Ukweli mchungu: Wasomi wetu hawauziki…!

Ukweli mchungu: Wasomi wetu hawauziki…!

we mleta maada ungeandika Wasomi niliopata kukutana nao hawauziki
 
Asilimia kubwa ya wasomi wa kibongo wanauzika sana na wengi wanafanya vitu vyao katika nchi za US, UK, UAE , Canada na nyingine nyingi duniani tena wana vyeo vya juu. Hata baadhi ya waajiri kuwaomba Wabongo waliowaajiri kuwapendekeza Wabongo wengine kwa waajiri hao ili nao waajiriwe. Wabongo hao wengi wamejijengea sifa ya uchapakazi, uaminifu, uelewa mkubwa wa kazi zao, kutokuwa walalamikaji.

Mmh.....haya we!!!!!!!!
 
Wacha sijazungumzia usomi wangu,mimi nachosema ni kwamba hata kama Zinduna hajaja na data ila ukweli upo palepale,maana yake kwa mfano mdogo tu wa matumizi ya kompyuta msomi wa leo hawez,ina maana muajiri akishakupa kazi akupeleke kompyuta kozi???
Usisimamie kwenye data,,,liangalie hila jambo kwa uhalisia lipo au halipo,na kwa miaka ya karibun wameibuka wanafunz wetu wanaenda form I hawajui kusoma wala kuandika,na hawa kwa miaka ijayo utataka data kama hawauziki,,,,,
isije ikawa wewe ndo unachekesha bila kujijua,,,,,

Wanafunzi wengi wa kitanzania wanafuata vyeti shuleni/vyuoni na sio KNOWLEDGE & SKILLS!!!!!!!!!!!!!!
 
hili hujalifanyia utafiti,wasomi wa kitanzania wanaheshimika sana nje ya nchi,watanzania wana tabia ya kutojikubali
 
Hawa wasomi ninaowazungumzia mimi ni wale ambao walizaliwa, kukulia na kusomea Tanzania mpaka degree yao ya kwanza. Baada ya hapo baadhi wakapata scholarships za Serikali kwa ajili ya Masters na labda Phd na wengine walizitafuta wenyewe kupitia balozi mbali mbali zilizo nchini. Kwa maoni yangu aliyezaliwa, kukulia na kusomea Tanzania kutoka shule ya msingi hadi 1st degree (katika vyuo vyetu nchini) ambayo ndiyo iliyomwezesha kupata scholarship nchi za nje kamwe huwezi kumtenga huyu kwamba si msomi wa Kitanzania.


That's precisely my point. Wewe umeamua kuwaita ni wasomi wa Kitanzania lakini ukweli ni kuwa kilichowapa hizo kazi SIO DEGREE (AU SECONDARY EDUCATION) ZA TANZANIA bali ni hiyo nyongeza ya elimu waliyoipata huko walikoipata - ambako si Tanzania. Nitajie mtu unaemfahamu ambae education qualifications zake zote ni za Tanzania na ambae amepata kazi hizo unazozitaja hapa.

Btw: Hata hizo admission za masters/PhD mara nyingi hazitolewi kwa kigezo cha elimu ya Tanzania pekee. Mara nyingi uki-submit first degree toka kwetu ili upate admission kwenye vyuo vya maana hasa watakulazimisha usome kozi kadhaa kabla hujawa admitted properly. This proves Zinduna's point in this thread.
 
Kinachoniudhi zaidi ni pale ninaposikia matangazo kwenye vyombo vya Habari kuwa kuna nafasi ya kusomea UALIMU kwa wenye DivIV 27,Form six kwa wenye Subs-jury pass 2 N.k Mimi hapo hasira kama ni TV au redio na switch OFF hadi hapo baadae na kama ni Gazeti nachana.Tangu lini mtu alishindwa akaandaa mtu wa kupata Div 1???????pleaseeeeeeeeee
LET CHANGE THIS!!!!!!! KWANZA ,mabadiliko mengine yafate
 
Hiyo definition yako ya yupi anayestahili kuitwa msomi wa Kitanzania mie siikubali. Huwezi kumuondoa Mtanzania aliyesoma Tanzania kwa miaka 16/17 katika kundi la wasomi wa Kitanzania eti kwa sababu Masters yake ya miaka miwili/mitatu (mitatu kama alirudia courses chache za 1st degree kwa mwaka mmoja). Yaani kwa kusoma nje miaka miwili a mitatu kama ni masters tu au miaka 7/8 pamoja na Phd basi ile miaka yake 17 iliyokuwa ni msingi mkubwa wa kwenda kusoma nje isiwe kigezo cha kumuona Mtanzania kama huyo ni msomi wa Kitanzania.

