SoC03 Ukosefu wa ajira

Stories of Change - 2023 Competition

DicksonMasoud

New Member
Jun 4, 2023
1
1
UKOSEFU WA AJIRA

"Tunateseka kupita kiasi Africa, Tusaidieni, Tunamatatizo Africa. Tumepoteza haki zetu kama watoto. Tuna Vita na maradhi, hatuna chakula dah! tunahitaji Elim na tunaomba mtusaidie kupata elim ili nasi huku tuwe kama ninyi."​

Ni ujumbe unao patikana katika miili ya Yoguine na Fode, Hawa ni vijana kutoka Guinea waliofaliki wakati wakijalibu kukimbilia Ulaya kwa kujificha katika mataili ya Ndege kamailivyo nukuliwa na Dr. Dambisa kwenye utangulizi wa kitabu chake "DEAD AID"

Vijana hawa kutoka Guinea wanawakilisha kundi kubwa, mamia Kwa mamilioni ya vijana wa kiafrika walio katika tamaa ya kukosa ajira zenye tija, hadi kutamani kukimbia nchi zao. fungua ubungo kama ifuatavyo,

Dhana ya Ajira na ukosefu wa ajira.

  • Ajira ni shuguri yoyote ambayo mtu huifanya kwajili ya kujipatia kipato ama akiwa anamiliki shuguri hiyo au anafanya chini ya umiliki wa mtu mwingine.
  • Ukosefu wa ajira ni hali ya mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi kukosa kazi ya kufanya ama ya kwake mwenyewe au ya mwingine hali inayomfanya aendelee kutafuta kazi. (Taalifa ya Benki ya Dunia ya mwaka 2013)
Pia,

  • Ni hali ya mtu mwenye umri wa kufanya kazi kukosa kaz ya kufanya ama Yuko tayari Kwa kufanya kazi na hana kazi na abatafuta kazi. (shilika la kazi duniani (ILO) mwaka 2013)
  • Ukisefu na upungufu wa Ajila ni tatizo la ulimwengu mzima (Global problem) lakini tatizo hili nikubwa sana Kwa nchi zinazo endelea hasa Kwa nchi za Africa. Tanzania kama nchi iliopo chini ya jagwa la Sahara haiwezi kukwepa tatizo ili.
Ukubwa wa tatizo

  • Ukosefu wa ajira umewaathili Kwa sehemu kubwa vijana ambao ni watu wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 (kulingana na sela ya taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007). vijana zaidi ya lakin tisa (900,000) huingia kwenye soko la ajira Kila mwaka (Mo Ibrahim Foundation 2012) lakini uwezo wa soko kutoa ajira ni mdogo hivyo husababisha kutokuwepo na uwiano baina ya uhitaji (demand) na uwezo (supply).
  • kwa kuwa karibia asilimia 66 ya idadi ya watu ni vijana, basi ndio wanaokua waathilika wakubwa (sensa ya watu na makazi 2012)
Juhudi za serikali kukabiliana na tatizo.

  • kumekuwepo na juhudi mbalimbali zilizochukuliwa na zinazo endelea kuchukuliwa na serikali kukabiliana na changamoto hii. Mfano MKUKUTA -(ii) ulitambua ukosefu wa ajira kama jambo muhimu (key issue) na kuweka mkakati wa kupunguza kutoka asilimia kumi 10 mwaka 2008 mpaka asilimia 5 mwaka 2015
  • Ali kadhalika mpango wa maendeleo wa miaka mitano 5 ( five years development plan)mwaka 2015/2020 mkakati wa kiuchumi kuelekea nchi ya viwanda.


Sababu zinazo pelekea kuwepo na ukosefu wa ajira.

  • Uwezo mdogo wa kutambua na kutengeneza ajira.
  • vijana wengi wana uwezo mdogo wa kutambua fursa na hata wakifanikiwa kutambua wanakua hawana uwezo wa kuzibadili / tafsiri hizo fursa kua ajira. mfano; kua na ardhi yenye rutuba ni fursa lakini kuwa na elimu ya kilimo cha kisasa, umwagiliaji , pempejeo na zana imara zakisasa ni uwezo wa kutafsili fursa kua ajira.
  • serikali pia inao uwezo mdogo wa kutambua na kutengeneza ajira, Mfano badala ya kuwekeza sana katika sekta ya kilimo ambayo inauwezo wa kuajili watu wengi kuliko sekta nyingine yoyote, inawekeza sana kwingine.


  • Uwezo mdogo wa mifumo ya elimu kuwaandaa waajiliwa na wanaotaka kujuajili.
  • Mfumo wa elimu wa Tanzania hauna mchago kamilifu kwenye mambo muhimu yanayo changia kuongea au kukuza uwezo wa kuajiliwa ama kujiajiri katika ushindani. Mambo hayo ni ubunifu, kipaji (tarents), mitazamo (attitudes) na vipaumbele (interest). Mambo haya huibuliwa sana na masomo ya stadi za kazi, ufundi,kilimo na ufugaji na biashara, masomo hayapewi uzito ama yamefutwa kabisa.
  • Mfumo wa elimu Tanzania umejikita kujenga uwezo wa akili(intelligence quotient IQ) Zaidi ya (emotional quotient EQ) ambao ni uwezo wa kihisia. EQ humfanya mtu kuzitambua hisia zake na zewengine hivyo kuzitumia vizuri hisia Mahalia pa kazi (mutisa 2014)
  • ujasiliamali kama somo lisilo la lazima kwa watoto na wanafunzi.

  • Uwezo mdogo wa waajili unao sababishwa na uchumi mbovu wa nchi.
  • uwezo wa waajiliwa huenda sambamba na ukuaji wa uchumi wa nchi. Mfano; kuzolota kwa uchumi kuanzia miaka sabini (70's) ilipelekea viwanda vingi ambavyo vilikuwa na uwezo wakujitengeneza ajira Kwa wingi.
  • uwezo mdogo wa taasisi za fedha na namna ambavyo hazimnufaishi mwananchi wa kawaida, hasa katika suala la riba na kodi.
  • Umaskini, Kuna maskini wengi Leo kuliko ilivyokuwa miaka hamsini iliyopita, umaskini wa kipato na fikra umepelekea kuwepo na uwezo mdogo wa kutengeneza ajira.
Sababu zote hizi hupelekea kuwepo kwa nafasi (gap) kubwa kati ya mahitaji ya Ajira (demand) na uwezo wa kutoa ajira (supply)

Nini kifanyike

  • kufanya mageuzi makubwa katika mifumo ya elimu hasa katika mitaala ya elimu ili kuluusu masomo yatakayo mjenga mwanafunzi kijiandaaa kuajiliwa na kama ajila zitasuasua awe na uwezo wa kujiajiri. kuakikisha kuwa mfumo wa elimu unakwenda mbali zaidi hata kuzilenga sababu za kisaikolojia zinazomjenga mtu ambazo ni mtazamo (attitudes).
  • kwakuwa jambo la kuwa mbobevu (competent) ni jambo la kuchagua, vijana wengi wanatakiwa kufanya mambo ambayo yataongeza uwezo wao kama kusoma na kufanya tafiti.
  • serikali kuwekeza zaidi kwenye sekta zinazoweza kutengeneza ajira nyingi mfano kilimo na viwanda.
 
Back
Top Bottom