Ukweli mchungu: Wasomi wetu hawauziki…!

Ukweli mchungu: Wasomi wetu hawauziki…!

Mkuu bado namba yetu ni ndogo kulinganisha na wenzetu huko majuu na vilevile inachangiwa na ubnafsi wetumaana watu waTanzania waliopo nje tena kwenye nafasi nzuri ni wagumu kutoa information au kuwa-connect wenzao.

Namba yetu ni ngapi mkuu, tutajie na source ya information please
 
Jamani elimu yetu sasa hivi ni majanga. Ukikutana na mtu huko ughaibuni anapiga kazi ya uhakika ni M-TZ basi huyo atakuwa wa miaka ya early 90s kurudi nyuma! Sasa hivi watoto wetu unakuta jamaa kamaliza university lakini ukimwuliza hata habari ya Jiografia ya darasa la saba hajui. Juzi hapa nilikuwa nasaidia mtu mmoja kumchapia barua yake ya uhamisho akawa ameandika kwenye anwani yake P.O.BOX....KILOMBERO, nikamwambia hakuna makao makuu ya wilaya ambayo yanajulikana kwa jina hilo akabaki ananishangaa. Nikamweleza makao makuu ya wilaya ya Kilombero ni IFAKARA. Nikaendelea kumwelimisha barua zote zinatakiwa zisomeke P.O.BOX ...IFAKARA, KILOMBERO. Msomi wangu akanipiga swali ulishawahi kuishi IFAKARA? Enzi zetu tulikuwa tunashindana kujua makao makuu ya mikoa, wilaya, nchi n.k pia kujua makabila kwa kila mkoa. Sasa hivi hata mtoto wa TCU hajui haya!

Ni kweli uliyoandika! Kizazi kilichoanza darasa la kwanza miaka ya 90 na kuendelea ni janga. Ni rahisi sana kuwajua hapa JF. Wengi sana hawajui tofauti ya H na A (eg hata vs ata), L na R (eg polisi vs porisi); achilia mbaya kuandika sentensi iliyonyooka! Lakini hatukufika hapa kwa bahati mbaya. Miaka ya 90 wakati tv na radio ndio zinaanza anza kuna kipindi cha watoto walikuwa wanaendesha Masudi Kipanya na marehemu Amina Chifupa. Wao ilikuwa chemsha bongo zao ni kushindanisha watoto kuimba nyimbo za twanga pepeta na the likes. Yalipoingia tena magazeti na radio yakagongea msumari wa mwisho! Nchi nyingine media kama TV, Radio na magazeti zimesheni vipindi vya chemsha bongo lakini Tanzania ni habari za umbeya na bongo flavour. watoto watajifunzaje?
 
Mtoa mada ungekuja na takwimu ingependeza nachojua Tanzania ni inchi isiyokua na idadi sahihi ya wasomi wake walio inje yani ughaibuni sasa takwim zinamuhusu nani. Uk wazanzibar kunakipindi walikua na kiongozi wao yaani wazenj walioko uk bar kushnehi.TUNAJIDHARAU SANA LAKINI HATA HAO UNAODHANI NDO WENYE ELIMU BORA JAPO HUJAWATAJA WANAFANYA KAZI ZIPI?Unaijua idadi ya madreva tax wakenya Iran ndio hio ajira unayosema?.Kuwawengi nje si kigezo cha elim bora.Kwakipindi kiref kulikua na kubanwa kutoka inchini
 
Najua kauli yangu hii itawakera wengi hususan hao wanaojiita wasomi, lakini najua kwamba ukweli mara nyingi huwa unauma sana.

Katika orodha ya nchi za Afrika ambazo wasomi wake wanaibwa na kusombwa na kupelekwa huko Ulaya na Marekani kufanya kazi , Tanzania haitajwi kabisa.

Watanzania wengi wanaokwenda nje kufanya kazi, ni vibarua zaidi, wenyewe wanajiita wabeba mabox, na hata kama ni wasomi, basi utawakuta wanafanya kazi ambazo huwezi kusema zitaweza kuisaidia nchi.

Hata hivyo wapo Watanzania wachache sana ambao wamenunuliwa nje na kufanya kazi huko kwa sababu ya uwezo wao kiufahamu katika taaluma zao.

Lakini hii yote ni kutokana na mfumo wetu wa elimu ambao kwa miaka mingi umekuwa ukidumaza akili zetu.
Mara nyingi wadau mbalimbali wakiwemo baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakipiga kelele kuhusu haja ya Serikali kubadili mfumo wa elimu ili kuweza kuwashindanisha wasomi wake na wasomi wa nchi nyingine duniani lakini jambo hilo limeonekana kama vile halina maana.

Najua serikali kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi imeshawahi kubadili mitaala ya elimu mara kdhaa, lakini ninachojaribu kusema hapa ni je tabia ya wanafunzi kukariri ili wafaulu mitihani badala ya kuelewa imekomeshwa kwa kutafuta chanzo chake?

