Ukweli mchungu: Wasomi wetu hawauziki…!

Ukweli mchungu: Wasomi wetu hawauziki…!

hapo anaongelea mfumo wa elimu, ya kwamba hautoi watu competent ambao wanaweza kushindana na jirani zetu kwenye soko la ajira nje hasa ulaya na USA nadhani ukilinganisha na nchi jirani kama kenya na uganda.

Mfumo wowote unaotegemea vyeti umeshindwa kabla haujaanza, kwa sababu nilizozieleza hapo juu.

Siku hizi mbona vyeti ni hela yako tu.
 
Hizo ni porojo tu, Mwanafunzi wa leo anayemaliza darasa la Saba mwambie ataje tu hata mikoa 5 ya tanzania na nchi walau 10 barani afrika kama atakwambia.
Badala ya kuitanua elimu tunazidi kuishusha na leo watoto wanasoma ramani za kata, wakifika sekondari hakuna mazoezi ya vitendo hata kidogo yanayopelekea watoto kuelewa bali ni ile ya kukariri na kuona majibu yanatoka yaliyoko katika vitabu na ikitokea vinginevyo hakuna anayeweza kuelezea.

Kuna vijana wamemaliza f.4 mwaka jana walikuwa wakiomba kazi ya uhudumu kwangu niliwaliza swali moja tu!mto Ruvu uko mkoa gani na unamwaga maji wapi?wa kwanza akajibu upo Kigoma na unamwaga maji ziwa Tanganyika!wa pili akasema uko Ruvuma unamwaga maji katika bahari ya Atlantiki!Ila wote wamepata D ya Geography na wanalalamika eti wameonewa walikuwa wazuri wa somo hilo ambalo ndilo waliomba niwaulize maswali yake!Mh!nilishindwa kuamini nilichokuwa nasikia!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
hapo anaongelea mfumo wa elimu, ya kwamba hautoi watu competent ambao wanaweza kushindana na jirani zetu kwenye soko la ajira nje hasa ulaya na USA nadhani ukilinganisha na nchi jirani kama kenya na uganda.

Kwa nini soko la ajira nje hasa Ulaya na Marekani? Kwani soko la ajira la ndani halihitaji na kustahili watu wenye ustadi na uwezo?
 
mimi naomba nianze kwa kuwataja wasomi ambao ninaajua na mambo wanayoyafanya nje ya nchi yetu.

Wa kwanza kabisa ni mwana jf mwenzetu ambaye yuko Marekani anafanya kazi na kampuni ya glaxo smith yeye ni mtaalam wa fluid micronization technique na sasayuko kwenye post doc.

wa pili nimemsahau jina lake halisi ila yeye yupo Kigali ndiye mtaalam wa biogas production huyu alikuwa ni mwanafunzi wa Dr. rubindamayugi na kwasasa Rwanda ndio nchi inayoongoza Africa kwa matuizi ya Biogas hapa Africa.

Mwingine ni huyu mwanamama Hulda Shaidi Swai huyu yeye ni Nanotechnologist anafanya na CSIR huko SA huyu anagroup ya wanasayansi zaid ya 100 huyu ndiye aliyegundua ANTI TB drug ambayo ni nanomedicine. Dawa hii imeshakuwa patented na soon itaingia sokoni. iko tofauti na dawa za TB za kawaida manake badala ya mtu kumeza dawa kama 60 hivi hapa anameza dawa 1 tu kila baada ya siku 4. kumbuka CSIR ni taasisi kubwa sanaa ambayo ni uti wa mgongo wa viwanda huko SA kwani wanazalisha malighafi nyingi sana kwajili ya viwanda vyao.

mwingine ni huyu aliayetengeneza BIOSENSORS huyu anaitwa Asanterabi Malima, yuko Boston marekani na ana fanyakazi na Biolom( hii ndiyo kampuni inayojihusisha na usambazaji wa biomakers na biosensors) lakini pia ni mwajiriwa wa Centre for High rate Nanomanufacturing (CHN) na anafanya post doc huko Northerneastern University.

