiita wasomi, lakini najua kwamba ukweli mara nyingi huwa unauma sana.

Katika orodha ya nchi za Afrika ambazo wasomi wake wanaibwa na kusombwa na kupelekwa huko Ulaya na Marekani kufanya kazi , Tanzania haitajwi kabisa.

Watanzania wengi wanaokwenda nje kufanya kazi, ni vibarua zaidi, wenyewe wanajiita wabeba mabox, na hata kama ni wasomi, basi utawakuta wanafanya kazi ambazo huwezi kusema zitaweza kuisaidia nchi.

Hata hivyo wapo Watanzania wachache sana ambao wamenunuliwa nje na kufanya kazi huko kwa sababu ya uwezo wao kiufahamu katika taaluma zao.

Lakini hii yote ni kutokana na mfumo wetu wa elimu ambao kwa miaka mingi umekuwa ukidumaza akili zetu.
Mara nyingi wadau mbalimbali wakiwemo baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakipiga kelele kuhusu haja ya Serikali kubadili mfumo wa elimu ili kuweza kuwashindanisha wasomi wake na wasomi wa nchi nyingine duniani lakini jambo hilo limeonekana kama vile halina maana.

Najua serikali kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi imeshawahi kubadili mitaala ya elimu mara kdhaa, lakini ninachojaribu kusema hapa ni je tabia ya wanafunzi kukariri ili wafaulu mitihani badala ya kuelewa imekomeshwa kwa kutafuta chanzo chake?

Ukweli ni kwamba, ni vigumu kwa wasomi wengi wa Tanzania kushindana kwenye soko la dunia kitaaluma kwa sababu, hawakuandaliwa kuwa watu wanaofahamu, bali wameandaliwa kuwa watu wanaokariri…
 
Nyongeaza, Elimu ya tanzania inafundisha story za masomo tuyasomayo na ndi maana wengi wetu unaweza kuta performance yake ipo vizuri ila ukimpeleka kwenye vitendo hamna kitu.
 
Nyongeaza, Elimu ya tanzania inafundisha story za masomo tuyasomayo na ndi maana wengi wetu unaweza kuta performance yake ipo vizuri ila ukimpeleka kwenye vitendo hamna kitu.

Hili Serikali imeliona na ndiyo sababu kwa sasa kuna kitu kinaitwa competence-based curriculum ambayo ni tofauti na ile ambayo ilikuwa teacher-centred. Tatizo ni kwamba bado walimu hawajaelewa jinsi ya kuimudu kwa hoyo bado wanafundisha wanafunzi past papers ili waweze kufaulu mitihani. Ila kama walimu watapata orientation hii hali itabadilika na hivyo kuwafanta Watz kuweze ku-compete kwenye soko la ajira au kuwa na ujuzi wa kujiajiri wenyewe.
 
Huyo mwalimu unaesema afundishe kwa huu mfumo mpya, yeye ameusomea wapi huo mfumo kama akusoma ule mfumo wa kukalilisha?



Hili Serikali imeliona na ndiyo sababu kwa sasa kuna kitu kinaitwa competence-based curriculum ambayo ni tofauti na ile ambayo ilikuwa teacher-centred. Tatizo ni kwamba bado walimu hawajaelewa jinsi ya kuimudu kwa hoyo bado wanafundisha wanafunzi past papers ili waweze kufaulu mitihani. Ila kama walimu watapata orientation hii hali itabadilika na hivyo kuwafanta Watz kuweze ku-compete kwenye soko la ajira au kuwa na ujuzi wa kujiajiri wenyewe.
 
Asilimia kubwa ya wasomi wa kibongo wanauzika sana na wengi wanafanya vitu vyao katika nchi za US, UK, UAE , Canada na nyingine nyingi duniani tena wana vyeo vya juu. Hata baadhi ya waajiri kuwaomba Wabongo waliowaajiri kuwapendekeza Wabongo wengine kwa waajiri hao ili nao waajiriwe. Wabongo hao wengi wamejijengea sifa ya uchapakazi, uaminifu, uelewa mkubwa wa kazi zao, kutokuwa walalamikaji.
 
Katika Elimu Tanzania tunatakiwa kubadilisha mambo mengi sana,na la kwanza ni jinsi tunavyowapata waalimu wetu hasa wa shule za msingi,sekondari na hata baadhi ya vyuo vyetu,watu (wanafunzi,wazazi) kubadili mitazamo,Mitaala kuboreshwa au kubadilishwa,mbinu za ufundishaji(vifaa and know how)..n.k.
 
