Ushahidi wa kutosha unaonyesha dini sio chanzo cha maadili ya dunia

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
61,008
Reaction score
100,956
Japo watu wengi wa dini huwa wanaamini dini ndiyo chanzo kikuu cha maadili duniani na kwamba dunia bila dini itageuka kuwa uwanja wa fujo ukweli wa historia unaonyesha tofauti kabisa.

Tukijikita katika dini kubwa tatu za Uyahudi, Ukristo na Uislamu zilizoanzia mashariki ya kati utagundua mambo makubwa maovu kinyume cha maadili ya ubinadamu yamefanyika chini yake kwa maagizo ya kidini, hayajakemewa au yameungwa mkono na hizi dini.

Tukianza na mifano michache utaona kwamba

Mauaji ya kimbari(genocide) yanapatikana katika agano la kale na quran. Hakuna maelezo ya kutosha kuelezea kwamba mambo haya ni sawa.

Utumwa(slavery) jambo baya zaidi kwa binadamu liliruhusiwa katika agano la kale na Quran pia. Huwa natatizika sana jinsi katika agano jipya la Biblia jinsi ambavyo watumwa(slaves) wanafundishwa kuwatii mabwana zao(slave masters)

Kuwatumia kingono wanawake mateka wa kivita ni jambo lililoruhusiwa katika agano la kale na quran pia.

Maandiko ya dini karibia zote hayaungi mkono demokrasia au haki za binadamu! Maandiko mengi yanatambua udikteta/uimla kama mfumo wa uongozi.

Linaweza kuwa bandiko refu sana nikizungumzia kuhusu crusades, ugaidi, ukoloni, ndoa za watoto wadogo, kurithi wake n.k

Kama dini zote kubwa mbili zisingeachana na baadhi ya maandiko katika vitabu vyao na kuzingatia kila andiko hakika duniani pasingekalika. Katika hili Wagalatia wamejitahidi sana kufanya reforms kubwa kwa kujikita katika agano jipya zaidi huku la kale wakichukua baadhi ya mambo mema tu.
 
Mzungu alisema: Little knowledge is a dangerous thing.

1) Demokrasia kwenye Ukristo.

YESU alikuja kuwainua wanawake wakati jamii nyingi zilikuwa haziheshimu wanawake.

"Wala hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume wala mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu."
Wagalatia.3.28.NENO

2) Mauaji ya kimbari.

Jamii zilizouawa hadi wanyama na watoto ni jamii zenye damu ya kinefili, pamoja na jamii zenye tamaduni ovu kabisa kama kutoa kafara watoto. Na hawakuwapenda Waisraeli, wakigundua Waisraeli wako karibu wanaenda kuwashambulia.

i)
"Mtakapoingia katika nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa, msijifunze kuiga njia za machukizo za mataifa ya huko.

Asionekane mtu yeyote miongoni mwenu ampitishaye mwanawe au binti yake katika moto, atakayefanya uaguzi, ulozi, anayetabiri nyakati, anayejishughulisha na uchawi,

wala arogaye kwa kupiga mafundo, wala mwaguzi au anayeabudu mizimu, wala awaombaye wafu.

Mtu yeyote afanyaye mambo haya ni chukizo kwa Bwana, tena ni kwa sababu ya matendo haya ya kuchukiza wayafanyayo ndiyo maana Bwana Mungu wenu atayafukuza mataifa hayo mbele yenu.

Kumbukumbu.18.9-12.NENO

ii)
"Wakati huo Yoshua akaenda kuwaangamiza Waanaki kutoka nchi ya vilima: kuanzia Hebroni, Debiri na Anabu, na kutoka nchi yote ya vilima ya Yuda na kutoka nchi yote ya vilima ya Israeli. Yoshua akawaangamiza kabisa pamoja na miji yao.

Hawakubaki Waanaki wowote katika nchi ya Israeli, ila tu katika nchi ya Gaza, Gathi na Ashdodi."