haya mimi nimeamua kuwataja hawa wa4 ila ninaamini kwamba wapo wengine ambao watataja. Kimsingi kama kuna mtu anafanya kazi nzuri apewe sifa zake binafsi mie nawakubali sana hawa niliowataja manake ni majembe sana tu.
Mwalimu je unaweza kutueleza hao watu uliowataja walisomea wapi Degree zao kuanzia ya kwanza na ya pili na kadhalika. Je walisomea degree zote kutoka UDSM na taasisi zake? Nauliza just kuweka mambo sawa ili nami nijivunie kwa confidence mafanikio ya hao watanzania wenzangu.
 
Uzuri wa Watanzania hawajikwezi kama waganda na wakenya.

Are you serious?
Mataifa hayo hujikweza kwa watu wasio wa mataifa hayo.
Watanzania wanajikweza kwa watanzania wenzao. Na hawakubali wa chini yao wawe kama wao, watawanyima information, na hata kamsaada kadogo ambako kangeweza kuwanyanyua.
Mtanzania asili yake inaanzia hapohapo nyumbani TZ, akiwa kijiweni atahubiri mazuri sana lakini akiingia kwenye system anabadilika na anaanza kuwakandamiza aliowaacha chini.

Proof:
Angalia wabunge wetu kabla hawajawa wabunge walikuwa wanaongea nini halafu linganisha na wanachoongea baada ya kuwa mjengoni. Huu ni mfano mmoja tu, ipo mingi na mingine nina uhakika umeshakumbana nayo. TZ ipo hapo ilipo for a reason sio hivihivi tu.
Watanzania ni watu wa kujikwenza na wakandamizaji wa wenzao.
 
Habari za kusikitisha kupitia BLOG ya Vijimambo ni kuwa Mtanzania ameuwawa huko Washington DC alikuwa akisoma katika chuo cha Howard University
 
Mifano ni mingi ukienda kwenye taasisi za Utalii kama mahotelini na kwenye Bank zetu hapa nchini, nafasi nyingi za maana zimeshikwa na Wakenya na waganda na hivi sasa wapo waafrika Magharibi wanaoanza kuchangamkia ajira za hapa nchini na hata waajiri wanakiri kwamba hatuwezi na hata tukipewa nafasi hatuna ufanisi. Hivi sasa kila kampuni inatafuta faida hivi unafikiri bado kuna kubebana kama enzi za mashirika ya umma?

Zinduna, mtu amekesha miaka minne kupata degree yake halafu wewe useme hauziki, lazima atatoa povu.
Mimi nilisoma bongo na pia nikasoma ughaibuni, ni kweli kabisa nimeona tofauti kubwa mno kwenye ufundishaji na hata kwenye ku-update material na zana za kufundishia, n.k. Na hata jinsi unavyo gain na jinsi unavyokuwa na confidence ya kwenye kazi ni tofauti mno.

Kitu ambacho nimekiona ni kwamba elimu yetu imelalia kwenye kukariri zaidi kufaulu mitihani, na tuko vizuri sana kwenye kukariri.
Elimu yetu ikiongezewa upande wa pili ambao sio wa kukariri ambao ni ku introduce real world wa kile tunachosomea, tutakuwa mbali mno hata afrika nzima haitatukamata. Kitu ambacho nimekiona ni kuwa tanzania kuna vipaji vingi mno kuliko nchi nyingi za kiafrika, lakini vipaji hivyo vipo gizani havijapewa mwanga wa kustawi.
Kabla, nilikuwa nadhani ni umasikini ndio umetufanya tufike hapo tulipo lakini sababu halisi ni mfumo mbovu wa elimu, ambao wakuu wa nchi wanaufahamu lakini hawana mpango wa kuubadilisha kwa sababu watoto zao wanasoma overseas, na pesa za kuboresha elimu wanazipeleka wanakojua wao.
 
