Jane kanunua kiwanja kabla ya ndoa na ameolewa 2008 ni kitambo kidogo so naelewa unachosema kuhusu thamani.
Ila sheria za umiliki zinasemaje? nani ni mmiliki, mwenye kiwanja au aliyejenga?
Enewei, Jane hakuandika jina lake kwenye hati, hata yeye si mmiliki bali msimamizi tu mpaka watoto watakapofikisha miaka 18 (usimamizi wake ulikua unaisha baada ya miaka 3, mtoto wao wa kwanza atakapofikisha miaka 18).
Ila nafikiri ile kasumba ya watoto ni wa mama, hata kama hati ikiwa kwenye jina la watoto bado mama atanufaika zaidi ndiyo ilimfanya Kweka asikubaliane na swala la kuandika majina ya watoto.