Yoshua.11.22-22.NEN

"Wakasema, “Nchi tuliyoipeleleza hula watu waishio ndani yake. Watu wote tuliowaona huko ni majitu.

Tuliwaona Wanefili huko (wazao wa Anaki wanatokana na Wanefili.) Tulijiona kama panzi machoni petu wenyewe, nao ndivyo walivyotuona.”

Ndipo Waamaleki na Wakanaani walioishi katika hiyo nchi ya vilima wakateremka na kuwashambulia, wakawapiga njia yote hadi Horma."

Hesabu 13:32b-33, 14:45 NEN

3) MUNGU amekataza kubaka. Kubaka kumefananishwa na kuua.

"Lakini ikiwa itatokea mwanaume akakutana na msichana aliyeposwa huko mashambani, akambaka, mwanaume aliyefanya hivi peke yake ndiye atakayeuawa.

Usimtendee msichana yule jambo lolote; hajafanya dhambi inayostahili kifo. Shauri hili ni kama lile la yeyote ambaye anamshambulia na kumuua kwa makusudi jirani yake"

Kumbukumbu.22.25-26.NENO

4) Sio tu kubaka, amekataza kushawishi / kurubuni wasichana.

"Mtu akimshawishi bikira ambaye hajaposwa na akalala naye, lazima alipe mahari, kisha atamwoa msichana huyo."
Kutoka.22.16.NENO

5) Wanawake waliochukuliwa kutoka vitani hawakubakwa.

Baada ya kuwachukua walipaswa kujitenga nao, wajitakase na mateka wajitakase.

Wanaume waliambiwa wawaache waishi na wanaweza kuwachukua kama wake, sio wawalazimishe, otherwise wangekuwa wanavunja sheria inayokata kubaka.

"lakini mwacheni hai kwa ajili yenu kila msichana ambaye hajawahi kulala na mwanaume.

Ninyi nyote ambao mmeua mtu yeyote au kumgusa mtu ambaye ameuawa, lazima mkae nje ya kambi kwa muda wa siku saba. Katika siku ya tatu na ya saba lazima mjitakase wenyewe pamoja na wafungwa wenu."

Hesabu.31.18-19.NENO

6) Maelezo mengine kuhusi mauaji ya kimbari:

Kwenye 1 Samweli 15:3, Mungu anamuamuru Mfalme Sauli “awaangamize kabisa” Waamaleki na kuwaua watoto wao pamoja na mifugo yao.

Wasomi kadhaa wameeleza kuwa neno lililotafsiriwa “kuwaangamiza kabisa” mara nyingi
halimaanishi mauaji ya kimbari ya kihalisi.

Badala yake linaweza kumaanisha kuangamiza utambulisho wa kitamaduni wa kundi fulani.

Wakanaani walikuwa na desturi ya kutoa kafara watoto wao kwa sanamu, kati ya matendo mengine ya kutisha.

Waisraeli mara nyingi waliamriwa kuharibu sanamu na vitu vitakatifu vya Wakanaani.

John Walton kwenye kitabu chake The Lost World of the Israelite Conquest, anaeleza kuwa katika visa vingi vinavyochukuliwa kuwa mauaji ya kimbari, Waisraeli walikuwa wanatekeleza "
herem" dhidi ya makabila mengine: yaani kuangamiza miungu yao na mifumo yao ya kidini, badala ya kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wenyewe.

Mfano ni kwenye Kumbukumbu la Torati 7. Mungu anawaamuru Waisraeli kuyaharibu (herem) mataifa yaliyokuwa yanaishi Kanaani.

Mistari inayofuata inaeleza wazi kwamba agizo hilo lilihusu kuvunja madhabahu yao na kuharibu nguzo za Ashera, si kuua watu wote.

Mfano mwingine
kwenye Kumbukumbu la Torati 20:17, Mungu anaamuru Waisraeli kuwaangamiza wakazi wote wa Kanaani.