Bwana mdogo Lukosi ni mmoja kati ya Wahuni na wababaishaji.
Leo yuko kwenye tope kesho yuko kwenye maji, yeye hushamiri penye sinia la wali na nyama choma, mbaniko.
 
Enzi hizo tulizijua hadi nchi zinaitwa Vanuatu na Tuvalu....

But siku hizi Mulugo hajui hata Zimbabwe na Pemba ziko wapi halafu mnawalaumu graduates wa bongo kwa kushindwa kujiamini. Kansa kubwa kuliko zote kwenye elimu ya vyuo vikuu vya bongo ni wanafunzi kuangaliziana na kuingia na makaratasi yenye majibu, Mzumbe ndio wanaongoza ligi. Graduate asiyejiamini hata kujibu exams akaingia na majibu a.k.a MIG au akakaa kwenye mtandao wa kuangaliziana darasani hawezi kuongoza Portfolio hata $10,000.

Hii nchi CCM wameifikisha pabaya sana.
Na hapa ni funafuti internationa airport(tuvalu). Utakoma mwenyewe.

funafuti-international-airport_400_300.jpg
220px-Air_Force_Hercules_-_Flickr_-_NZ_Defence_Force.jpg
 
Watu wote wenye PhD ninao wafahamu wamesom first digree UDSM na baada ya hapo kuendelea na masomo nje ya nchi. Ni walimu wazoefu wa zaidi ya miaka kumi katika State Universities kibao.
Kaulize mahli popote ndani ya serikali ya CCM kama wanawajua, watakwmbia kila mtu huko majuu anabeba Box.
Hawa ni wasomi wetu ambao hawakusoma English Media a Kenya wala Uganda ni uzao wa elimu ile ya Bongo.

Wako wenye Masters za Engineering ambao walikuja hapa na vyeti vya a evel tu, hawa walikuwa A level Kibaha, Tosa Iliboru na kwingineko miaka ile ya 90 sasa hivi wapo hapa USA wanakula mzigo huku wakivuta pochi ya uhakika.

Yuko jamaa yangu yeye alikula Mzinga form 6 PCB lakini sasa hivi ni head wa hardware test department kwenye kampuni moja ya kutengeneza wireless divices. Alianza na associate digree ya Electrical engineering hadi Masters ya Eletrical Engineering.

kama Elimu yetu ni completely nyanya watu wangekuwa wakifika huku wabnabuma kishenzi.

Wanao buma na kutia aibu ni watoto wa Mafisadi wa CCM tu ambao pamoja na kulipiwa full ada ya shule wakienda shule wanaona maluelue hivyo wanaishia kuvaa milegezeo na kuvuta ganja.

Me naona hapa hata hamjamuelewa mleta mada ila nina imani alimanisha wasomi wetu ambao ni product ya mfumo wetu huu wa elimu wa tanzania.

Sasa tunaanza kuchambua watz sijui yuko nchi gani na wapi ila hebu tupeni background zao utakuta kasoma shule au chuo mbele huko huko... wewe niambie mtu typicall product of our education system anayefanya vizuri mbele kama si wabeba mabokis na ni wazi watz ni wachache wanaotoka nje ya nchi ukilinganisha na jirani zetu kenya na uganda.

Pia sis wenyew tunalalamika kila siku kuhusu wakenya na waganda wanachukua kazi zetu hapa nchini na pia wenzetu wakenya wamesambaa hata mpaka arabic world..tatizo letu kubwa ni mfumo wa elimu, lugha ya kufundishia,vitendea kazi na sifa hata za walimu wetu toka juu mpaka chini, alafu hatupendi kukosolewa.

