Chukulia context ya vitu vifuatavyo
1.Lugha
2.Chakula
3.Tamaduni mbalimbali
Hivi ni vitu ambavyo vinazaliwa na jamii
Mfano lugha nimekwambia mtu anazaliwa ana uwezo wa (1) kugundua lugha mpya ,kama hakuna lugha nyingine (2) ku adopt lugha anayo ikuta.
Same kwa dini, unazaliwa na hali ya ombwe lenye kukuambia kuwa wewe si kila kitu,kuna mamlaka ya juu zaid yako
Ukizaliwa mahali ambapo hilo ombwe wamelijaza na Yehova, na taratibu zake,unafundishwa hizo,ukizaliwa wamejaza hilo ombwe na Allah ,unabeba hilo ,same way to Mito,majabali etc etc inayopewa nafasi ya uungu.
Wazee wa kilimanjaro,walizaliwa na hilo ombwe,na wakakuta hakuna cha kuamini kuwa hiki ndo Mungu,wanaangalia hivi wanaona mlima mrefu,ambao wakitazama hawaoni mwisho wake,unatiririsha maji mazuri na unapendeza kuuona, wakaufanya ukawa Mungu wao.
Wahindi wao waligundua mto sindu ndo chanzo cha maji,chakula ,na chanzo cha ustawi wao,ukawa ndo Mungu.
So conclusion ni kuwa kama ambavyo tunatofautiana lugha,ni lazima tutofautiane na nini tumekipa nafasi ya uungu
Sababu hiyo inatokana na mazingira tofauti,
Unachozaliwa nacho ni uwezo wa kuongea na kubuni/ku adopt lugha na ombwe la kiroho linalohitaji kujazwa. Utalijaza na nini ? Inategemea na wewe umekuta nini na ku adopt nini au umegundua na kubuni nini.
Sent using
Jamii Forums mobile app