Lakino ukisoma sehemu nyingine za Taurati, inaonekana kwamba Mungu hakuwa na tatizo na watu hawa kuendelea kuishi, na hata aliwaamuru Waisraeli kuwatendea wageni kama wao wenyewe:

"Wakati mgeni anaishi pamoja nawe katika nchi yako, usimnyanyase.

Mgeni anayeishi pamoja nawe ni lazima umtendee kama mmoja wa wazawa wa nchi yako. Mpende kama unavyojipenda mwenyewe, kwa maana ulikuwa mgeni katika nchi ya Misri. Mimi ndimi Bwana Mungu wako."

Walawi.19.33-34.NENO

Kwa hiyo, Biblia
haizungumzii mauaji ya kimbari ya Wakanaani kwa maana ya kuwaua kabisa, bali inaelekeza zaidi kwenye kuangamiza desturi na mifumo yao ya kidini na kitamaduni.

7) Utumwa

Utumwa kwenye Biblia sio utumwa huu tunaojua wa kukandamiza na kuonea watu.

Utumwa kwenye Biblia hauna tofauti na ajira leo hii, ndomaana mnaitwa Watumishi.

a) Mtu hakupaswa kuchukuliwa kinguvu na kufanywa mtumwa. Adhabu ya mtu anayefanya hivi ni kifo. Kwahiyo mpaka hapa tuna uhakika MUNGU hakuunga mkono utumwa tunaoujua.

"Yeyote anayemteka nyara mwingine akamuuza au akamweka kwake, akikamatwa ni lazima auawe."
Kutoka.21.16.NENO

b) MUNGU alikataza kuonea na kudhulumu watu, hata wageni / watumwa.

i) "Usimwonee mtu maskini na mhitaji ambaye umemwajiri, akiwa ni nduguyo Mwisraeli au mgeni anayeishi katika mojawapo ya miji yenu.

Mlipe ujira wake kila siku kabla ya jua kutua, kwa sababu yeye ni maskini na anautegemea ujira huo. La sivyo, anaweza kumlilia Bwana dhidi yako, nawe ukapata hatia ya dhambi."

Kumbukumbu.24.14-15.NENO

i)
"Usimtendee mgeni vibaya au kumdhulumu, kwa kuwa nanyi mlikuwa wageni huko Misri.

“Usimdhulumu mjane wala yatima.

Ukifanya hivyo nao wakinililia, hakika nitasikia kilio chao.

Hasira yangu itawaka, nami nitawaua kwa upanga, wake zenu watakuwa wajane na watoto wenu watakuwa yatima."

Kutoka.22.21-24.NENO

c) Utumwa ulikuwa makubaliano, hasa ili kulipa deni.

Watumwa wa kiyahudi wamepewa muongozo kabisa wa muda wa kazi. Watumwa wa kigeni ni wazi ingekuwa makubaliano yao na mabosi zao maana ni kosa kuwalazimisha.

i)Ukimnunua mtumwa Mwebrania, atakutumikia kwa miaka sita. Lakini katika mwaka wa saba, atakuwa huru naye ataenda zake pasipo kulipa chochote."
Kutoka.21.2-3.NENO

ii)
"Kama Mwebrania mwenzako, mwanaume au mwanamke, akijiuza kwako na kukutumikia miaka sita, katika mwaka wa saba ni lazima umwache aende zake akiwa huru.

Nawe wakati utakapomwachia usimwache aende mikono mitupu."

Kumbukumbu.15.12-13.NENO

d) Watumwa waliokimbia kutoka nchi zingine walipaswa kupokelewa vuzuri na waisraeli. Labda walikuwa wanateswa huko. Wakija Israeli wanakuja nyumbani.

"Ikiwa mtumwa amekimbilia kwako, usimrudishe kwa bwana wake.