That's precisely my point. Wewe umeamua kuwaita ni wasomi wa Kitanzania lakini ukweli ni kuwa kilichowapa hizo kazi SIO DEGREE (AU SECONDARY EDUCATION) ZA TANZANIA bali ni hiyo nyongeza ya elimu waliyoipata huko walikoipata - ambako si Tanzania. Nitajie mtu unaemfahamu ambae education qualifications zake zote ni za Tanzania na ambae amepata kazi hizo unazozitaja hapa.

Btw: Hata hizo admission za masters/PhD mara nyingi hazitolewi kwa kigezo cha elimu ya Tanzania pekee. Mara nyingi uki-submit first degree toka kwetu ili upate admission kwenye vyuo vya maana hasa watakulazimisha usome kozi kadhaa kabla hujawa admitted properly. This proves Zinduna's point in this thread.
 
Hapo kwenye performance na vitendo tofauti yake nini?
Nyongeaza, Elimu ya tanzania inafundisha story za masomo tuyasomayo na ndi maana wengi wetu unaweza kuta performance yake ipo vizuri ila ukimpeleka kwenye vitendo hamna kitu.
 
Hakuna mtu anayemtaka aliyeshindwa akamwandae mtu kuweza kupata DVN 1.Mazingira ya kazi ya ualimu ndiyo yaliyowalazimisha mahitaji ya sifa hizo. Waliopata upper DVNs wanahitajika pia kwenye fani zingine zenye kuhitajika zaidi kwenye soko. Kwa maana zina mazingira mazuri, mishahara mizuri nk. Lakini la pili upo ushahidi wa kutosha wa kuwa waalimu wenye point hizo ndiyo hao hao wanafundisha wanafunzi wanaopata Dvn 1.Upo ushaihidi pia kuwa kufeli mtihani sio mara zote kutokuwa na maarifa (knowledge) Mtu anaweza kufaulu vizuri mtihani lakini asiwe na uwezo wa kuwafundisha wengine. Mipo mifano pia ya watu wanaopata Dvn 1, lakini ukimuuliza swali hilohilo katika stadi za maisha asiwe anajua kitu chochote na pengine akasema alisomea mtihani tu. Huku kitaaluma ya ualimu tunasema 'kujifunza kipurure'. Waalimu wengi walioko sekondari wanaotoa Dvns one ni wale unaowaona wewe kuwa hawakufaulu vizuri katika mitihani yao ya Form six lakini ndiyo hawo wanatoa wanachuo kwenda kusomea udaktari, uhandisi, uhasibu, uanasheria, nk leo ukisema tangu lini mtu aliyeshindwa akatoa Dvn one, mimi nitakuambia tangu kale
Kinachoniudhi zaidi ni pale ninaposikia matangazo kwenye vyombo vya Habari kuwa kuna nafasi ya kusomea UALIMU kwa wenye DivIV 27,Form six kwa wenye Subs-jury pass 2 N.k Mimi hapo hasira kama ni TV au redio na switch OFF hadi hapo baadae na kama ni Gazeti nachana.Tangu lini mtu alishindwa akaandaa mtu wa kupata Div 1???????pleaseeeeeeeeee
LET CHANGE THIS!!!!!!! KWANZA ,mabadiliko mengine yafate
 
Nyongeaza, Elimu ya tanzania inafundisha story za masomo tuyasomayo na ndi maana wengi wetu unaweza kuta performance yake ipo vizuri ila ukimpeleka kwenye vitendo hamna kitu.

Nakubaliana na wewe. Tusiikimmbilie takwimu za ufaulu bali tujiulize haowaliofaulu wanaweza kufanya nini?
 
BAK uko sahihi sana mkuu, yaani mimi ninamarafiki ambao wameajiriwa UK, USA, CANADA NA SA ambao kwanza utashangaa mambo wanayoyafanya. yaani mimi nilimshangaa mama mmoja anaitwa Hulda swai yaani ukiona team yako na jins alivyo excell utashangaa. ana run centre yenye watu zaid ya 100 ambao wanafanya kazi chini yake na wote wanaperform vizuri.