Ukweli ni kwamba, ni vigumu kwa wasomi wengi wa Tanzania kushindana kwenye soko la dunia kitaaluma kwa sababu, hawakuandaliwa kuwa watu wanaofahamu, bali wameandaliwa kuwa watu wanaokariri…

Hizi ni story, hearsay Bebu tuwekee takwimu kuhusu hiki kitu unasema!
 
Hao Madar na Maprof unaowaona feki idadi kubwa ndio wanaofundisha hata vyuo vya hao wenye elimu bora kwa kipindi cha miaka isiyopungua 20 chuo kikuu cha dar kimekuwepo ktk vyuo bora Africa na ndio chuo kilichokuana school of thought ya mlengo wa kiafrika. Ni miongoni mwavyuo vinavyofanya vizuri kaika utafiti na uandishi wa journals angalia tovuti na idadi ya research kwa mwaka huu.
 
Elimu itakuaje bora wakati viongozi na wanasiasa mashuhuri wana vyeti bandia au vya kugushi? Kila mwanasiasa anataka kuitwa dokta kwa kununua shahada bandia au ya kugushi. Udokta wa wengi unagunduliwa kwa kiwango chao cha chini cha ufahamu.
 
Zinduna
Nilivyokufahamu, unapiga kelele kwenye mfumo wa elimu TZ sio wasomi wa TZ, kwani umekubali kuwa wapo wasomi wanaofanyakazi huko majuu kutokana na elimu yao, sina uhakika kama wapo wasomi walioshindwa na kufanyakazi huko ulaya kwa kukosa maarifa na elimu, wengi wetu wa waTZ tuna nidhamu ya woga tunao ma phd kutokea kusini mwa dunia mpaka kaskazini ya dunia na ni wataalamu lakini sio wengi waliokaribu na waTZ ni watu waliojitenga sababu siijuwi
Kweli nakubaliana nawe kwenye soko la wasomi waTZ ni kidogo kulinganisha mahasimu wetu(Kenya)

Mfumo wetu wa elimu unadumaza sana kama walivyosema wachangiaji ni wa kuhariri zaidi kutokana na siasa yetu
 
Kwa jinsi mada inavyojadiliwa hapa hapa jamvini inajionesha picha halisi ya wasomi wetu hakuna kitu!!
Mtoa mada anasema wasomi wa kitanzania hawauziki na si watanzania waliosoma!! hawauziki!!! .Hana maana ya kukashifu msomi wa Tanzania bali anatoa picha halisi ni jinsi mfumo wa elimu yetu ulivyo wa kurundika vyeti zaidi kuliko maarifa!. Inawezekana kweli mtoa mada hana data za kujusty anachosema lakini kama kuna msomi anapinga si ni uungwana kuja na data za upande wa wasomi waliouzika !
Hatukatai kuna wasomi wengi tu huko nje wa kitanzania na wanafanya makubwa sana , fact is they had to execute a huge u turn kuelekea kwenye elimu iliyowapatia maarifa!
MAJI YAKIWA MEPESI KAMA HEWA ... SI MAJI TENA BALI NI HEWA ....... SHAABAN ROBERT
 
Waandishi wa vitabu wenyewe hakuna na kama wapo ni wale wa kukopi na kupesti na ndio maana vina makosa kibao kwa sababu ya lugha kugongana

Sasa kama hatuna uwezo wa kujenga hoja elimu ya kuandika vitabu inayotaka uwezo wa mtiririko wa mawazo utatokea wapi?
 
Viongozi wa kisiasa wasiokuwa makini pamoja na wengi wao kuwa wababaishaji ndio chanzo cha elimu yetu kuporomoka.
Mtu kama Mulugo ambaye imebainika kuwa kwenye elimu ni ''maimuna'' halafu ndiye amekabidhiwa dhima ya kuiongoza wizara ya elimu hapo tunategemea nini?
Wacha watu waendelee kupiga box tu hadi pale kwa pamoja tutakapoamua kuwaondoa madarakani wababaishaji wote na kuweka watu makini watakaolinda na kuzingatia maslahi mapana ya nchi na wananchi wake wote.
 
Hili Serikali imeliona na ndiyo sababu kwa sasa kuna kitu kinaitwa competence-based curriculum ambayo ni tofauti na ile ambayo ilikuwa teacher-centred. Tatizo ni kwamba bado walimu hawajaelewa jinsi ya kuimudu kwa hoyo bado wanafundisha wanafunzi past papers ili waweze kufaulu mitihani. Ila kama walimu watapata orientation hii hali itabadilika na hivyo kuwafanta Watz kuweze ku-compete kwenye soko la ajira au kuwa na ujuzi wa kujiajiri wenyewe.
Km maneno ya kweny ekanga vile..akili ndogo haiwezi jito aktk tope ,ilipojiingiza.huwezi jisukuma mwenyewe.Misamiati bongo ni mingi sana..Mojawap ni hii:
-TAMISEMI.
-BIOGAS.
-KILIMOKWANZA.
-BIG RESULT NOW.
N.k
 