Mwache aishi miongoni mwenu mahali popote anapopapenda na katika mji wowote anaochagua. Usimdhulumu."

Kumbukumbu.23.15-16.NENO

e) Atakayempiga akamuumiza mtumwa, mtumwa anakuwa huru kutoka hapo hata kama muda wa kuondoka haujafika.

“Mtu akimpiga mtumwa wa kiume au wa kike kwenye jicho na kuliharibu, ni lazima amwache huru yule mtumwa kama fidia ya hilo jicho.

Akimvunja jino mtumwa wa kiume au wa kike, ni lazima amwache huru huyo mtumwa kwa kufidia hilo jino."

Kutoka. 21.26-27.NENO

f) Atakayeua mtumwa wake ataadhibiwa. Damu kwa kwa damu. Mtumwa asipokufa hatoadhibiwa lakini tumeona mtumwa anakuwa hutu kuondoka akitaka.

"Mtu akimpiga mtumwa wake wa kiume au wa kike kwa fimbo na mtumwa huyo akafa papo hapo, ni lazima aadhibiwe,

lakini ikiwa mtumwa ataamka baada ya siku moja au mbili, hataadhibiwa, kwa sababu yule mtumwa ni mali yake."

Kutoka.21.20-21.NENO

g) Mabosi wakristo wanaagizwa watendee watumwa wao / wafanyakazi wao / watumishi kwa haki.

"Ninyi mabwana, watendeeni watumwa wenu yaliyo haki na yanayostahili, mkitambua kwamba ninyi pia mnaye Bwana mbinguni."
Wakolosai.4.1.NENO

h) Utumwa kwenye biblia hauna ubaguzi wa rangi, taifa, kabila. Wote waisraeli na wasio wasiraeli walikuwa watumwa. Utumwa wa kutesa tunaojua ulikuwa ni ubaguzi kwa binadamu wengine.

8) Kuna ile sheria ya mwanamke kutogusa kitu akiwa kwenye hedhi.

Watu wanasema wanawake wanaonewa!

Wanawake wangapi leo wakiambiwa kwa siku 7 na zaidi ikibidi kila mwezi watakuwa wanapewa OFF wasifanye kitu chochote wakae kama
Malkia, watasema wanaonewa? ? ?

"Ikiwa mwanamke atatokwa na damu ya kawaida ya mwezi, atakuwa najisi kwa siku saba, na yeyote atakayemgusa atakuwa najisi hadi jioni.

Ikiwa mwanamke atatokwa na damu kwa siku nyingi zaidi ya siku zake za mwezi, au amekuwa na damu inayoendelea zaidi ya kipindi chake, atakuwa najisi kwa kipindi chote cha shida hiyo, kama ilivyokuwa katika siku za hedhi yake."

Walawi.15.19-25.NENO

OUR GOD YAHWEH IS GOOD.

HIS LAWS ARE GOOD.

PRAISE THE LORD!
 
Mzungu alisema: Little knowledge is a dangerous thing.

1) Demokrasia kwenye Ukristo.

YESU alikuja kuwainua wanawake wakati jamii nyingi zilikuwa haziheshimu wanawake.

"Wala hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume wala mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu."
Wagalatia.3.28.NENO

2) Mauaji ya kimbari.

Jamii zilizouawa hadi wanyama na watoto ni jamii zenye damu ya kinefili, pamoja na jamii zenye tamaduni ovu kabisa kama kutoa kafara watoto. Na hawakuwapenda Waisraeli, wakigundua Waisraeli wako karibu wanaenda kuwashambulia.

i)
"Mtakapoingia katika nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa, msijifunze kuiga njia za machukizo za mataifa ya huko.

Asionekane mtu yeyote miongoni mwenu ampitishaye mwanawe au binti yake katika moto, atakayefanya uaguzi, ulozi, anayetabiri nyakati, anayejishughulisha na uchawi,

wala arogaye kwa kupiga mafundo, wala mwaguzi au anayeabudu mizimu, wala awaombaye wafu.