Nilisikitika sana alipoambiwa arudi Tz na mkuu wa nchi watu wakamtisha ukirudi Tz utafanyiwa majungu bora uendelee kujilia bata wako huko CSIR.
hapa kuna ukweli....
 
Kuna watu ni wa ------- sana,,,hivi mmeshabahatika kusoma syllabus ya kenya ama uganda,,we are far more better than them,,,kinachojalisha ni i.q yako na utendaji wa kazi plus morals,,na anayesema elimu yetu duni ni -------- kwani hakuna elimu bora kama yetu na ni copy and paste ya u.k sylabusses,,,eti wasomi wa tz hawauziki,nadhani hujawahi kwenda botswanna,malysia,u.sa,,,,,,
 
Najua kauli yangu hii itawakera wengi hususan hao wanaojiita wasomi, lakini najua kwamba ukweli mara nyingi huwa unauma sana.

Katika orodha ya nchi za Afrika ambazo wasomi wake wanaibwa na kusombwa na kupelekwa huko Ulaya na Marekani kufanya kazi , Tanzania haitajwi kabisa.

Watanzania wengi wanaokwenda nje kufanya kazi, ni vibarua zaidi, wenyewe wanajiita wabeba mabox, na hata kama ni wasomi, basi utawakuta wanafanya kazi ambazo huwezi kusema zitaweza kuisaidia nchi.

Hata hivyo wapo Watanzania wachache sana ambao wamenunuliwa nje na kufanya kazi huko kwa sababu ya uwezo wao kiufahamu katika taaluma zao.

Lakini hii yote ni kutokana na mfumo wetu wa elimu ambao kwa miaka mingi umekuwa ukidumaza akili zetu.
Mara nyingi wadau mbalimbali wakiwemo baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakipiga kelele kuhusu haja ya Serikali kubadili mfumo wa elimu ili kuweza kuwashindanisha wasomi wake na wasomi wa nchi nyingine duniani lakini jambo hilo limeonekana kama vile halina maana.

Najua serikali kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi imeshawahi kubadili mitaala ya elimu mara kdhaa, lakini ninachojaribu kusema hapa ni je tabia ya wanafunzi kukariri ili wafaulu mitihani badala ya kuelewa imekomeshwa kwa kutafuta chanzo chake?

Ukweli ni kwamba, ni vigumu kwa wasomi wengi wa Tanzania kushindana kwenye soko la dunia kitaaluma kwa sababu, hawakuandaliwa kuwa watu wanaofahamu, bali wameandaliwa kuwa watu wanaokariri…

Nikiwa primary (ambako ni msingi kabisa wa mwanafunzi) nilifundishwa kuwa Mtu wa kwanza kuona ziwa victoria ni mzungu (wakati wasukuma na wahaya wakiwa kando ya mto) na kilimo cha Ndizi Jamaica wakati wachaga na wahaya wakilima ndizi usiku na mchana.

Elimu ya kitanzania ya kutuandaa kutawaliwa hasa sasa kwenye ubepari unaoptia kwa lugha ya uwekezaji!
 
Wenzetu wako makini katika kupanga na kuchagua,huwezi kununua msomi ambaye anatoka katika nchi ambayo hainufaiki na wasomi wake,angalia mikataba mibovu na hao wanaoitwa wawekezaji,angalia mipango miji,kumbuka upasuaji wa kichwa badala ya goti,Maghorofa kuporomoka kabla ya kuisha,kununua vifaa duni vya kupimia Malaria hayo ni baadhi ya mambo yaliyowahi kufanywa na wasomi wetu!Kwa msingi/ historia hiyo,hata ungekuwa wewe ungeweza kununua kununua wasomi kama hao?
 
Wanafunzi wengi wa kitanzania wanafuata vyeti shuleni/vyuoni na sio KNOWLEDGE & SKILLS!!!!!!!!!!!!!!

No more words that what you have said MOSSAD II....And that brutal truth becomes like a thorn in the heart...it pains people. Instead of working towards improving ourselves, we come with all nonsense stories that please our laziness.
 
Wasomi wa nchi hii tujiulize mara mbili mbili nini kikubwa tunachofanya kupeleka gurudumu la maendeleo mbele? Au tunaendekeza kuchumia matumboni tu?
 
Back
Top Bottom