SoC02 Ukosefu wa ajira unavyotoa fursa kwa wapigaji (matapeli)

Stories of Change - 2022 Competition

samwely1

Member
Jan 2, 2014
12
3
UKOSEFU WA AJIRA UNAVYOTOA FURSA KWA WAPIGAJI (MATAPELI)

Kila mwaka vijana maelfu kwa maelfu wanahitimu vyuo vya kati pamaoja na vile vya elimu ya juu. Kundi hili ni wale wahitimu wa fani mbalimbali kama vile mafundi, walimu, madaktari, wahasibu, mahakimu, nakadharika. Wahitimu hawa, wanahitimu wakiwa na matarajio makubwa ya kuingia katika ajira rasmini mara tu wanapotoka vyuoni. Kwakuwa mfumo wetu wa elimu unamwandaa muhitimu kuajiliwa na si kujiajiri basi ni nadra sana katika watu 10 kupata 2 wenge lengo la kujiajiri baada ya kuhitimu masomo yao.

Hapo ndipo tatizo linapoanzia, soko la ajira linafurika utitiri wa wataalamu wa fani mbalimbali wakati uhitaji ama uwezo wa serikali, taasisi, viwanda pamoja na mshirika mbalimbali kuajiri ni mdogo kulinganisha na idadi ya wahitimu wa kila mwaka. Hali hii hupelekea idadi kubwa ya wahitimu wakibaki bila ajira rasmi walizozitarajia wakati wa kuhitimu kwao, hapa ndipo matarajio hewa yanapoibuka. Pamoja na wahitimu hawa kuwa na ujuzi stahiki katika fani zao walizozisomea lakini hichi peke yake hakiwi kigezo cha wao kuajirika katika kazi za za ndoto zao. Hapo ndipo wapigaji/matapeli wanapogeuka uhitaji huu wa ajira kuwa fursa kwao kujinufaisha.

Watu hawa wanapokuja hawaji na sura ya kitapeli, wanakuja na maarifa makubwa sawia na uwezo ama kuzidi uwezo wa wanaowalenga. Wao hubuni miradi mbalimbali wanayoileta kwa wahitaji kupitia mwavuli wa ujasiliamali, huku wakijua fika lengo lao si kutia fursa kwa vijana kujiajili bali kuwatapeli baada kuwaaminisha mradi wai utakavyowanufaisha. Miradi mingi ya kitapeli imewaliza vijana wengi wenye uhitaji wa ajira, wapo waliolizwa kupitia Qnet, ufugaji wa sungura, kilimo cha milonge, biashara mtandao na miradi mingine mingi.

Chukulia mfano wa wale walioingia kichwa kichwa kwenye mradi wa ufugaji sungura wakiaminishwa sungura mmoja atauzwa kati ya elfu 25 na 30, hawa waliaminishwa na matapeli wa mradi kuwa lipo soko barani ulaya lenye uhitaji mkubwa wa sungura hivyo wao kama mawakala wameamua kufungua shamba la uzalishaji wa sungura na kuwataka wanaohitaji kuwa wabia wa mradi kunua sungura wa mbegu kutika kwao.

Watu wakanunua kweli kweli sungura wa mbegu, wakafuga mwisho wa siku mawakala wale wakatoweka baada ya kujinufaisha kupitia kuwauzia wabia wao sungura wa mbegu. Wote walionunua sungura na wakawazalisha walikosa pa kuwapeleka. Huu ni utapeli wa kiwango cha juu. Uhitaji wao wa ajira ukawaponza.


NINI KIFANYIKE?

Kabla ya kusema nini kifanyike, tunapaswa kujiuliza hivi ni kweli hakuna Ajira? Ama ni mfumo wetu wa elimu unalemaza uwezo wetu wa kuwaza nje ya box? Pamoja na kuona wahitimu wengi wamebaki bila ajira lakini bado tunaendelea kuwaaminisha wanafunzi wetu kuwa wasome ili waajiliwe, wakati mtaani wapo wahitimu makundi kwa makundi ambao bado kupata ajira ni mtihani mkubwa.

Umefika muda sasa wa kubadilisha namna tunavyoandaa wahitimu wetu, lazima tuwaambie ukweli juu ya tafsiri pana ya neno ajira, lazima wafahamu ajira si ile inayokufanya uvae suti na tai tu ama kufanya kazi kiwandani na kusubiri mshahara wa mwisho wa mwezi. Lazima wajue ajira si lazima zitokane na serkali, mashirika ama taasisi fulani bali wanapaswa kujua ya kuwa ajira nyingi ni lazima zitokane na ubunifu pamoja na uwezo wa kuibadilisha changamoto kuwa kuwa fursa. Wakijua hivyo tutakuwa tumebadili namna ya kufikiri na hivyo tutakuwa tumetafuta muarobaini wa ukisefu wa ajira kwa kiasi kikubwa.

