Ukweli mchungu: Wasomi wetu hawauziki…!

Ukweli mchungu: Wasomi wetu hawauziki…!

Mkuu hatimaye nimepata Taarifa zake huyu Mzee wetu ndugu Erasto B Mpemba.Kumbe hakujiendeleza kwenye fani ya fizikia, baadae alisomea maswala ya wanyamapori na kufikia level ya shahada ya uzmili toka Texas na baadae akaajiriwa wizara ya utalii na mpaka kastaafia hapo.

tumblr_lv3x2gTxxh1r73aw3o1_400.png

TEDxDar Speaker
Erasto B. Mpemba
In 1963, Tanzanian Erasto B. Mpemba discovered a phenomenon that questions principles of established Newtonian physics – this phenomenon became (internationally) known as the "Mpemba effect." The Mpemba effect is the observation that under certain circumstances, warm water freezes faster than cold water. Mr. Mpemba made this discovery while in form 3 at Magamba Secondary School, and later collaborated with University of Dar es Salaam Professor Denis Osborne to publish theMpemba effect in a 1969 paper "Cool?" Although earlier allusions of the Mpemba effect were made by the likes of Aristotle, Francis Bacon, and Descartes, Mpemba's resolve to question conventional physics – with unadulterated curiosity – illuminated a phenomenon overlooked in popular physics.
After his groundbreaking work Mr. Mpemba went on to get a diploma from the College of African Wildlife Management in Moshi, completing further study in Natural Resource Management at the Canberra College of Advanced Education (now University of Canberra) in Australia, and a masters degree from Alpine, Texas, USA. He went on to become the Principal Game Officer in the Ministry of Natural Resources and Tourism in the Wildlife Division. He is now retired.
Duh, mimi nilifikiri aligundua hii kitu akiwa Mkwawa? Hili ndiyo tatizo kubwa tulilonalo Tanzania. Yaani kuna vipaji vizuri na vikubwa ambavyo kama vingeendelezwa vingefanya mambo makubwa na ya kutisha lakini hakuna ambaye huwa anavijali. Mtu kama huyu angekuwa kwenye nchi za wenzetu angepelekwa kwenye shule maalumu ili kumdevelop katika area aliyofanyia ugunduzi, lakini kwa Tanzania ameachwa tu.
 
Hili Serikali imeliona na ndiyo sababu kwa sasa kuna kitu kinaitwa competence-based curriculum ambayo ni tofauti na ile ambayo ilikuwa teacher-centred. Tatizo ni kwamba bado walimu hawajaelewa jinsi ya kuimudu kwa hoyo bado wanafundisha wanafunzi past papers ili waweze kufaulu mitihani. Ila kama walimu watapata orientation hii hali itabadilika na hivyo kuwafanta Watz kuweze ku-compete kwenye soko la ajira au kuwa na ujuzi wa kujiajiri wenyewe.
Hiyo competency based curriculum inafahamika theoretically lakini practically walimu hawaijui na wala hawaipractice kabisa. At your convenient jaribu kupitia hii article japo kiingereza chake hakijakaa vizuri;http://universalresearchjournals.org/ujegs/pdf/2012/December/Kafyulilo et al.pdf
Lakini kuna second version ambayo ni highly improved imeandikwa kwenye Makerere Journal of higher education, toleo la mwezi wa sita mwaka huu.
Na kwa utafiti ambao umefanyika mashuleni ambao upo mbioni kuwa published unaonyesha kwamba walimu wanaendelea na utaratibu wao wa kufundisha kwa njia zile za kawaida ambazo ni content-based, and teacher-based approach.
 
Kwa dhana ya mtoa mada hapa ni vyeti....
Mkuu Kipokola naomba kukusahihisha, naomba usome majibu yangu kwa Mentor kuhusu msomi ni nani, kisha tuanzie hapo

Mentor, Kwa mtazamo wangu msomi ni yule anayezalisha maarifa baada ya tafakari kubwa na ya muda mrefu. Mtu anayejiuliza maswali na kupata majibu ili aweze kuisaidia jamii hapa duniani.