Ukweli upo wazi...si tunawasikia ktk akina werema, maghembe, chenge etc....wanavyotolewa jasho na CDM hadi wanakuwa mbogo.
 
mkuu Wacha ukweli ni kwamba kuna changamoto nyingi sana hapa nyumbani,hivi una habar kuna watu wanamaliza form 6 na hadi university hawajui hata kutuma e-mail????tumesoma nao,,,,jaman data za nini???alichoandika Zinduna kina ukweli,hebu angalia avatar yangu hilo dawat ni la shule fulani hapa tanzania,ambayo hata kifaranga ana uwezo wa kupita ukutan na kuzama class


Kwa hiyo wewe mwenye afadhali unayeweza kutumia e-mail ndio unabandika post zako chijui mara ngapi? Na usomi wako wote hutaki tutumie data unachekesha sana ... .... ..... ....
 

Kwa hiyo wewe mwenye afadhali unayeweza kutumia e-mail ndio unabandika post zako chijui mara ngapi? Na usomi wako wote hutaki tutumie data unachekesha sana ... .... ..... ....

Wacha sijazungumzia usomi wangu,mimi nachosema ni kwamba hata kama Zinduna hajaja na data ila ukweli upo palepale,maana yake kwa mfano mdogo tu wa matumizi ya kompyuta msomi wa leo hawez,ina maana muajiri akishakupa kazi akupeleke kompyuta kozi???
Usisimamie kwenye data,,,liangalie hila jambo kwa uhalisia lipo au halipo,na kwa miaka ya karibun wameibuka wanafunz wetu wanaenda form I hawajui kusoma wala kuandika,na hawa kwa miaka ijayo utataka data kama hawauziki,,,,,
isije ikawa wewe ndo unachekesha bila kujijua,,,,,
 
Last edited by a moderator:
Asilimia kubwa ya wasomi wa kibongo wanauzika sana na wengi wanafanya vitu vyao katika nchi za US, UK, UAE , Canada na nyingine nyingi duniani tena wana vyeo vya juu. Hata baadhi ya waajiri kuwaomba Wabongo waliowaajiri kuwapendekeza Wabongo wengine kwa waajiri hao ili nao waajiriwe. Wabongo hao wengi wamejijengea sifa ya uchapakazi, uaminifu, uelewa mkubwa wa kazi zao, kutokuwa walalamikaji.
Lete ushaidi.
 
Ukienda UDSM kwa sasa kuna wasomi waliobobea ambao taasisi Na mashirika ya kimataifa hutumia Ujuzi wao. Mfano, Kama kuna Mtu alihudhuria international conference on oil and gas Mlimani city, kuna msomi Nathani kutoka idara ya political science alitoa mikakati Na mifumo ambayo Kama ikifuatwa Tanzania itamufaika sana Na rasilimali hizi. Mimi binafsi niliwasikia baadhi ya wenye makampuni ya mafuta wakisema kuwa huyo jamaa inabidi awe compromised maana mawazo yake yanaweza kuleta shida kwao. Hakika Tunao wasomi Nguli lakini je tunawatumia? By the way donors wote huwTumia Hawa Hawa kutubana. Sasa wafanyeje wakati wanahitaji kula
 
Najua kauli yangu hii itawakera wengi hususan hao wanaojiita wasomi, lakini najua kwamba ukweli mara nyingi huwa unauma sana.

Katika orodha ya nchi za Afrika ambazo wasomi wake wanaibwa na kusombwa na kupelekwa huko Ulaya na Marekani kufanya kazi , Tanzania haitajwi kabisa.

Watanzania wengi wanaokwenda nje kufanya kazi, ni vibarua zaidi, wenyewe wanajiita wabeba mabox, na hata kama ni wasomi, basi utawakuta wanafanya kazi ambazo huwezi kusema zitaweza kuisaidia nchi.

Hata hivyo wapo Watanzania wachache sana ambao wamenunuliwa nje na kufanya kazi huko kwa sababu ya uwezo wao kiufahamu katika taaluma zao.

Lakini hii yote ni kutokana na mfumo wetu wa elimu ambao kwa miaka mingi umekuwa ukidumaza akili zetu.
Mara nyingi wadau mbalimbali wakiwemo baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakipiga kelele kuhusu haja ya Serikali kubadili mfumo wa elimu ili kuweza kuwashindanisha wasomi wake na wasomi wa nchi nyingine duniani lakini jambo hilo limeonekana kama vile halina maana.

Najua serikali kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi imeshawahi kubadili mitaala ya elimu mara kdhaa, lakini ninachojaribu kusema hapa ni je tabia ya wanafunzi kukariri ili wafaulu mitihani badala ya kuelewa imekomeshwa kwa kutafuta chanzo chake?

Ukweli ni kwamba, ni vigumu kwa wasomi wengi wa Tanzania kushindana kwenye soko la dunia kitaaluma kwa sababu, hawakuandaliwa kuwa watu wanaofahamu, bali wameandaliwa kuwa watu wanaokariri…

Uko sahihi mia kwa mia!
 
Back
Top Bottom