Tukubali ya kwamba mfumo wetu ni tatizo toka primary mpaka chuo kikuu...tunadhalisha wasomi hewa wanajua kukariri tu na ndiyo maana wengi wetu wanasiasa maneno mengi kweli ila vitendo hafifu. angalia wachumi wetu wa first class kina Mwigulu ndo alikuwa BOT unadhani hapo kweli kuna kitu???? Prof.Lipumba anaongea ila alishakuwa mshauri wa mwinyi uchumi ila uliona madudu hakuwa na la maana ila hapo unaona bora ambao waliishia la nane kina Lyatonga Mrema wamefanya makubwa kwa taifa hili.
 
Elimu leo?

Elimu enzi zetu bwana, hadi khati unafundishwa kwa majina yake

Princess Margaret, Lady Victoria
 
Ukitaka kujua ukweli wa haya jifanye SEKI tu walau kwa dakika 10 katika primary yeyote utabaini ukweli wa hili.
Sitaki kukutafunia sana, this is just a clue kukupa hamasa ya kujionea.

Raha ya kitu utest mwenyewe sio uhadithiwe.

uko sahihi mkuu...tatizo nadhani hatuishi maisha yetu yalio katika mazingira yetu...watoto wetu wanalishwa habari nyingi kutoka magazeti radio tv mitandao ya kijamii zisizo na maana kwenye maisha...ujauzito wa Beyonce (mwanamuziki)inaweza kuwa ni habari kubwa inayojadiliwa na vijana wengi katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuliko rasimu ya katiba......na hata kama masuala yenye tija yakijadiliwa utagundua wengi hawajui hata wanachokijadili.....tumekata tamaa....tumewadharauwasomi na watalaam wetu......tumedharau mchango katika jamii....mjomba wangu mmoja ana elimu shahada ya uzamifu ni mtumishi wa serikali....lakini kila wakati namsikia akiomba msaada wa kifedha kwa baba yangu ambaye anaelimu ya msingi lakini ni diwani au huwa anaomba kwa mdogo wangu aliyeacha shule kwa sababu ya muziki wa bongofleva......hapo bado unadhani nitapokea kwa dhati kile ninachofundishwa kweli????
 
Wauzike je angali haijulikani ni mitaaka gani inafundishiwa mashuleni tena tangia shule za kata ndo hatari tupu
 
Jambo moja kubwa na mhimu sana ambalo hulijui kuhusu bongo, ni kwamba amani na utulivu, uzalendo na maisha yenye unafuu kidogo kwa bongo ndicho kinachowafanya wabongo wengi watamani kufanya kazi ndani ya nchi na hata kubaki nchini kwao.

Tofauti na hizo nchi nyingine unazozifia kama vile Kenya, Nigeria, Ethiopia, na nyinginezo nyingi ambazo zina matatizo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, kiasi cha kwamba watu wengi mara tu baada ya kuhitimu masomo yao hukimbilia nje ya nchi kwa ajili ya kutafuta kazi zenye unafuu. Lakini kwa ninavyoelewa kuna wabongo wengi sana wazuri sana academically na wenye uwezo mkubwa sana, waliogundua vitu vingi na vikubwa mno.

Tunazo Mbilinyi's principles of Economy ambazo ziligunduliwa na Professor mbilinyi, tuna Mpemba Effect ya kwenye Physics ambayo hivi sasa inatumiwa viwandani na kwenye sayansi za mambo ya maji, tuna biological research nyingi sana zinafanywa na watu wa botany pale UDSM na SUA zenye results ambazo hazijawahi kuwepo pengine popote duniani. Sasa utaonekana ni kituko unaposema Tanzania watu wamefundishwa kukariri.

Kwa taarifa yako elimu ya Tanzania ni mojawapo ya classic education katika Africa. Na hivi sasa elimu yetu tunaiuza sana tu. Maana katika universities zetu sasa hivi tunapokea wanafunzi kutoka mataifa mbalimbali duniani yakiwemo; Zambia, Botswana, Zimbabwe, Uganda, Kenya na hata Africa kusini.