Naomba nikutolee mfano wa Sophocles, na wale wasomi wa kwanza duniani. Hawa ndio tunaoweza kuwaita wasomi, kwa sababu utafiti wao unagusa kila eneo la maarifa bila kujali kama ni sayansi, biashara, tiba au sanaa.
 
Last edited by a moderator:
Najua kauli yangu hii itawakera wengi hususan hao wanaojiita wasomi, lakini najua kwamba ukweli mara nyingi huwa unauma sana.

Katika orodha ya nchi za Afrika ambazo wasomi wake wanaibwa na kusombwa na kupelekwa huko Ulaya na Marekani kufanya kazi , Tanzania haitajwi kabisa.

Watanzania wengi wanaokwenda nje kufanya kazi, ni vibarua zaidi, wenyewe wanajiita wabeba mabox, na hata kama ni wasomi, basi utawakuta wanafanya kazi ambazo huwezi kusema zitaweza kuisaidia nchi.

Hata hivyo wapo Watanzania wachache sana ambao wamenunuliwa nje na kufanya kazi huko kwa sababu ya uwezo wao kiufahamu katika taaluma zao.

Lakini hii yote ni kutokana na mfumo wetu wa elimu ambao kwa miaka mingi umekuwa ukidumaza akili zetu.
Mara nyingi wadau mbalimbali wakiwemo baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakipiga kelele kuhusu haja ya Serikali kubadili mfumo wa elimu ili kuweza kuwashindanisha wasomi wake na wasomi wa nchi nyingine duniani lakini jambo hilo limeonekana kama vile halina maana.

Najua serikali kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi imeshawahi kubadili mitaala ya elimu mara kdhaa, lakini ninachojaribu kusema hapa ni je tabia ya wanafunzi kukariri ili wafaulu mitihani badala ya kuelewa imekomeshwa kwa kutafuta chanzo chake?

Ukweli ni kwamba, ni vigumu kwa wasomi wengi wa Tanzania kushindana kwenye soko la dunia kitaaluma kwa sababu, hawakuandaliwa kuwa watu wanaofahamu, bali wameandaliwa kuwa watu wanaokariri…

u r dead wrong.....last time i checked you r telling how u r

pole....nimetembea nchi kibao na kote ni xprt
 
Kuna vijana wamemaliza f.4 mwaka jana walikuwa wakiomba kazi ya uhudumu kwangu niliwaliza swali moja tu!mto Ruvu uko mkoa gani na unamwaga maji wapi?wa kwanza akajibu upo Kigoma na unamwaga maji ziwa Tanganyika!wa pili akasema uko Ruvuma unamwaga maji katika bahari ya Atlantiki!Ila wote wamepata D ya Geography na wanalalamika eti wameonewa walikuwa wazuri wa somo hilo ambalo ndilo waliomba niwaulize maswali yake!Mh!nilishindwa kuamini nilichokuwa nasikia!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Tupeane pole maana ndio majanga tulionayo ndani ya Taifa letu huku tukiendelea kusifiwa kwa kuongeza idadi ya udahili na ufaulu wa standadizations.
 
Kwanza hata ma prof walio wengi ukiuatilia kwa makini utagundua wanakariri tu.Wapo wachache wanatambulika kimataifa kwa kazi zao kama Prof Shivji,prof mbele na wengineo.
 
Hivi wandugu kama mtu yuko Kigali, Rwanda naye tunasema yuko "nchi za nje"
tafsiri ya nchi za nje inabaki ni nchi za nje tu mkuu.distance btwn countries or continent is not the case.kama una ndg. au jamaa yako mtz anaishi rwanda,uganda,kenya...chukulia tu anaishi nje ya nchi.correct me if i'm wrong.
 
Najua kauli yangu hii itawakera wengi hususan hao wanaojiita wasomi, lakini najua kwamba ukweli mara nyingi huwa unauma sana.