Mkuu bado namba yetu ni ndogo kulinganisha na wenzetu huko majuu na vilevile inachangiwa na ubnafsi wetumaana watu waTanzania waliopo nje tena kwenye nafasi nzuri ni wagumu kutoa information au kuwa-connect wenzao.
Asilimia kubwa ya wasomi wa kibongo wanauzika sana na wengi wanafanya vitu vyao katika nchi za US, UK, UAE , Canada na nyingine nyingi duniani tena wana vyeo vya juu. Hata baadhi ya waajiri kuwaomba Wabongo waliowaajiri kuwapendekeza Wabongo wengine kwa waajiri hao ili nao waajiriwe. Wabongo hao wengi wamejijengea sifa ya uchapakazi, uaminifu, uelewa mkubwa wa kazi zao, kutokuwa walalamikaji.
 
Tz hakuna tofauti kati ya prof na std 7,wasomi ndio wezi,majivuno kibao,ufisadi na kila aina ya takataka,wengi wanataka kuajiriwa tu na ni tegemezi wa kutisha.Afadhali hata yule ambaye hajui kusoma na kuandika kijijini maana analima na watz wote wanafaidi matunda yake
 
Huyo mwalimu unaesema afundishe kwa huu mfumo mpya, yeye ameusomea wapi huo mfumo kama akusoma ule mfumo wa kukalilisha?


Ndiyo maana nimesema wakipewa orientation, they will make it and the whole system will change. Lakini hii inahitaji both political will and commitment on the side of teachers.
 
Mama elimu inakusaidia tu namna ya kujikimu kimaisha.
Tatizo kubwa watanzania hawako daring kuyakabili maisha wanafikiria kila kitu kuajiriwa na serikali.
Na wengi wanafikiri kuenda huko nje ni hivyo hivyo, kudekezwa kimaisha.

Wenzetu kujiajiri au kuajiriwa ni a do-or-die situation.

Nawafahamu watanzania walioko nje wanao weka mzigo wa kufa mtu!

Jamaa mmoja nimemkuta New York, pamoja na degree yake ya Masters katika Adminisration anafanya kazi kweli kweli na anaishi sehemu nzuri sana kimaisha, sehemu wanayokaaa wtu wanaojiweza.

Kwa hiyo tatizo si elimu bali attitude ya mtu kujiamini.
 
Naomba tu Busara itawale katika kujadili hii mada....
Katika kupinga hoja yako iliyojaa dharau na kejeli kwetu waTanganyika tulioajiriwa nje, nitaanza na hiyo picha yako. Hiyo Laptop ipo on, na webcam inarecord uchafu unaofanywa na huyo prostitute kwa mikono yake kustarehesha wengine. Kwa akili zako zilivyo ndogo ulidhani its funny kuweka uchafu. Kwa kuwa wewe ni mchafu, mshamba na usiyejua athari za picha kwa wakwe zako au wazazi wako. Kuhusu mada uliyoleta, kuna maswali mengi naomba nikuulize. Je unayo takwimu za wabongo wote wanaoishi nje? Je uliwasiliana na employers wa nje kupata maoni yao kuhusu wabongo? Je uliongea na wabongo wangapi na wa nchi ngapi mpaka ukafikia conclusion hii? Nini nafasi yako na elimu yako kwa ujumla?
 
Kuna ka ukweli lakini.
ukweli wenyewe ni kwamba Watanzania walioko nje wako kivyao serikali ya Tanzania hata haijui.
Hizi Data kwamba Watanzania hawauziki si zakweli na sielewi watu wanazitoa wapi.
Binafsi nawajua waTanzania zaidi ya 100 wenye PhD wanao fanya kazi hapa USA tu.

Achilia mbali vijana waliopata divion 4 form six wakazamia hapa ambao sasa wana Masters za Computer science engineering accounting na finance!!!
Hawa wote serikali ya Tanzania bado inawaona ni form six failures.



Serikali yetu ni adui namba moja wa wasomi wake na pengine hiki ndo kisa hasa cha kuwa na viongozi wengi wenye PhD feki katika idara nyeti za serikali ikiwa hata Uwaziri Tanzania.

Akina David Mathayo huyu dogo ni Daktari wa kuchoma mbwa na ng'ombe sindano lakini ndo hivyo ni Dr wa PhD.

Nchimbi, alisoma Diplama pale Mzumbe kwa taabu sana Masters alisoma kwa Remote na PhD hakusoma kabisaaa, lakini ndo hivyo serikali imewakumbatia kama wasomi

Wako wengi sana, wanalindana kama mbwa mwitu wakiwa na baraka za serikali ya CCM

Hata hivyo ni kweli kwamba elimu yetu ni ya kukariri ili ufauru mtihani.