Pamoja na hayo, ni lazima sasa kilimo na ufugaji iwe ni ajenda ya pamoja kama taifa, hii ni pamoja na kuhakikisha kuanzia msingi mpaka elimu ya juu somo la kilimo na ufugaji linakuwa somo la msingi. Hii si tu itasaidia kuwapatia wanafunzi ujuzi wa kulima na kufuga kitaalam lakini Pia hii itasaifia kuwavutia wahitimu wengi kujikita katika kazi hizi kwakuwa huko ndiko fursa pekee ya ajira inakopatikana bila ya misukumano kama zilivyo kazi za ofisini.

Ili kulifanya eneo hili liwe la kuvutia zaidi ni lazima serikali ihakikishe upatikanaje wa wataalam wa kilimo na ufugaji wanapatikana mpaka ngazi za vijiji, sambambana na hilo ni lazima usambazaji wa pembejeo uwe wa kukidhi uhitaji. Lakini pia wizara ya kilimo lazima iwahakikishie wakulima na wafugaji hawa uhakika wa masoko ili mtu anapoingia huko asiwe na wasiwasi wa wapi atapata wateja wa anachozalisha

Kuhitimisha, tafsiri ya neno ajira lazima itafsiriwe kwa upana ili kuwafungua macho vijana wetu. Lazima tafsiri hii iwe wazi zaidi, wanatakiwa kujua na kuelewa kuwa ajira si lazima itokane na ulichosoma darasani bali ulichosoma darasani kikufungue fikra uone fursa zilizojificha. Hebu tujiulize, ni kweli hatuioni fursa kubwa katika kuzalisha mafuta ya kula ambayo tunaagiza zaidi ya tani laki 6 kwa mwaka?

Uwezo wetu wa uzalishaji wa ndani si zaidi ya tani 2.5 wakati uhitaji wa soko la ndani ni zaidi ya tani laki 8 kwa mwaka, Je hii si fursa ya kuwahamasisha vijana wetu kujikita katika kulima mazao kama karanga, ufuta na alizeti? Kama hatuioni hii kuwa fursa ambayo itatoa ajira maelfu basi bado maalifa yetu ya darasani hayajatusaidia. Pamoja na Mungu kutujaalaia ardhi kubwa, mito inatiririsha maji mwaka mzima lakini bado hatujaweza kuzitumia rasilimali hizi ipasavyo ndio maana tunalia kila siku ati ajira hakuna wakati ajira nyingi ziko kwenye kilimo.

Ili mvuto uwe mkubwa, urasimishaji wa sekta hii upewe kipaumbele. Mkulima asionekana mtu aliyeshindwa maisha kama inavyoonekanaa sasa katika mitazamo ya wengi. Kama upatikanaji wa mbegu bora, pembejeo kwa wingi, miundominu mizuri ya umwagiliaji, upatikanaji wa vifaa vya kilimo kwa urahisi na masoko ya uhakika basi sekta hii inakwenda kupunguza tatizo la ajira kwa kiasi kikubwa.

Lakini pia uwepo mkakati wa makusudi kumuwezesha kila kijana muhitimu anaeamua kujiiingiza katika kilimo kwa kuwapatia mikopo midogo midogo yenye riba nafuu, mikopo hii si lazima iwe pesa, inaweza kuwa mbegu, dawa, vifaa kamaa pawatila, majembe ya ng'ombe, trekta na vifaa vingine vya kilimo na ufugaji, hii itakuwa chambo kuwavutia wengi wapende kilimo
 
Kuna jambo lazima lifanyike, tukubali kua nchi yetu haiwez kutajiri woote nchini wenye diploma,Degree, masters, PhD cha msingi ni wasomi kutafuta plan B ili kujiajiri sasa.
 
Kuna jambo lazima lifanyike, tukubali kua nchi yetu haiwez kutajiri woote nchini wenye diploma,Degree, masters, PhD cha msingi ni wasomi kutafuta plan B ili kujiajiri sasa.
Ndio maana kwenye andiki langu nimesema ni nyema neno ajira litafsiliwe katika upana wake ili kuleta uelewa kwa watu kuwa ajira sio razima uajiliwe na serikali ama taasisi fulani bali ni kubadili changamoto kuwa fursa ya ajira
 
Back
Top Bottom