Katika orodha ya nchi za Afrika ambazo wasomi wake wanaibwa na kusombwa na kupelekwa huko Ulaya na Marekani kufanya kazi , Tanzania haitajwi kabisa.

Watanzania wengi wanaokwenda nje kufanya kazi, ni vibarua zaidi, wenyewe wanajiita wabeba mabox, na hata kama ni wasomi, basi utawakuta wanafanya kazi ambazo huwezi kusema zitaweza kuisaidia nchi.

Hata hivyo wapo Watanzania wachache sana ambao wamenunuliwa nje na kufanya kazi huko kwa sababu ya uwezo wao kiufahamu katika taaluma zao.

Lakini hii yote ni kutokana na mfumo wetu wa elimu ambao kwa miaka mingi umekuwa ukidumaza akili zetu.
Mara nyingi wadau mbalimbali wakiwemo baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakipiga kelele kuhusu haja ya Serikali kubadili mfumo wa elimu ili kuweza kuwashindanisha wasomi wake na wasomi wa nchi nyingine duniani lakini jambo hilo limeonekana kama vile halina maana.

Najua serikali kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi imeshawahi kubadili mitaala ya elimu mara kdhaa, lakini ninachojaribu kusema hapa ni je tabia ya wanafunzi kukariri ili wafaulu mitihani badala ya kuelewa imekomeshwa kwa kutafuta chanzo chake?

Ukweli ni kwamba, ni vigumu kwa wasomi wengi wa Tanzania kushindana kwenye soko la dunia kitaaluma kwa sababu, hawakuandaliwa kuwa watu wanaofahamu, bali wameandaliwa kuwa watu wanaokariri…

Zinduna, sikubaliani sana na hoja yako kwa sababu hujaipatia ushahidi wa kutosha japo kuna baadhi ya facts ulizozitaja ambazo ni ukweli mtupu.

Ninachojua mimi, nchi nyingi za Kiafrika zinatuzidi katika kuzalisha idadi kubwa ya wasomi kiasi kwamba soko la ajira ktk nchi zao limejaa na hakuna namna nyingine zaidi ya kukimbilia nje. Na hili hatulioni kwa wasomi tu, bali katika nyanja zote za utafutaji maisha ikiwa ni pamoja na michezo, biashara, nk. Kwa hiyo kama unazungumzia kwa wingi unaweza kuwa sawa lakini kama ni ubora, tunahitaji ushahidi zaidi.

Kingine ambacho nimekishuhudia ni kuwa wasomi wa nchi nyingine hasa Kenya na Afrika Magharibi wanatabia ya kujikweza na kiherehere kiasi kwamba hata kama unamzidi ujuzi na maarifa lakini anaweza kuonekana yuko juu hasa kwa kuwa ni wajanja sana wa kutumia competitive advantage yao ambayo mara nyingi ni lugha ya kiingereza at the expense of other competencies. Kiingereza kwetu sio lugha ya mama maana tunatokea kwenye lguha zetu za makabila kisha tunapambana kujua kiswahili halafu baadae ndio tunakwenda kwenye Kiingereza wakati wenzetu wakitokea kwenye makabila yao wanaingia moja kwa moja kwenye kiingereza wakiwa bado na umri mdogo wa kuanzia shule.

Ushauri kwa Watanzania wenzangu, tusijiingize katka mkondo wa kujikatisha tamaa kuwa hatuwezi na tuko dhaifu hii si kweli, mimi nimeithibitisha kwa kufanya kazi na waTZ wenzangu kwa pamoja na watu wa mataifa mbalimbali ya Africa na kwingineko, ukiacha lugha sioni eti elimu yetu iko chini - labda ya siku hizi. Najua hii ni propaganda hasa ya nchi moja jirani ili wao wapate ajira zaidi, na huwezi wakiilenga nchi nyingine zaidi ya TZ.