Mtu yeyote afanyaye mambo haya ni chukizo kwa Bwana, tena ni kwa sababu ya matendo haya ya kuchukiza wayafanyayo ndiyo maana Bwana Mungu wenu atayafukuza mataifa hayo mbele yenu.

Kumbukumbu.18.9-12.NENO

ii)
"Wakati huo Yoshua akaenda kuwaangamiza Waanaki kutoka nchi ya vilima: kuanzia Hebroni, Debiri na Anabu, na kutoka nchi yote ya vilima ya Yuda na kutoka nchi yote ya vilima ya Israeli. Yoshua akawaangamiza kabisa pamoja na miji yao.

Hawakubaki Waanaki wowote katika nchi ya Israeli, ila tu katika nchi ya Gaza, Gathi na Ashdodi."

Yoshua.11.22-22.NEN

"Wakasema, “Nchi tuliyoipeleleza hula watu waishio ndani yake. Watu wote tuliowaona huko ni majitu.

Tuliwaona Wanefili huko (wazao wa Anaki wanatokana na Wanefili.) Tulijiona kama panzi machoni petu wenyewe, nao ndivyo walivyotuona.”

Ndipo Waamaleki na Wakanaani walioishi katika hiyo nchi ya vilima wakateremka na kuwashambulia, wakawapiga njia yote hadi Horma."

Hesabu 13:32b-33, 14:45 NEN

3) MUNGU amekataza kubaka. Kubaka kumefananishwa na kuua.

"Lakini ikiwa itatokea mwanaume akakutana na msichana aliyeposwa huko mashambani, akambaka, mwanaume aliyefanya hivi peke yake ndiye atakayeuawa.

Usimtendee msichana yule jambo lolote; hajafanya dhambi inayostahili kifo. Shauri hili ni kama lile la yeyote ambaye anamshambulia na kumuua kwa makusudi jirani yake"

Kumbukumbu.22.25-26.NENO

4) Sio tu kubaka, amekataza kushawishi / kurubuni wasichana.

"
Mtu akimshawishi bikira ambaye hajaposwa na akalala naye, lazima alipe mahari, kisha atamwoa msichana huyo."
Kutoka.22.16.NENO

5) Wanawake waliochukuliwa kutoka vitani hawakubakwa.

Baada ya kuwachukua walipaswa kujitenga nao, wajitakase na mateka wajitakase.

Wanaume waliambiwa wawaache waishi na wanaweza kuwachukua kama wake, sio wawalazimishe, otherwise wangekuwa wanavunja sheria inayokata kubaka.

"lakini mwacheni hai kwa ajili yenu kila msichana ambaye hajawahi kulala na mwanaume.

Ninyi nyote ambao mmeua mtu yeyote au kumgusa mtu ambaye ameuawa, lazima mkae nje ya kambi kwa muda wa siku saba. Katika siku ya tatu na ya saba lazima mjitakase wenyewe pamoja na wafungwa wenu."

Hesabu.31.18-19.NENO

6) Maelezo mengine kuhusi mauaji ya kimbari:

Kwenye 1 Samweli 15:3, Mungu anamuamuru Mfalme Sauli “awaangamize kabisa” Waamaleki na kuwaua watoto wao pamoja na mifugo yao.

Wasomi kadhaa wameeleza kuwa neno lililotafsiriwa “kuwaangamiza kabisa” mara nyingi
halimaanishi mauaji ya kimbari ya kihalisi.

Badala yake linaweza kumaanisha kuangamiza utambulisho wa kitamaduni wa kundi fulani.

Wakanaani walikuwa na desturi ya kutoa kafara watoto wao kwa sanamu, kati ya matendo mengine ya kutisha.

Waisraeli mara nyingi waliamriwa kuharibu sanamu na vitu vitakatifu vya Wakanaani.

