Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 6,860
- 12,291
Habari zenu wana JF wenzangu, ama baada ya salam ningependa sasa nijielekeze kwenye mada husika.
Ndugu wanajamii forum wenzangu, unapokuwa nje ya nchi mara nyingi unakumbana na changamoto nyingi kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki uliyowaacha nyumbani.
Hii ni kutokana na wao kuona, au kuamini kwamba unao uwezo wa kufanya kila kitu kwao. Na kibaya zaidi hata utapojaribu kufanya baadhi ya vile unavyoweza kufanya bado utaendelea kubebeshwa lawama tu, ili mradi wahakikishe kuwa wew hauwezi ukaishi bila lawama zao.
Mwaka 2019 before corona nilikwenda bongo nikanunua kiji eneo maeneo ya salasala. Mpaka hapo tayari nilikuwa na eneo langu lingine ambalo tayari nimeshajenga kule Kigamboni, sehemu fulan inaitwa yebo yebo. Ila mimi binafsi nilipojaribu kupalinganisha Kigamboni na Salasala maeneo niliyonunua mimi, niliona kwamba Salasala ndio panafaa kuwa makazi yang ya kudumu pindi ntaporudi kuishi bongo mpaka pale muumba ataponichukua.
Kwahiyo nilivyorudi kaburu ikabidi nianze jitihada za ujenzi kule Salasala ili nishushe mjengo nitakaoishi mimi na familia yangu afu ile nyumba ya Kigamboni nitaipangisha. Kwa sasa kule yebo yebo Kigamboni anaishi brother wangu ambae na yey ana kiwanja chake huko huko Kigamboni anajenga, kwahiyo wakati namalizia mjengo wangu wa Kigamboni aliniomba akae kwanza kwa muda ili awe karibu na shughuli yake ya ujenzi afu nyumba yake ikishaisha ndo atapohama na kuniachia nyumba yangu nipangishe, nkasema haina noma bro.
Sasa basi ujenzi wa Salasala niliuanza mwaka 2020 nikitarajia kuwa katikati ya mwaka huu wa 2022 niwe nimeshamaliza afu ikiwezekana mwezi wa 12 nikienda bongo likizo iwe ndo kimoja nisirudi tena Kaburu. Cha kushangaza pamoja na jitihada zote nlizofanya lkn wanaosimamia mjengo wangu ndio wananikwamisha. Nyumba inaenda kimdondo sana mpaka inanikatisha tamaa kama ninaweza kuihamia mwishoni mwa mwaka huu.
Kabla ya kuanza ujenzi huu kuna watu walinishauri kwamba ni bora nimtume mama watoto aende kukaa bongo ili awe anasimamia shughuli za ujenzi kuliko kuwaamini ndugu tu pekee, mimi nikakaidi kwa kuona kuwa kamwe siwezi kumuweka mke wangu mbele ya ndugu zangu.
Sasa matokeo yake majuto ni mjukuu. Na mimi kuhamia Kigamboni staki naona kumenikalia kushoto sana aisee. Wana JF wenzangu mnaonaje, hivi mjengo huu unaweza kuisha kwa mwezi mmoja uliobaki kweli?
Maanake kuishi mbali na nyumbani kwa muda mrefu nako kunachosha.