Hata hivyo nitoe angalizo kuwa ukiangalia wasomi wetu wengi wa siku hizi ambapo vyuo vimekuwa vingi ipo haja kubwa ya kuwa makini na ubora wao wa sasa, japo hata huko nje pia kuna vyuo vya magumashi vingi tu. Serikali iwe makini na vyuo hivi vinavyoota kama uyoga ili kufanya ubora wa elimu usiwe compromised!
 
Wasomi wengi wa Tanzania hawana viwango ni wa hapa hapa tu.
 
Damn,we should look for him,put him in the Lab again he must have something to share with academics!
Mkuu hatimaye nimepata Taarifa zake huyu Mzee wetu ndugu Erasto B Mpemba.Kumbe hakujiendeleza kwenye fani ya fizikia, baadae alisomea maswala ya wanyamapori na kufikia level ya shahada ya uzmili toka Texas na baadae akaajiriwa wizara ya utalii na mpaka kastaafia hapo.

tumblr_lv3x2gTxxh1r73aw3o1_400.png

TEDxDar Speaker
Erasto B. Mpemba
In 1963, Tanzanian Erasto B. Mpemba discovered a phenomenon that questions principles of established Newtonian physics – this phenomenon became (internationally) known as the "Mpemba effect." The Mpemba effect is the observation that under certain circumstances, warm water freezes faster than cold water. Mr. Mpemba made this discovery while in form 3 at Magamba Secondary School, and later collaborated with University of Dar es Salaam Professor Denis Osborne to publish theMpemba effect in a 1969 paper "Cool?" Although earlier allusions of the Mpemba effect were made by the likes of Aristotle, Francis Bacon, and Descartes, Mpemba's resolve to question conventional physics – with unadulterated curiosity – illuminated a phenomenon overlooked in popular physics.
After his groundbreaking work Mr. Mpemba went on to get a diploma from the College of African Wildlife Management in Moshi, completing further study in Natural Resource Management at the Canberra College of Advanced Education (now University of Canberra) in Australia, and a masters degree from Alpine, Texas, USA. He went on to become the Principal Game Officer in the Ministry of Natural Resources and Tourism in the Wildlife Division. He is now retired.
 
Zinduna
Umesema kweli kabisa wasomi wa Tanzania hata kama wapo hawauziki kwenye soko la ajira,huyu kingmairo hana hoja anatoa povu tu hamna kitu,msomi kwenda nje ya nchi ni jitihada yako mwenyewe tunasumbuliwa na uoga wa kufikiri na kutokujiamini,wengine wanajiuliza akienda nje ya nchi atawasilianan na nani wakati lugha ya kuwasiliana hajui,anajua kiswahili tu?
Angalia mfano mdogo tu kwenye fb fungua alichoandika msomi ambaye anasema amegraduate UDSM,SAUT na vyuo vingine vya hapa nchini,wanavyoporomosha matusi,na ushauri wanaotoa hata mganga wa kienyeji ana nafuu halafu unajiuliza kwamba huyu ni msomi amekopeshwa kodi za wananchi ndie anaetoa matusi namna hiyo yaani hamna nafuu Tukubaliane tu kwamba Tanzania kuna baadhi ya wasomi hawauziki kama si wote ni bogus wataendelea kwenda kuwa maboi na wachambisha wazungu na pia wabeba maboksi kama akina Lukosi

Wasomi wetu ni taabu sana

Wewe ndo undhihirisha ulivyo mweupe kwanza kwa matumizi ya lugha yasiyo ya kistaarabu.Kila mtu ana haki ya kupembua kwa mtazamo wake na kusupport kwa hoja, Mie na wadau wengine tumeuliza maswali ya msingi ili muweze kuitetea hoja yenu mfano Je mnafahamu idadi ya watanzania wanaofanya kazi nje? Ni wasomi wangapi wameshindwa kuperform huko nje? Hilo la soko la ndani nimelitoa kwa mtazamo wa upande wa pili. Jibu hoja kwa hoja na usilete reference za kwenye facebook hapa. Kama wewe ni kijana wa kwenye facebook, peleka lugha zako huko huko. Hapa ni hoja kwa hoja
 