John Walton kwenye kitabu chake The Lost World of the Israelite Conquest, anaeleza kuwa katika visa vingi vinavyochukuliwa kuwa mauaji ya kimbari, Waisraeli walikuwa wanatekeleza "
herem" dhidi ya makabila mengine: yaani kuangamiza miungu yao na mifumo yao ya kidini, badala ya kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wenyewe.

Mfano ni kwenye Kumbukumbu la Torati 7. Mungu anawaamuru Waisraeli kuyaharibu (herem) mataifa yaliyokuwa yanaishi Kanaani.

Mistari inayofuata inaeleza wazi kwamba agizo hilo lilihusu kuvunja madhabahu yao na kuharibu nguzo za Ashera, si kuua watu wote.

Mfano mwingine
kwenye Kumbukumbu la Torati 20:17, Mungu anaamuru Waisraeli kuwaangamiza wakazi wote wa Kanaani.

Lakino ukisoma sehemu nyingine za Taurati, inaonekana kwamba Mungu hakuwa na tatizo na watu hawa kuendelea kuishi, na hata aliwaamuru Waisraeli kuwatendea wageni kama wao wenyewe:

"Wakati mgeni anaishi pamoja nawe katika nchi yako, usimnyanyase.

Mgeni anayeishi pamoja nawe ni lazima umtendee kama mmoja wa wazawa wa nchi yako. Mpende kama unavyojipenda mwenyewe, kwa maana ulikuwa mgeni katika nchi ya Misri. Mimi ndimi Bwana Mungu wako."

Walawi.19.33-34.NENO

Kwa hiyo, Biblia
haizungumzii mauaji ya kimbari ya Wakanaani kwa maana ya kuwaua kabisa, bali inaelekeza zaidi kwenye kuangamiza desturi na mifumo yao ya kidini na kitamaduni.

7) Utumwa

Utumwa kwenye Biblia sio utumwa huu tunaojua wa kukandamiza na kuonea watu.

Utumwa kwenye Biblia hauna tofauti na ajira leo hii, ndomaana mnaitwa Watumishi.

a) Mtu hakupaswa kuchukuliwa kinguvu na kufanywa mtumwa. Adhabu ya mtu anayefanya hivi ni kifo. Kwahiyo mpaka hapa tuna uhakika MUNGU hakuunda mkono utumwa tunaoujua.

"Yeyote anayemteka nyara mwingine akamuuza au akamweka kwake, akikamatwa ni lazima auawe."
Kutoka.21.16.NENO

b) MUNGU alikataza kuonea na kudhulumu watu, hata wageni / watumwa.

i)
"Usimwonee mtu maskini na mhitaji ambaye umemwajiri, akiwa ni nduguyo Mwisraeli au mgeni anayeishi katika mojawapo ya miji yenu.

Mlipe ujira wake kila siku kabla ya jua kutua, kwa sababu yeye ni maskini na anautegemea ujira huo. La sivyo, anaweza kumlilia Bwana dhidi yako, nawe ukapata hatia ya dhambi."

Kumbukumbu.24.14-15.NENO

i)
"Usimtendee mgeni vibaya au kumdhulumu, kwa kuwa nanyi mlikuwa wageni huko Misri.

“Usimdhulumu mjane wala yatima.

Ukifanya hivyo nao wakinililia, hakika nitasikia kilio chao.

Hasira yangu itawaka, nami nitawaua kwa upanga, wake zenu watakuwa wajane na watoto wenu watakuwa yatima."

Kutoka.22.21-24.NENO

c) Utumwa ulikuwa makubaliano, hasa ili kulipa deni.