Tuna changamoto kubwa tu ya mazingira na hasa accomodation kwa foreign students. Otherwise, naweza kusema we are the best. Suala la watanzania wangapi wapo nje kikazi hicho si kipimo cha uwezo wetu na elimu yetu. Maana uzalendo kwa nchi yetu ndiyo hasa sababu kubwa ya sisi kutokuwa nje ya nchi.


Mkuu nimetokewa kuvutiwa sana na ugunduzi wa huyu mtanzania wenzetu miaka hiyo ndugu Mpemba. Hivi unafahamu siku hizi yupo wapi huyu mtu na maisha yake briefly kama amefanyakazi wapi na amefaidika vipi na ugunduzi wake? Huko nyuma nilijaribu kumgoogle lakini nikaishia kumpata wikipaedia tu tena hawajaongelea maisha yake bali ni ugunduzi wake tu. Any Info about him please?
 
Mkuu nimetokewa kuvutiwa sana na ugunduzi wa huyu mtanzania wenzetu miaka hiyo ndugu Mpemba. Hivi unafahamu siku hizi yupo wapi huyu mtu na maisha yake briefly kama amefanyakazi wapi na amefaidika vipi na ugunduzi wake? Huko nyuma nilijaribu kumgoogle lakini nikaishia kumpata wikipaedia tu tena hawajaongelea maisha yake bali ni ugunduzi wake tu. Any Info about him please?
kwa bahati mbaya sana sijui huyu jamaa aliko. najua ugunduzi wake tu.
 
kwa bahati mbaya sana sijui huyu jamaa aliko. najua ugunduzi wake tu.


Mkuu hatimaye nimepata Taarifa zake huyu Mzee wetu ndugu Erasto B Mpemba.Kumbe hakujiendeleza kwenye fani ya fizikia, baadae alisomea maswala ya wanyamapori na kufikia level ya shahada ya uzmili toka Texas na baadae akaajiriwa wizara ya utalii na mpaka kastaafia hapo.


tumblr_lv3x2gTxxh1r73aw3o1_400.png



TEDxDar Speaker
Erasto B. Mpemba
In 1963, Tanzanian Erasto B. Mpemba discovered a phenomenon that questions principles of established Newtonian physics – this phenomenon became (internationally) known as the "Mpemba effect." The Mpemba effect is the observation that under certain circumstances, warm water freezes faster than cold water. Mr. Mpemba made this discovery while in form 3 at Magamba Secondary School, and later collaborated with University of Dar es Salaam Professor Denis Osborne to publish theMpemba effect in a 1969 paper "Cool?" Although earlier allusions of the Mpemba effect were made by the likes of Aristotle, Francis Bacon, and Descartes, Mpemba's resolve to question conventional physics – with unadulterated curiosity – illuminated a phenomenon overlooked in popular physics.
After his groundbreaking work Mr. Mpemba went on to get a diploma from the College of African Wildlife Management in Moshi, completing further study in Natural Resource Management at the Canberra College of Advanced Education (now University of Canberra) in Australia, and a masters degree from Alpine, Texas, USA. He went on to become the Principal Game Officer in the Ministry of Natural Resources and Tourism in the Wildlife Division. He is now retired.
 
Hili Serikali imeliona na ndiyo sababu kwa sasa kuna kitu kinaitwa competence-based curriculum ambayo ni tofauti na ile ambayo ilikuwa teacher-centred. Tatizo ni kwamba bado walimu hawajaelewa jinsi ya kuimudu kwa hoyo bado wanafundisha wanafunzi past papers ili waweze kufaulu mitihani. Ila kama walimu watapata orientation hii hali itabadilika na hivyo kuwafanta Watz kuweze ku-compete kwenye soko la ajira au kuwa na ujuzi
wa kujiajiri wenyewe.

Mara serikali imeliona halafu punde ooooonh walimu hawana orientation

Sasa hapo imeona kwa ku intrduce new sylabi ili watoto waelewe kwa osmosis???
 
Back
Top Bottom