Jamani elimu yetu sasa hivi ni majanga. Ukikutana na mtu huko ughaibuni anapiga kazi ya uhakika ni M-TZ basi huyo atakuwa wa miaka ya early 90s kurudi nyuma! Sasa hivi watoto wetu unakuta jamaa kamaliza university lakini ukimwuliza hata habari ya Jiografia ya darasa la saba hajui. Juzi hapa nilikuwa nasaidia mtu mmoja kumchapia barua yake ya uhamisho akawa ameandika kwenye anwani yake P.O.BOX....KILOMBERO, nikamwambia hakuna makao makuu ya wilaya ambayo yanajulikana kwa jina hilo akabaki ananishangaa. Nikamweleza makao makuu ya wilaya ya Kilombero ni IFAKARA. Nikaendelea kumwelimisha barua zote zinatakiwa zisomeke P.O.BOX ...IFAKARA, KILOMBERO. Msomi wangu akanipiga swali ulishawahi kuishi IFAKARA? Enzi zetu tulikuwa tunashindana kujua makao makuu ya mikoa, wilaya, nchi n.k pia kujua makabila kwa kila mkoa. Sasa hivi hata mtoto wa TCU hajui haya!
 
Duh, mimi nilifikiri aligundua hii kitu akiwa Mkwawa? Hili ndiyo tatizo kubwa tulilonalo Tanzania. Yaani kuna vipaji vizuri na vikubwa ambavyo kama vingeendelezwa vingefanya mambo makubwa na ya kutisha lakini hakuna ambaye huwa anavijali. Mtu kama huyu angekuwa kwenye nchi za wenzetu angepelekwa kwenye shule maalumu ili kumdevelop katika area aliyofanyia ugunduzi, lakini kwa Tanzania ameachwa tu.

Tena cha ajabu mkuu, miaka ya hivi karibuni COSTECH wameanzisha utaratibu wa kuwa-award watafiti mbalimbali wakisayansi waliofanya makubwa nchini na kulipaisha jina la nchi yetu lakini si ajabu huyu mzee hajawahi hata kufikiriwa. Nchi hii inavichwa vikali sana lakini serikali ndiyo ya kipu.uzi haitaki kuwatumia wanajazana nafasi nyeti watu wasio na sifa kisa ni mtoto wa fulani. Kwa mwenendo huu maendeleo kwetu tutasubiri sana.
 
Sisi wa darasa la saba la wakati wa Nyerere ngoja huu uzi tuuache kwanza.
 
Kwa nini soko la ajira nje hasa Ulaya na Marekani? Kwani soko la ajira la ndani halihitaji na kustahili watu wenye ustadi na uwezo?

Mkuu hiyo ni changamoto tuliyonayo na ni maswali ya kujiuliza... hivi wewe ukiangalia viongozi wetu mfano: mtu kama Kova kwa kauli zake anastahili kuwa na nafasi aliyonayo??? na je unadhani chini yake hakuna wenye uwezo wa kutosha kushika ile nafasi??? ninachokiona si elimu tu ila na mfumo mzima wa utendaji wa nchi yetu ni mbovu:confused2:
 
Asilimia kubwa ya wasomi wa kibongo wanauzika sana na wengi wanafanya vitu vyao katika nchi za US, UK, UAE , Canada na nyingine nyingi duniani tena wana vyeo vya juu. Hata baadhi ya waajiri kuwaomba Wabongo waliowaajiri kuwapendekeza Wabongo wengine kwa waajiri hao ili nao waajiriwe. Wabongo hao wengi wamejijengea sifa ya uchapakazi, uaminifu, uelewa mkubwa wa kazi zao, kutokuwa walalamikaji.

Hao unaowataja hapa ni Watanzania ila sio wasomi wa Kitanzania. Kama kuna mtu kasomea - kwa mfano - USA au Australia na akapata cheo kikubwa au kazi nzuri huko huyo ni raia wa Tanzania ALIESOMEA NJE. Kwa mantiki hiyo huyo si msomi wa Kitanzania.
 
Back
Top Bottom