Watumwa wa kiyahudi wamepewa muongozo kabisa wa muda wa kazi. Watumwa wa kigeni ni wazi ingekuwa makubaliano yao na mabosi zao maana ni kosa kuwalazimisha.

i)
Ukimnunua mtumwa Mwebrania, atakutumikia kwa miaka sita. Lakini katika mwaka wa saba, atakuwa huru naye ataenda zake pasipo kulipa chochote."
Kutoka.21.2-3.NENO

ii)
"Kama Mwebrania mwenzako, mwanaume au mwanamke, akijiuza kwako na kukutumikia miaka sita, katika mwaka wa saba ni lazima umwache aende zake akiwa huru.

Nawe wakati utakapomwachia usimwache aende mikono mitupu."

Kumbukumbu.15.12-13.NENO

d) Watumwa waliokimbia kutoka nchi zingine walipaswa kupokelewa vuzuri na waisraeli. Labda walikuwa wanateswa huko. Wakija Israeli wanakuja nyumbani.

"Ikiwa mtumwa amekimbilia kwako, usimrudishe kwa bwana wake.

Mwache aishi miongoni mwenu mahali popote anapopapenda na katika mji wowote anaochagua. Usimdhulumu."

Kumbukumbu.23.15-16.NENO

e) Atakayempiga akamuumiza mtumwa, mtumwa anakuwa huru kutoka hapo hata kama muda wa kuondoka haujafika.

“Mtu akimpiga mtumwa wa kiume au wa kike kwenye jicho na kuliharibu, ni lazima amwache huru yule mtumwa kama fidia ya hilo jicho.

Akimvunja jino mtumwa wa kiume au wa kike, ni lazima amwache huru huyo mtumwa kwa kufidia hilo jino."

Kutoka. 21.26-27.NENO

f) Atakayeua mtumwa wake ataadhibiwa. Damu kwa kwa damu. Mtumwa asipokufa hatoadhibiwa lakini tumeona mtumwa anakuwa hutu kuondoka akitaka.

"Mtu akimpiga mtumwa wake wa kiume au wa kike kwa fimbo na mtumwa huyo akafa papo hapo, ni lazima aadhibiwe,

lakini ikiwa mtumwa ataamka baada ya siku moja au mbili, hataadhibiwa, kwa sababu yule mtumwa ni mali yake."

Kutoka.21.20-21.NENO

g) Mabosi wakristo wanaagizwa watendee watumwa wao / wafanyakazi wao / watumishi kwa haki.

"Ninyi mabwana, watendeeni watumwa wenu yaliyo haki na yanayostahili, mkitambua kwamba ninyi pia mnaye Bwana mbinguni."
Wakolosai.4.1.NENO

h) Utumwa kwenye biblia hauna ubaguzi wa rangi, taifa, kabila. Wote waisraeli na wasio wasiraeli walikuwa watumwa. Utumwa wa kutesa tunaojua ulikuwa ni ubaguzi kwa binadamu wengine.

7) Kuna ile sheria ya mwanamke kutogusa kitu akiwa kwenye hedhi.

Watu wanasema wanawake wanaonewa!

Wanawake wangapi leo wakiambiwa kwa siku 7 na zaidi ikibidi kila mwezi watakuwa wanapewa OFF wasifanye kitu chochote wakae kama
Malkia, watasema wanaonewa? ? ?

"Ikiwa mwanamke atatokwa na damu ya kawaida ya mwezi, atakuwa najisi kwa siku saba, na yeyote atakayemgusa atakuwa najisi hadi jioni.

Ikiwa mwanamke atatokwa na damu kwa siku nyingi zaidi ya siku zake za mwezi, au amekuwa na damu inayoendelea zaidi ya kipindi chake, atakuwa najisi kwa kipindi chote cha shida hiyo, kama ilivyokuwa katika siku za hedhi yake."

Walawi.15.19-25.NENO

OUR GOD YAHWEH IS GOOD.

HIS LAWS ARE GOOD.

PRAISE THE LORD!
Covax ERTUGRUL BEY adriz naombeni mlete nondo zenu zilizoshiba hivi
 
Back
Top Bottom