Tunahtakiwa kuandika mtaala wa elimu ya kuwezesha wahitimu kuitumia katika kutatua maisha ya kila siku.
 
mimi naomba nianze kwa kuwataja wasomi ambao ninaajua na mambo wanayoyafanya nje ya nchi yetu.

Wa kwanza kabisa ni mwana jf mwenzetu ambaye yuko Marekani anafanya kazi na kampuni ya glaxo smith yeye ni mtaalam wa fluid micronization technique na sasayuko kwenye post doc.

wa pili nimemsahau jina lake halisi ila yeye yupo Kigali ndiye mtaalam wa biogas production huyu alikuwa ni mwanafunzi wa Dr. rubindamayugi na kwasasa Rwanda ndio nchi inayoongoza Africa kwa matuizi ya Biogas hapa Africa.

Mwingine ni huyu mwanamama Hulda Shaidi Swai huyu yeye ni Nanotechnologist anafanya na CSIR huko SA huyu anagroup ya wanasayansi zaid ya 100 huyu ndiye aliyegundua ANTI TB drug ambayo ni nanomedicine. Dawa hii imeshakuwa patented na soon itaingia sokoni. iko tofauti na dawa za TB za kawaida manake badala ya mtu kumeza dawa kama 60 hivi hapa anameza dawa 1 tu kila baada ya siku 4. kumbuka CSIR ni taasisi kubwa sanaa ambayo ni uti wa mgongo wa viwanda huko SA kwani wanazalisha malighafi nyingi sana kwajili ya viwanda vyao.

mwingine ni huyu aliayetengeneza BIOSENSORS huyu anaitwa Asanterabi Malima, yuko Boston marekani na ana fanyakazi na Biolom( hii ndiyo kampuni inayojihusisha na usambazaji wa biomakers na biosensors) lakini pia ni mwajiriwa wa Centre for High rate Nanomanufacturing (CHN) na anafanya post doc huko Northerneastern University.

haya mimi nimeamua kuwataja hawa wa4 ila ninaamini kwamba wapo wengine ambao watataja. Kimsingi kama kuna mtu anafanya kazi nzuri apewe sifa zake binafsi mie nawakubali sana hawa niliowataja manake ni majembe sana tu.
 
Asilimia kubwa ya wasomi wa kibongo wanauzika sana na wengi wanafanya vitu vyao katika nchi za US, UK, UAE , Canada na nyingine nyingi duniani tena wana vyeo vya juu. Hata baadhi ya waajiri kuwaomba Wabongo waliowaajiri kuwapendekeza Wabongo wengine kwa waajiri hao ili nao waajiriwe. Wabongo hao wengi wamejijengea sifa ya uchapakazi, uaminifu, uelewa mkubwa wa kazi zao, kutokuwa walalamikaji.
BAK uko sahihi sana mkuu, yaani mimi ninamarafiki ambao wameajiriwa UK, USA, CANADA NA SA ambao kwanza utashangaa mambo wanayoyafanya. yaani mimi nilimshangaa mama mmoja anaitwa Hulda swai yaani ukiona team yako na jins alivyo excell utashangaa. ana run centre yenye watu zaid ya 100 ambao wanafanya kazi chini yake na wote wanaperform vizuri.

Nilisikitika sana alipoambiwa arudi Tz na mkuu wa nchi watu wakamtisha ukirudi Tz utafanyiwa majungu bora uendelee kujilia bata wako huko CSIR.
 
Last edited by a moderator:
Unamaana hata Chris Lukosi nae sio msomi akaamua kubeba box?
 
Last edited by a moderator:
Usomi definition yake ni ipi da Zinduna, naomba tuanzie hapo!

Pili, je haiwezekani Watanzania hawaibwi kwa sababu wana uzalendo sana na nchi yao? #jusAskin '
Mentor, Kwa mtazamo wangu msomi ni yule anayezalisha maarifa baada ya tafakari kubwa na ya muda mrefu. Mtu anayejiuliza maswali na kupata majibu ili aweze kuisaidia jamii hapa duniani.

Naomba nikutolee mfano wa Sophocles, na wale wasomi wa kwanza duniani. Hawa ndio tunaoweza kuwaita wasomi, kwa sababu utafiti wao unagusa kila eneo la maarifa bila kujali kama ni sayansi, biashara, tiba au sanaa.
 
Last edited by a moderator:
Elimu zenyewe ndo hizi za kubadili matokeao na kufaulisha wanafunzi ili wasichafue rekodi za watawala!
Unategemea ni products gani zitatoka?
Natabiri kuanzia miaka kumi ijayo nchi hii, products zitakazotoka sio tuu hawatauzika nje ya nchi bali hawatahuzika humu humu nchini.
 
Back
Top Bottom